Kwanini Dini za asili hazipewi nafasi?

Kwanini Dini za asili hazipewi nafasi?

Achana na dini yako ukoo tu,kuna dini za wahindu,mabohora,budha n.k hizo ndizo mtoa mada anataka nazo zipiwe nafasi pia katika jukwaa la kitaifa.
Nimekuelewa mkuu si unamaanisha wale wanaoabudu tembo,nyoka,masanamu,ngombe n.k hii nchi huru na haki nakumbuka katika kampeni za Jiwe jimbo la KAWE kuna kiongozi mmoja wapo wa kati hizo dini alikuwepo maybe alikosa nafasi ya kupanda jukwaani kutokana na maudhui ya ibada zao au ufinyu wa waumini wao hapa nchini.Sifungamani cha chama chochote lakini kuna kauli Mgombea wa CCM akisema TZ ni ya raia wote husika hata wale wasio na dini.
 
Habari zenu wakuu?

Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu sana, hasa inapokuja kwenye suala la mikutano au hafla za kiserikali, taasisi au hata siasa!

Nchi yetu inafahamika kwa kufuata Sera ya secularism, yaani nchi isiyofuata dini rasmi, nchi ambayo kila mwananchi ana imani yake binafsi, hakuna dini Moja rasmini ya kitaifa!

Lakini jambo linaloniumiza kichwa sana ni kwamba kwanini kwenye hafla, mikutano au mikusanyiko ya kitaifa, kisiasa au mingineyo viongozi wa dini zetu za asili hawapewi nafasi ya kufanya Maombi kama dini nyingine hususani uislam, ukristo au hata uhindu?

Nashindwa kuelewa sababu hasa ya kuibagua imani hii, japo ni dini zetu za asili kabla hata ya kuja imani hizi tulizoletewa na wakoloni (waarabu na wazungu) lakini cha kushangaza ni vigumu sana kukuta viongozi wa dini zetu za asili wakipewa nafasi ya kufanya Maombi kama wenzao wa dini ya Kikristo na Kiislam?

Tatizo ni nini?! Bado tunakasumba za kuthamini sana vitu vya kikoloni kuliko vyetu kama Tulivyo aminishwa na wakoloni kwamba ni dini za kishenzi au ni dini hizo kukosa wawakilishi wao rasmi ni?

Maana hata kwenye mikutano ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 28 October 2020 sijawahi kuona chama chochote kikianza kwa kuwapa nafasi viongozi wa dini za asili, zaidi ya viongozi wa dini za kiislam, kikristo na kihindu kidogo!

NB: Mimi sio mfuasi wala muumini wa dini za asili.

Lakini kama tunajinasibihisha kuwa nchi yetu haina dini je, hatuoni kwamba tunafanya ubaguzi kwa kuwatenga na kutowapa nafasi viongozi wa dini za asili?

Tena tunaonekana kama bado tunakasumba za kupuuza vitu vyetu wenyewe na kuthamini zaidi vitu vilivyoletwa na wageni?
Wazungu na waarabu walituaminisha kuabudu na kutambika katika mizimu yetu ni uchawi,Wakati wazee wetu waliomba mizimu,na mvua zikanyesha,waliomba milima,na chakula kikaja,

Wakaja na vitabu kwa kivuli Cha kutufundisha ustaraabu,Wenyewe wakachukua ardhi,madini na kutupeleka utumwani zaidi ya miaka 600,

Leo hii mbembe akikutwa kigoma anajulikana Kama mkimbizi,Mzungu akionekana nchini anaitwa mwekezaji au mdau wa maendeleo,

Congo leo hii Kuna Vita kila kukicha na UN haifanyi Cha maana zaidi ya kufitinisha tu,wacongo wanapewa vyakula vya 'GMO' kutoka ulaya ili wapate cancer na saratani wafe waibiwe vizuri,

Viva Africa,Viva Tanzania.
 
Wazungu na waarabu walituaminisha kuabudu na kutambika katika mizimu yetu ni uchawi,Wakati wazee wetu waliomba mizimu,na mvua zikanyesha,waliomba milima,na chakula kikaja,

Wakaja na vitabu kwa kivuli Cha kutufundisha ustaraabu,Wenyewe wakachukua ardhi,madini na kutupeleka utumwani zaidi ya miaka 600,

Leo hii mbembe akikutwa kigoma anajulikana Kama mkimbizi,Mzungu akionekana nchini anaitwa mwekezaji au mdau wa maendeleo,

Congo leo hii Kuna Vita kila kukicha na UN haifanyi Cha maana zaidi ya kufitinisha tu,wacongo wanapewa vyakula vya 'GMO' kutoka ulaya ili wapate cancer na saratani wafe waibiwe vizuri,

Viva Africa,Viva Tanzania.
mizimu ni nn?
 
safi ancestors. uwezo huo wa kunyeshea mvua wanautoa wapi wakati wamshidwa hata kuzuia vifo vyao
Uwezo wa kusababisha mvua kunyesha na uwezo wa kujizuia kufa ni hoja mbili tofauti na hazitegemeani,Ni sawa tu na kusema "Aldolf Hitler amewaua wayahudi wengi,kwanini ameshindwa kujizuia yeye Kwenye kifo?".

You are welcome boss for another challenge [emoji39].
 
Point of correction-Uislamu si dini ya Waarabu, Ni dini ya Mwenyezi Mungu iliyokuwepo kabla ya kuumbwa kwetu, Soma Qur aan ujue
 
Uwezo wa kusababisha mvua kunyesha na uwezo wa kujizuia kufa ni hoja mbili tofauti na hazitegemeani,Ni sawa tu na kusema "Aldolf Hitler amewaua wayahudi wengi,kwanini ameshindwa kujizuia yeye Kwenye kifo?".

You are welcome boss for another challenge [emoji39].
yan pont ni hiv unamuambuduje mfu?
 
wat other says is anceators are like to te the messengers of their creator although the spirt of God is everywhere so it doesnt need messengers
I have not yet got the concept,

What do you mean BTW?
 
Mzungu ukristo
Muarabu uislamu
Mu asia buddha
Kuna jews ajili ya mataifa flan flan

Muafrica ni kama hastahili kuwa na dini yaani africa ni soko huria kutangaza dini zao.Sijui imekuaje kuaje mpk imani zetu zimekuwa ushetani na nguvu za giza. Ina maana sisi wazee wetu hawana jema,mizimu yetu tu ndo mashetani?mbona wahindi wanaabudu hadi ng’ombe!nyoka!watu!

Nadhani kuwa watu flani flani walijua dini zetu zinanguvu sasa wakataka kuzibadili lkn swali ni je tunawabadilishia tunawapa dini gani?????Pili,hawa wapuuzi walijua wakitufanya tuchukie utamaduni wetu na imani zetu halfu tukapenda za kwao ni rahisi sana kututawala.

Dini zinakuja ili tutawalike kirahisi na kimsingi Dini zote zinafundisha basics priniciple ambazo ni imani,msamaha,maombi,ibada,matendo mema yaani kifupi mpagani akifanya hayo ana nguvu sawa na mshika dini...

usizini inayozungumzia kwenye biblia ndo ile ile ya kwenye quaran sema tu lugha tofauti uwasilishaji tofauti.Ukweli huu unahitaji uwe na akili huru sana..

Leo hii hata kunywa dawa ya asili unaonekana mshirikina!!!unaonekana mshamba!
Ingekuwa vyema kama ungezitaja hizo dini za afrika ambazo tulikuwa nazo kabla ya hizo za kuja.
 
Ingekuwa vyema kama ungezitaja hizo dini za afrika ambazo tulikuwa nazo kabla ya hizo za kuja.
Mkuu, dini za asili au za jadi hazinaga majina kama brand za kibiashara, maana hizi za kikoloni za kuletwa na meli na majahazi zina majina mengi,

Kila kabila au jamii inaijua dini yake au imani yake, iliyokuwa inaifuata kabla ya kufika kwa wageni wa mwanzo, waarabu, wazungu na wahindi hata Wachina (Buddha, Tao nk).

Ukisema utaje majina sidhani kama tutaelewana au hata thread itatosha hii, majina ya dini za asili yako mengi kulingana na lugha ya kabila husika, mfano wazaramo, wachagga, wasambaa, wazigua, wangazija, wasukuma, wahaya,wamakonde, wamwela, wangoni, wayao, wagogo, wanyamwezi,waha,wangindo, wanyakyusa, n.k. kila kabila lilikuwa na imani yake au dini yake waliyokuwa wanaitumia kufanya ibada na Maombi kwenye matukio mbalimbali mfano:

majanga ya asili kama ukame (wanapoomba mvua), kubariki watoto wanapozaliwa, jando na unyago, ndoa, mavuno, ugonjwa hata vita!
 
Back
Top Bottom