Kwanini Dini za asili hazipewi nafasi?

Kwanini Dini za asili hazipewi nafasi?

Kama wewe si mfuasi wa hiyo unaita dini ya asili, huoni hadi wewe umeipuuza na kuitenga?
 
Kama wewe si mfuasi wa hiyo unaita dini ya asili, huoni hadi wewe umeipuuza na kuitenga?
Unajua nini maana ya ASILI mkuu?!

Pengine hufahamu nini maana ya asili, asili sio tusi, wala sio dhihaka, wala sio neno la kubeza kama labda unavyodhani mkuu,

Asili maana yake ni natural, kisicho ghoshiwa wala kuongezwa vitu vingine bandia, asili maana yake original, halisi,

Asili ni sifa na sio dhihaka! Asili ni sifa kubwa mkuu, mtu akisema una "ngozi ya asili maana yake hujatumia mikorogo ya bandia" akisema "chakula cha asili maana yake hakijaongezwa makemikali ya sumu ni chakula salama!"

Asili ni sifa kubwa mkuu, usichanganye na zile dhihaka za "kienyeji" sijasema dini za kienyeji,,,, neno kienyeji linatumika kama dhihaka Fulani, mfano mtu anakwambia unafanya mambo yako kienyeji sana! Maana yake hauna mpangilio wa kazi, unafanya mambo yako ovyo ovyo!

Asili ni sifa mkuu, sio dhihaka!
 
Mkuu Loyalist, heshima mbele!

Hata mimi sijachanganya asili na kienyeji, hakuna sehemu nimeandika namna hiyo.

Swali langu liko pale pale, kwa tafsiri yako kuwa asili ni heshima.... pengine ulitaka kumaanisha nini uliposema "wewe pia si mfuasi wa dini za asili"?
 
Kweli mkuu,,, nakumbuka hata kupiga nyungu (kujifukiza wakati wa covid - 19) watu walidai kuwa ni ushirikina?! Wakati ulaya na marekani kuna rooms za mvuke !

Na cha kushangaza zaidi, hizi dini zetu kubwa ukristo na uislam wanasisitiza sana kwenda kuhiji au kuzuru kwenye makaburi ya mitume na masharifu kule Israel na saudia wakidai utapata thawabu kiasi kwamba watu maskini wanadunduliza fedha hadi mamilioni ili tu kwenda kudhuru makaburi hayo,

wakati huohuo wanatukataza hata kwenda kuyafanyia usafi na kuyajengea makaburi ya babu zetu na ndugu zetu ili kudumisha kumbukumbu zao zisipotee, kwa madai kwamba hiyo ni haramu na ni ibada ya mizimu! Hata kama lengo lako ni kwenda tu kuyafanyia usafi na si vinginevyo!

Sasa najiuliza hivi inakuwaje kwenda kutembelea makaburi ya babu zetu na ndugu zetu kule kijijini na kuyafanyia usafi ni haramu na ushetani na ni ibada ya mizimu lakini kukusanya mamilioni ya fedha kwenda kutembelea au kuzuru makaburi ya hao wa Israel au saudia ni thawabu (wanaita kuhijji na sio ibada ya mizimu) na sio ushetani kama kwenda kutembelea nakusafisha haya makaburi ya ndugu zetu?!
This is point
 
Mkuu Loyalist, heshima mbele!

Hata mimi sijachanganya asili na kienyeji, hakuna sehemu nimeandika namna hiyo.

Swali langu liko pale pale, kwa tafsiri yako kuwa asili ni heshima.... pengine ulitaka kumaanisha nini uliposema "wewe pia si mfuasi wa dini za asili"?
Sawa kabisa mkuu, swali zuri kabisa, ungeuliza hivyo mwanzo ningekujibu directly! Ila hitimisho lako kwamba " huoni na wewe kuiita dini ya asili umeipuuza dini hiyo?! Ndio nikakujibu kuiita asili sio kuipuuza Bali ni kuiheshimu maana asili sio tusi Bali ni sifa!

Any way turudi kwenye swali lako la sasa mkuu wangu:

"Pengine ulitaka kumaanisha nini kusema wewe pia sio mfuasi wa dini ya asili!"

Swali zuri mkuu na rahisi sana:

Mosi: ni kweli Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini ya asili (japo kwetu mila zipo, lakini ni mila tu sio dini au imani ya asili).

Siwezi kudanganya watu hapa jamiiforum kuwa Mimi ni muumini au mfuasi wa dini ya asili wakati sikweli (msemakweli ni mpenzi wa Mungu). Pia kusema sio mfuasi japo ni ukweli lakini itaondosha dhana, narudia "dhana" ambapo watu wengine hudhani labda napigia debe dini yangu ya asili. Nope!

Pili: lengo la kuleta mada hii sio kwasababu ya kuipigia debe dini / imani ya asili, la hasha! Wala sio kuonyesha kuwa dini /imani nyingine ni mbaya (ukristo, uislam, Buddha n.k.) hapana!

*Lengo lilikuwa ni kutoa haki, narudia "haki" kwa mujibu wa katiba yetu! Katiba yetu inasema taifa letu ni secular halina dini Fulani rasmini, hivyo kila dini au imani inapaswa kupewa haki sawa mbele ya katiba bila kujali ni dini kubwa au ndogo. Sasa hoja ilikuwa kwanini dini ya asili haipewi haki ya kufanya Maombi kwenye mikutano ya kitaifa kama dini za kikristo na kiislam?! Kwani Tanzania ni nchi ya kikristo au kiislam tu?! Basi tubadili katiba na kuandika dini rasmini za Tanzania ni uislam Na ukristo!

Nilichokuwa nashangaa ni kuto kutoa haki, yaani haki, haki, haki, hivi ingekuwaje kama kwenye mikutano ya kitaifa dini ya kiislam au kikristo isingekuwa inajumuishwa kuliombea taifa?! Nadhani watu wa imani hizo wangelalamika sana! Sasa kwanini dini za asili zinatengwa na kunyanyapaliwa makusudi?! Kinyume cha katiba yetu?! Tanzania haina dini rasmini hivyo imani za asili nazo zipewe heshima yake na haki zao kitaifa kama dini nyingine!

Ndio hoja ya msingi mkuu,, hivyo Mimi kuwa muumini/mfuasi au kutokuwa muumini wa dini ya asili sio jambo la maana sana, hoja ni kwanini haki ya kikatiba ya dini ya asili inapuuzwa kitaifa?! Maana kila mtu ana haki ya kupigania haki ya mwingine hata kama yeye sio muathirika/ muhanga wa moja kwa moja mkuu!
 
Mkuu, dini za asili au za jadi hazinaga majina kama brand za kibiashara, maana hizi za kikoloni za kuletwa na meli na majahazi zina majina mengi,

Kila kabila au jamii inaijua dini yake au imani yake, iliyokuwa inaifuata kabla ya kufika kwa wageni wa mwanzo, waarabu, wazungu na wahindi hata Wachina (Buddha, Tao nk).

Ukisema utaje majina sidhani kama tutaelewana au hata thread itatosha hii, majina ya dini za asili yako mengi kulingana na lugha ya kabila husika, mfano wazaramo, wachagga, wasambaa, wazigua, wangazija, wasukuma, wahaya,wamakonde, wamwela, wangoni, wayao, wagogo, wanyamwezi,waha,wangindo, wanyakyusa, n.k. kila kabila lilikuwa na imani yake au dini yake waliyokuwa wanaitumia kufanya ibada na Maombi kwenye matukio mbalimbali mfano:

majanga ya asili kama ukame (wanapoomba mvua), kubariki watoto wanapozaliwa, jando na unyago, ndoa, mavuno, ugonjwa hata vita!
Unachanganya imani,dini na mila/tamaduni.

Hayo mambo unayosema kwenye hayo makabila yetu sio dini ni tamaduni au mila zenye kuambatana na imani mbalimbali.
 
Nimeshawahi kuleta mada inafanana hivi kuwa hapa nchini kuna watanzania wenzetu ambao wana asili ya Asia.Wana dini yao inaitwa Hindu pia wapo Sikh na pia Buddha.Kwanini wako nyuma ya pazia kwenye kuliombea taifa au hafla za kitaifa nao hawajitokezi ilhali ni watanzania wenzetu?

JIBU NI RAHISI MTOA MADA NAOMBA NILIANDIKE INFERIORITY COMPLEX KWA DINI ZA ASILI NA DINI AMBAZO SIO ZA IBRAHIM(ukristo na uislam)
Ni nyerere tu alivyofariki mkuu wa dini ya Hindi Nyerere alipokuwa anaombewa naye alijitokeza akamuombea.

Naomba nimnukuu askofu Desmond Tutu ''Wakoloni walivyokuja tulikuwa na dini zetu wakatuletea biblia.Wakatuambia tufunge macho tuombe.Tulipofunga macho na kuomba baada ya kufungua tu tukakuta wamechukua ardhi yetu na sisi tumebaki na biblia''-------mwisho wa kunukuu
Wahindi sio ndugu zetu hebu toa ushamba wa wazungu waarabu na wazungu kichwani mwsko
 
Kiongozi eti kuzidharau dini zetu za kiasili ni kasumba''HAPANA SIWEZI NARUDIA TENA HAPANA''sitaki uniaminishe katika miungu Hivi unajua hizi madhabahu za ukoo jinsi zinavetesa watu wewe watu wanawekewa vikwazo wanashindwa kuishi katika ndoto zao kwa ajili ya maagano ya giza walioingia mababu zao miaka na miaka roho za magonjwa,ufukara,utasa/ugumba kwanini tuishi nje ya misingi ya baraka MUNGU alizotuwekea...Kilichotokea pale msalabani ni pigo kubwa kwa shetani(NA YOTE IMEKWISHA)Yani tumekombolewa rejea "Eeeh BABA WASAMEHE KWAKUWA HAWAJUI WALITENDALO" lakini sio kwamba shetani kafungwa minyororo la hasha hapana ndio maana ana hasira zaidi so usishangae mabaya yanayotekea.Nimechoka kidogo tupo pamoja
Zilimtesa Nani
 
Kiongozi eti kuzidharau dini zetu za kiasili ni kasumba''HAPANA SIWEZI NARUDIA TENA HAPANA''sitaki uniaminishe katika miungu Hivi unajua hizi madhabahu za ukoo jinsi zinavetesa watu wewe watu wanawekewa vikwazo wanashindwa kuishi katika ndoto zao kwa ajili ya maagano ya giza walioingia mababu zao miaka na miaka roho za magonjwa,ufukara,utasa/ugumba kwanini tuishi nje ya misingi ya baraka MUNGU alizotuwekea...Kilichotokea pale msalabani ni pigo kubwa kwa shetani(NA YOTE IMEKWISHA)Yani tumekombolewa rejea "Eeeh BABA WASAMEHE KWAKUWA HAWAJUI WALITENDALO" lakini sio kwamba shetani kafungwa minyororo la hasha hapana ndio maana ana hasira zaidi so usishangae mabaya yanayotekea.Nimechoka kidogo tupo pamoja
Wewe unabeba kama yalivyo ndipo unapokosea...

Kwani yesu hakutoka kwenye ukoo!? Biblia nzima inaongelea ukoo wa yesu.. kuwa na ukoo kunakosa gani!?

Ikiwa sisi sote ni wa Abrahamu je hii dini tuliyonayo ni ya ukoo!? Au sio ya ukoo!?

Maombi yalikuwa ni kwa Mungu.. waafrika wote katika tamaduni na dini zao waliomba kwa Mungu wote kwa majina yao... Aliyesema tuombe kwa jina la Yesu ni nani!? Ikiwa ukristo ni kufanana naye.. na yeye hakuwahi kuomba kupitia jina la Yesu kwanini sisi tunaomba kupitia jina la Yesu!?

Mungu ameonya, tusijifanyie miungu mingine je sisi kumpa uzito yesu ambaye alipaswa kuwa mfano kwetu tunamkosea Mungu au ni sawa!?

Je ninaweza kuomba kwa jina la babu yangu!? Ikiwa Mungu alitenda makuu ndani yao ya kushangaza na kustaajabisha.. ninaweza kuwataja mf. Ahsante Mungu wa James, Wa Marieta wa Juma...... Nk. Kama siwezi kwann... Maana waliishi kabla ya utandawazi na kufikiwa na habari za Yesu... Ninahaki ya kuamini Mungu aliendelea kuwatunza hata wakati huo au Mungu wa kweli ni mpaka tu usikie habari zake ndio anakuwa active maishani mwako!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wakuu?

Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu sana, hasa inapokuja kwenye suala la mikutano au hafla za kiserikali, taasisi au hata siasa!

Nchi yetu inafahamika kwa kufuata Sera ya secularism, yaani nchi isiyofuata dini rasmi, nchi ambayo kila mwananchi ana imani yake binafsi, hakuna dini Moja rasmini ya kitaifa!

Lakini jambo linaloniumiza kichwa sana ni kwamba kwanini kwenye hafla, mikutano au mikusanyiko ya kitaifa, kisiasa au mingineyo viongozi wa dini zetu za asili hawapewi nafasi ya kufanya Maombi kama dini nyingine hususani uislam, ukristo au hata uhindu?

Nashindwa kuelewa sababu hasa ya kuibagua imani hii, japo ni dini zetu za asili kabla hata ya kuja imani hizi tulizoletewa na wakoloni (waarabu na wazungu) lakini cha kushangaza ni vigumu sana kukuta viongozi wa dini zetu za asili wakipewa nafasi ya kufanya Maombi kama wenzao wa dini ya Kikristo na Kiislam?

Tatizo ni nini?! Bado tunakasumba za kuthamini sana vitu vya kikoloni kuliko vyetu kama Tulivyo aminishwa na wakoloni kwamba ni dini za kishenzi au ni dini hizo kukosa wawakilishi wao rasmi ni?

Maana hata kwenye mikutano ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 28 October 2020 sijawahi kuona chama chochote kikianza kwa kuwapa nafasi viongozi wa dini za asili, zaidi ya viongozi wa dini za kiislam, kikristo na kihindu kidogo!

NB: Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini za asili.

Lakini kama tunajinasibihisha kuwa nchi yetu haina dini je, hatuoni kwamba tunafanya ubaguzi kwa kuwatenga na kutowapa nafasi viongozi wa dini za asili?

Tena tunaonekana kama bado tunakasumba za kupuuza vitu vyetu wenyewe na kuthamini zaidi vitu vilivyoletwa na wageni?
Uzi mzuri huu
 
Back
Top Bottom