Loyalist
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 411
- 884
Habari zenu wakuu?
Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu sana, hasa inapokuja kwenye suala la mikutano au hafla za kiserikali, taasisi au hata siasa!
Nchi yetu inafahamika kwa kufuata Sera ya secularism, yaani nchi isiyofuata dini rasmi, nchi ambayo kila mwananchi ana imani yake binafsi, hakuna dini Moja rasmini ya kitaifa!
Lakini jambo linaloniumiza kichwa sana ni kwamba kwanini kwenye hafla, mikutano au mikusanyiko ya kitaifa, kisiasa au mingineyo viongozi wa dini zetu za asili hawapewi nafasi ya kufanya Maombi kama dini nyingine hususani uislam, ukristo au hata uhindu?
Nashindwa kuelewa sababu hasa ya kuibagua imani hii, japo ni dini zetu za asili kabla hata ya kuja imani hizi tulizoletewa na wakoloni (waarabu na wazungu) lakini cha kushangaza ni vigumu sana kukuta viongozi wa dini zetu za asili wakipewa nafasi ya kufanya Maombi kama wenzao wa dini ya Kikristo na Kiislam?
Tatizo ni nini?! Bado tunakasumba za kuthamini sana vitu vya kikoloni kuliko vyetu kama Tulivyo aminishwa na wakoloni kwamba ni dini za kishenzi au ni dini hizo kukosa wawakilishi wao rasmi ni?
Maana hata kwenye mikutano ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 28 October 2020 sijawahi kuona chama chochote kikianza kwa kuwapa nafasi viongozi wa dini za asili, zaidi ya viongozi wa dini za kiislam, kikristo na kihindu kidogo!
NB: Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini za asili.
Lakini kama tunajinasibihisha kuwa nchi yetu haina dini je, hatuoni kwamba tunafanya ubaguzi kwa kuwatenga na kutowapa nafasi viongozi wa dini za asili?
Tena tunaonekana kama bado tunakasumba za kupuuza vitu vyetu wenyewe na kuthamini zaidi vitu vilivyoletwa na wageni?