Mkuu wewe ndio unachanganya kuhusu mila, tamaduni na imani, hebu tuangalie nini tofauti ya hivi vitu dini, mila na tamaduni.Unachanganya imani,dini na mila/tamaduni.
Hayo mambo unayosema kwenye hayo makabila yetu sio dini ni tamaduni au mila zenye kuambatana na imani mbalimbali.
Mkuu hoja ni kwamba Tanzania hatuna dini rasmini kila dini ina haki ya kuwakilishwa kwenye hafla za kitaifa,Dini za zamani unazoziita dini za asili zimejaa mila potofu,
Kwahiyo usijisumbue kuzitetea hazina maana zina ujinga tu mtupu.
Mtu akivaa kanzu je hilo ni vazi tuu!? Au kiashiria cha dini!?Wewe unabeba kama yalivyo ndipo unapokosea...
Kwani yesu hakutoka kwenye ukoo!? Biblia nzima inaongelea ukoo wa yesu.. kuwa na ukoo kunakosa gani!?
Ikiwa sisi sote ni wa Abrahamu je hii dini tuliyonayo ni ya ukoo!? Au sio ya ukoo!?
Maombi yalikuwa ni kwa Mungu.. waafrika wote katika tamaduni na dini zao waliomba kwa Mungu wote kwa majina yao... Aliyesema tuombe kwa jina la Yesu ni nani!? Ikiwa ukristo ni kufanana naye.. na yeye hakuwahi kuomba kupitia jina la Yesu kwanini sisi tunaomba kupitia jina la Yesu!?
Mungu ameonya, tusijifanyie miungu mingine je sisi kumpa uzito yesu ambaye alipaswa kuwa mfano kwetu tunamkosea Mungu au ni sawa!?
Je ninaweza kuomba kwa jina la babu yangu!? Ikiwa Mungu alitenda makuu ndani yao ya kushangaza na kustaajabisha.. ninaweza kuwataja mf. Ahsante Mungu wa James, Wa Marieta wa Juma...... Nk. Kama siwezi kwann... Maana waliishi kabla ya utandawazi na kufikiwa na habari za Yesu... Ninahaki ya kuamini Mungu aliendelea kuwatunza hata wakati huo au Mungu wa kweli ni mpaka tu usikie habari zake ndio anakuwa active maishani mwako!?
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wakilioitwa ni wale wenye ushawishi mkubwa wa watu na wanafahamika na hasa viongozi hunafahamika.Mkuu hoja ni kwamba Tanzania hatuna dini rasmini kila dini ina haki ya kuwakilishwa kwenye hafla za kitaifa,
Kuhusu upotofu au usawa wa imani husika inategema kwayule anayeiamini, kila dini ni nzuri kwake yeye anayeiamini, na sio lengo la mada hii kutafuta hasa dini gani ni ya haki au potofu, lengo ni kwanini dini nyingine zinabaguliwa kwenye uwakilishi kwenye mikutano au hafla za kitaifa?!
Mkuu hoja sio ushawishi mkuu wangu, hoja ni haki yao ya kikatiba, katiba inatoa haki kwa dini zote kutambulika na kuheshimika na kujumuishwa katika taifa.Wakilioitwa ni wale wenye ushawishi mkubwa wa watu na wanafahamika na hasa viongozi hunafahamika.
Sasa wanao ongoza matambiko ya asili nani anawajua???? na wana ushawishi kwa watu wengi????
Hafla gani ya kitaifa unayoisema wewe, utaitwa wakati hutambuliki kama upo??????????Mkuu hoja sio ushawishi mkuu wangu, hoja ni haki yao ya kikatiba, katiba inatoa haki kwa dini zote kutambulika na kuheshimika na kujumuishwa katika taifa.
Haisemi "watu au viongozi kwenye dini zenye ushawishi" ndio wana haki ya kuitwa kwenye mikutano ya kitaifa! La hasha, Bal dini zote zina haki ya kutambuliwa, kuheshimika na kujumuishwa katika hafla za kitaifa hiyo ni haki yao ya kikatiba na hakuna mtu anayeweza kuwapora mkuu wangu!
Ndugu sio kweli kama hawatambuliki kama wapo, Raisi akiapishwa Uwanja wa taifa, utaona angalau wanamualika kiongozi wa mila Uwanja wa taifa, wengine humpa Rais ngao na mkuki,Hafla gani ya kitaifa unayoisema wewe, utaitwa wakati hutambuliki kama upo??????????
Unaitwa vip wakati hata haijulikani unapatikana wapi???
Ni dini ipi hiyo wew mfano unaona imesahaulika???
Upotofu wake ni upi!?Dini za zamani unazoziita dini za asili zimejaa mila potofu,
Kwahiyo usijisumbue kuzitetea hazina maana zina ujinga tu mtupu.
Haiwezekani kutoa nafasi kwa kila dini kwa kuwa dini ni nyingi mno. La sivyo tutakaa siku nzima tukiomba kabla ya mkutano kuanza. Kuna dini kama Hindu hawapewi nafasi kwa kuwa japo ni wengi kwa idadi lakini kiasilimia ni wachache. Wakristo na Waislamu ni zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Hao asilimia 20 zilizobakia ndiyo dini zingine, pamoja na zile za asilia. Wengi wape. Hakuna nia mbaya kwa dini zingine zaidi ya Ukristo na Uislamu.Habari zenu wakuu?
Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu sana, hasa inapokuja kwenye suala la mikutano au hafla za kiserikali, taasisi au hata siasa!
Nchi yetu inafahamika kwa kufuata Sera ya secularism, yaani nchi isiyofuata dini rasmi, nchi ambayo kila mwananchi ana imani yake binafsi, hakuna dini Moja rasmini ya kitaifa!
Lakini jambo linaloniumiza kichwa sana ni kwamba kwanini kwenye hafla, mikutano au mikusanyiko ya kitaifa, kisiasa au mingineyo viongozi wa dini zetu za asili hawapewi nafasi ya kufanya Maombi kama dini nyingine hususani uislam, ukristo au hata uhindu?
Nashindwa kuelewa sababu hasa ya kuibagua imani hii, japo ni dini zetu za asili kabla hata ya kuja imani hizi tulizoletewa na wakoloni (waarabu na wazungu) lakini cha kushangaza ni vigumu sana kukuta viongozi wa dini zetu za asili wakipewa nafasi ya kufanya Maombi kama wenzao wa dini ya Kikristo na Kiislam?
Tatizo ni nini?! Bado tunakasumba za kuthamini sana vitu vya kikoloni kuliko vyetu kama Tulivyo aminishwa na wakoloni kwamba ni dini za kishenzi au ni dini hizo kukosa wawakilishi wao rasmi ni?
Maana hata kwenye mikutano ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 28 October 2020 sijawahi kuona chama chochote kikianza kwa kuwapa nafasi viongozi wa dini za asili, zaidi ya viongozi wa dini za kiislam, kikristo na kihindu kidogo!
NB: Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini za asili.
Lakini kama tunajinasibihisha kuwa nchi yetu haina dini je, hatuoni kwamba tunafanya ubaguzi kwa kuwatenga na kutowapa nafasi viongozi wa dini za asili?
Tena tunaonekana kama bado tunakasumba za kupuuza vitu vyetu wenyewe na kuthamini zaidi vitu vilivyoletwa na wageni?
Hivi dini ya asili maana yake nini?Mimi ni mfuasi wa dini za asili dini za wazungu na waarabu ni dini za ma shetani
Kwenye dini kuna tamaduni na kuna imani ila huwezi kusema tamaduni ndio dini.Dini ni sehemu ya utamaduni
Hazina pesa mkuu kwani hazikusanyi Zaka wala Sadaka.Habari zenu wakuu?
Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu sana, hasa inapokuja kwenye suala la mikutano au hafla za kiserikali, taasisi au hata siasa!
Nchi yetu inafahamika kwa kufuata Sera ya secularism, yaani nchi isiyofuata dini rasmi, nchi ambayo kila mwananchi ana imani yake binafsi, hakuna dini Moja rasmini ya kitaifa!
Lakini jambo linaloniumiza kichwa sana ni kwamba kwanini kwenye hafla, mikutano au mikusanyiko ya kitaifa, kisiasa au mingineyo viongozi wa dini zetu za asili hawapewi nafasi ya kufanya Maombi kama dini nyingine hususani uislam, ukristo au hata uhindu?
Nashindwa kuelewa sababu hasa ya kuibagua imani hii, japo ni dini zetu za asili kabla hata ya kuja imani hizi tulizoletewa na wakoloni (waarabu na wazungu) lakini cha kushangaza ni vigumu sana kukuta viongozi wa dini zetu za asili wakipewa nafasi ya kufanya Maombi kama wenzao wa dini ya Kikristo na Kiislam?
Tatizo ni nini?! Bado tunakasumba za kuthamini sana vitu vya kikoloni kuliko vyetu kama Tulivyo aminishwa na wakoloni kwamba ni dini za kishenzi au ni dini hizo kukosa wawakilishi wao rasmi ni?
Maana hata kwenye mikutano ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 28 October 2020 sijawahi kuona chama chochote kikianza kwa kuwapa nafasi viongozi wa dini za asili, zaidi ya viongozi wa dini za kiislam, kikristo na kihindu kidogo!
NB: Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini za asili.
Lakini kama tunajinasibihisha kuwa nchi yetu haina dini je, hatuoni kwamba tunafanya ubaguzi kwa kuwatenga na kutowapa nafasi viongozi wa dini za asili?
Tena tunaonekana kama bado tunakasumba za kupuuza vitu vyetu wenyewe na kuthamini zaidi vitu vilivyoletwa na wageni?
Very trueKweli mkuu,,, nakumbuka hata kupiga nyungu (kujifukiza wakati wa covid - 19) watu walidai kuwa ni ushirikina?! Wakati ulaya na marekani kuna rooms za mvuke !
Na cha kushangaza zaidi, hizi dini zetu kubwa ukristo na uislam wanasisitiza sana kwenda kuhiji au kuzuru kwenye makaburi ya mitume na masharifu kule Israel na saudia wakidai utapata thawabu kiasi kwamba watu maskini wanadunduliza fedha hadi mamilioni ili tu kwenda kudhuru makaburi hayo,
wakati huohuo wanatukataza hata kwenda kuyafanyia usafi na kuyajengea makaburi ya babu zetu na ndugu zetu ili kudumisha kumbukumbu zao zisipotee, kwa madai kwamba hiyo ni haramu na ni ibada ya mizimu! Hata kama lengo lako ni kwenda tu kuyafanyia usafi na si vinginevyo!
Sasa najiuliza hivi inakuwaje kwenda kutembelea makaburi ya babu zetu na ndugu zetu kule kijijini na kuyafanyia usafi ni haramu na ushetani na ni ibada ya mizimu lakini kukusanya mamilioni ya fedha kwenda kutembelea au kuzuru makaburi ya hao wa Israel au saudia ni thawabu (wanaita kuhijji na sio ibada ya mizimu) na sio ushetani kama kwenda kutembelea nakusafisha haya makaburi ya ndugu zetu?!
Umezungumza vitu vingi ila nitagusia vichache.Mkuu wewe ndio unachanganya kuhusu mila, tamaduni na imani, hebu tuangalie nini tofauti ya hivi vitu dini, mila na tamaduni.
Tamaduni ni mambo yaliyorithishwa kwenye jamii kama amali ambayo jamii husika huyaenzi na kuyafuata mfano vyakula vya asili (kitamaduni) mfano ugali, makande,mtori,matoborwa,senene, ni baadhi ya vyakula vya kitamaduni (asili) pia kuna vinywaji kama ulanzi, mbege, chibuku, komoni, mnazi ,togwa n.k. ni vinywaji vya kitamaduni.
Pia kuna mavazi ya kitamaduni mfano wamaasai wanajulikana sana kwa mavazi yao ya kitamaduni, pia mavazi kama kanga, batiki n.k ni mavazi ya kitamaduni ya waafrika!
Pia kuna nyimbo za kitamaduni kwa makabila ya kiafrika na lugha zao, hivi ni vitu vingine chache tu vinavyofanya utamaduni.
Mila ni mambo yanayofanywa na jamii husika na kurithishwa kwa vizazi na vizazi katika kudumisha desturi zao mfano wa mila ni kama ukeketaji, kurithi wajane, kurithi mashamba, nk Mara nyingi mila huendana na tamaduni au desturi za jamii husika.
mfano wa mila ni hizo za kukeketa na kurithi wajane, (kuna mila nzuri na mbaya), kule kanda ya ziwa kuna mpaka mila za nyumba ntobi, pia mila za kutakasa wajane kwa kulala nao ili kuwatoa mikosi, pia kuna mila za wamaasai kulala na Mke wa mwenzio kwa kuchomeka mkuki mlangoni n.k.
Hizo ni mila na sio imani au dini, kukeketa na kurithi wajane au kuwatakasa kwa kulala nao, au nyumba ntobi, sio dini ni mila (tuko pamoja?!)
Dini ni imani juu ya Mungu au miungu (mizimu ) n.k. kupitia mfumo Fulani, inaweza isiwe Mungu mmoja, au isihusu mfumo rasmini lakini lazima ihusishe kuabudu yaani kufanya tendo la ibada,
mfano waislam hufanya ibada kwa Mungu wao Allah, wana mfumo maalum wa ibada kwenye mpangilio kulingana na imani yao, kupitia kwa mtume wao Muhammad S.A.W. na kitabu chao Quran. Hivyo uislam ni dini.
Wakristo pia hufanya ibada yenye mpangilio maalum kwa Mungu wao Yehova au Yahweh (jehova) , kupitia kwa Bwana wao Yesu Kristo kwa kutumia kitabu chao cha Biblia. Hivyo ukristo ni dini.
Wayahudi pia hufanya ibada kwa Mungu wao elohim(adonai) Yahweh kupitia kitabu chao cha Torati, na nabii wao Mussa. Na wanampangilio maalum wa kufanya ibada zao. Hivyo uyahudi ni dini pia.
Alikadhalika Budhaism, Hinduism, Taoism, Shintoism, nao pia wana taratibu zao, vitabu vyao na Mungu (miungu) yao hivyo hizo pia ni dini.
Dini za asili pia wanataratibu zao za KUFANYA IBADA kupitia kutoa kafara, matambiko, kula vyakula au kunywa, kujenga madhabahu chini ya miti mikubwa, makaburini, maporini, mashambani, vilingeni, n.k. wakiomba miungu yao kupitia mizimu (roho za mababu waliokufa) pamoja na vitu vingine. Wana tamka maneno maalum na wanampangilio maalum wa kufanya ibada zao hivyo HII SIO TAMADUNI NI DINI maana kufanya ibada sio tamaduni au mila Bali ni dini/imani
Sasa mkuu wa umetofauti mpaka hapo ya mila, tamaduni na dini?! Je, Umegundua kuwa wewe ndiye unayechanganya kati ya tamaduni, mila na dini/imani
Narudia kidogo hitimisho, Mila haina kufanya ibada kama kutambika, kutoa kafara ya mnyama au Ndege na kuomba makaburini, chini ya miti, vilingeni au sehemu maalum, mila ni matendo ya kurithishwa kwenye jamii/kabila Fulani mfano ukeketaji na kurithi wajane! Lakini dini inaweza kutumia kwenye mila na tamaduni, mfano ,wazee wa zamani walifanya IBADA KWA KUOMBA NA KUTAMBIKA kabla ya kufanya JANDO au KUKEKETA, baada ya MAVUNO n.k.
Pia ukiangalia mavazi ya waislamu kama kanzu , kofia na kilemba kwa wanaume au baibui kwa wanawake ni mavazi ya kitamaduni ya kiarabu! Lakini uenda sambamba na dini/imani ya kiislam!
Mavazi ya wachungaji, mapadre, maaskofu wa kikristo wanayovaa wakati wa ibada kama majoho makubwa, kuweka mishumaa madhabahuni, kuvaa kofia za kiaskofu, Pete na kushika fimbo ya Kichungaji ni utamaduni wa wazungu hasa ulitokea ulaya Roma (Vatican) lakini uenda sambamba na dini ya kikristo! Wachungaji au mapadre na maaskofu kuvaa Shari lenye kola maalumu shingoni kwa mbele ni utamaduni wa wazungu lakini uenda sambamba na dini/imani ya kikristo.
sasa wakati mwingine mila ,utamaduni na imani huenda pamoja mkuu!
Hivi unaonaje kama uislam au ukristo ungeachwa kushirikishwa kwa kisingizio cha dini zenye wafuasi/waumini wengi?! Pangetosha kweli?! Kumbuka hizo dini unazodai zinawaumuni wengi ni za kuja, zimeikuta dini yetu ya asili ya mtanzania hapa hapa!Ku
Haiwezekani kutoa nafasi kwa kila dini kwa kuwa dini ni nyingi mno. La sivyo tutakaa siku nzima tukiomba kabla ya mkutano kuanza. Kuna dini kama Hindu hawapewi nafasi kwa kuwa japo ni wengi kwa idadi lakini kiasilimia ni wachache. Wakristo na Waislamu ni zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Hao asilimia 20 zilizobakia ndiyo dini zingine, pamoja na zile za asilia. Wengi wape. Hakuna nia mbaya kwa dini zingine zaidi ya Ukristo na Uislamu.
Mkuu imani ipo ya aina nyingi sana, unaweza kuwa na imani ya kushinda mechi ya mpira kati ya simba na yanga. Au Barcelona na Real Madrid, imani ipo ya kushinda mtihani, imani ipo ya kushinda uchaguzi, kupata kazi, n.kUmezungumza vitu vingi ila nitagusia vichache.
Imani sio lazima ihusiane masuala ya dini au Mungu tu,mfano mie nikisema kuwa nina nguo yangu fulani nikiiva lazima nipate hela,hii ni imani na ni jambo langu binafsi halihusiani na dini wala Mungu. Hivyo imani pia inaweza kupatikana kwenye mila kama hapo uliposema kuwa kuna mila ya kulala na wajane ili kuwaondoa mikosi,hiyo hali ya kufikiri kuwa kulala na mjane basi mikos huondoka hiyo ni imani watu wenye hiyo mila huamini hivyo.
Na hayo uliyoita dini za asili kama matambiko na makafara n.k ni mambo ambayo yanategemea na jamii husika hivyo yanaingia kwenye mila sambamba na imani,huwezi kuita kuwa ni dini.
Dini inaenda mbali zaidi si masuala tu ya kuabudu na kuomba,dini inagusa hadi kwenye hayo masuala ya mila na desturi.
Mkuu dini na imani hayo ni maneno mawili tofauti,lazima ujue neno imani linasimama vp lenyewe na neno dini linasimama vp. Mtu akikuuliza "wewe ni imani gani?" haina maana moja kwa moja anaulizia dini,unaweza usiwe na dini ila ukawa unaamini Mungu tu au chochote ila hauamini dini.Mkuu imani ipo ya aina nyingi sana, unaweza kuwa na imani ya kushinda mechi ya mpira kati ya simba na yanga. Au Barcelona na Real Madrid, imani ipo ya kushinda mtihani, imani ipo ya kushinda uchaguzi, kupata kazi, n.k
Hapa tunaongelea imani yenye mlengo Wa dini, ndio mada husika, sasa ukienda kwenye imani yenye mlengo mwingine mfano siasa kuwa na imani na mgombea Fulani unatoka nje ya mada ambayo tunajadili imani yenye mlengo Wa dini na sio hizo imani nyingine kama ulizozitaja za kupata hela ukivaa nguo Fulani utakuwa unatoka kabisa nje ya mada, zingatia hili tunazungumzia imani kwa upande Wa DINI.
Pili kuhusu mitambiko na kafara ni matendo ya ibada, na ibada inahusisha imani, tamaduni na dini, nimeeleza kwakirefu sana namna ambavyo utamaduni Wa kanzu na baibui kwa waislam ulivyobeba tamaduni za kiarabu, nikaeleza pia majoho na kola za maaskofu, mapadre na wachungaji wakikristo zilivyobeba utamaduni Wa kizungu (Roman - Vatican) japo ndani ya tamaduni hizo kuna imani Na dini, Mara nyingi dini huenda sambamba na imani na utamaduni,,,,
Wazee wetu Wa mwanzo (our ancestors) walikuwa na njia zao za kumwabudu Mungu wao, wamaasai walimwita Ngai, wachagga walimwita Ruwa, wanyakyusa walimwita Kyala, n.k. pia waliomba kupitia Roho za wazee wetu waliotangulia kama mizimu, vinyamkera, warumu n.k.
Wazee wetu walifanya ibada zao kwenye misitu, chini ya miti mikubwa, mashamba, mawe makubwa, mapangoni, kando ya mito, visima, vilingeni n.k. wakitoa sadaka au kafara kwakufanya matambiko na ibada zao!
Hii ilikuwa DINI YAO dini ni mfumo ambao jamii fulani imejitengenezea ili kumwabudu, kumwomba na kumshukuru Mungu au miungu yao! Kwenye hili la kuwepo kwa dini za asili halina ubishi kaka, vitabu vyote vya kihistoria vinathibitisha hilo kwamba waafrika walikuwa na DINI ZAO ZA ASILI na bado zipo (mpaka leo) hata kabla ya kuwasili kwa wageni Wa kwanza (explorers) ,
Sasa mkuu wewe ukidai kuwa eti mitambiko na kafara sio dini Bali ni imani tu nadhani watu watakushangaa ina maana unapingana na watafiti wote na vitabu vyote vilivyoandikwa vinavyothibitisha kwamba WAAFRIKA WALIKUWA NA DINI ZAO KABLA YA KUWASILI KWA WAKOLONI BARANI AFRIKA. Tena ni kasumba mbaya sana ya kujidharau sisi wenyewe waafrika kwamba hatukuwa na DINI zetu mpaka tulipoletewa (kama vifurushi ) na hawa wakoloni weupe! Shame on us! Tusiwe brainwashed sanaaaa! Tujiheshimu hata kidogo jamani!
Na wenye dini za asili wanaweza kusema uislam na ukristo ni imani tu na sio dini nadhani itakuwa sio sahihi. Dini ni njia au mfumo wowote ambao watu wamejiamulia kumwabudu Mungu wao hata kama wanaabudu Jiwe hii ni dini, sio lazima dini iwe na majengo makubwa kama makanisa na misikiti, nguo rasmini za ibada au vitabu rasmini.