Kiongozi eti kuzidharau dini zetu za kiasili ni kasumba''HAPANA SIWEZI NARUDIA TENA HAPANA''sitaki uniaminishe katika miungu Hivi unajua hizi madhabahu za ukoo jinsi zinavetesa watu wewe watu wanawekewa vikwazo wanashindwa kuishi katika ndoto zao kwa ajili ya maagano ya giza walioingia mababu zao miaka na miaka roho za magonjwa,ufukara,utasa/ugumba kwanini tuishi nje ya misingi ya baraka MUNGU alizotuwekea...Kilichotokea pale msalabani ni pigo kubwa kwa shetani(NA YOTE IMEKWISHA)Yani tumekombolewa rejea "Eeeh BABA WASAMEHE KWAKUWA HAWAJUI WALITENDALO" lakini sio kwamba shetani kafungwa minyororo la hasha hapana ndio maana ana hasira zaidi so usishangae mabaya yanayotekea.Nimechoka kidogo tupo pamoja
Kwanza sidhani kama umeelewa hoja yangu mkuu,,
Hoja ni kwamba Tanzania haina dini rasmini ya taifa, tuko pamoja?! Kila dini ina haki sawa mbele ya katiba yetu, tuko pamoja mpaka hapo?! Kwahiyo kwa mujibu wa katiba yetu kila dini ina HAKI SAWA YA KUSHIRIKISHWA KWENYE MATUKIO MBALIMBALI YA KITAIFA hii ndio hoja ya msingi mkuu,
Tatizo linakuja pale unapojadili hoja kwa mlengo wa dini yako, kwamba dini hii ya asili si nzuri, ni ya kishetani, yakichawi au inatuletea laana, heeeee!! Hakuna aliyekuuliza kama dini ipi ni nzuri, wala sio hoja ya hapa kujadili dini gani ya kichawi, kishetani au nzuri, hoja ni usawa wa kushirikishwa kikatiba!
Kuhusu uhalali au uzuri wa dini basi kila mtu atapigia debe dini yake mkuu, hivi kama wewe ni mkristo unataka kuniambia uhindu wanaoabudu ng'ombe, nyoka na miungu mingine ni nzuri kwa imani yako mpaka ishirikishwe kwenye mikutano ya kitaifa?! Mbona sasa huipingi hii dini ?! Uislam je,?! Ubudha wanaoabudu masanamu?! Mbona hizo husemi umeng'ang'ania dini asili ni mbaya?! Hizo nyingine kwa dini yako ni sawa?!
Na kama wewe ni muislam je, unadhani kushirikishwa kwa uhindu kwenye ibada za kitaifa ni haki?! Ukristo je?! Ubudha ?! Uislam unazikubali dini hizi kuwa ni za haki?! Mbona sasa mnashupalia dini ya asili tu jamani?! Hizo nyingine vipi?! Ni za haki?! Ndio maana nasema mmepandikiziwa kasumba mbaya sana ya "kujidharau" na kudharau vya kwetu kwamba ni uchawi mtupu na ushetani lakini vya wengine ni vitakatifu na vya haki! Ujinga mtupu! Absolutely nonsense!
Kila dini /imani ina mapungufu yake hata huo ukristo wako una mapungufu yake kuanzia kwenye mauaji ya vita nyingi sana za crusades ambapo malaki ya watu waliuawa ulaya na middle east, mpaka kutumia dini hiyo kama fimbo ya kututawala (submission) na kutubagua (wakidai kuwa Mungu alimlaani mtoto wa Nuhu aitwae Ham, hivyo kizazi cha waafrika weusi kimelaaniwa na Mungu), Tena ukristo wa leo baadhi ya madhehebu umeanza kuunga mkono ushoga na usagaji.!! uongo?!
Uislam vilevile kama ukristo, uliletwa na waarabu, wakatumia dini hiyo, kututawala kuanzia Zanzibar mpaka ukanda wote wa mwambao wa bahari ya Hindi, kuanzia somalia mpaka msumbiji, wakatesa babu zetu na kuwakamata watumwa: kwauchache referred wakina seyyid said, tip tip, abushir, n.k. wakatuuza watumwa huko kwao na kwenye mashamba ya wazungu, wakajenga mpaka masoko ya watumwa referred bagamoyo na zanzibar bila aibu wala soni,
wakati wote huo walikuwa na dini yao tayari,,, tena wakijifanya ndio dini ya haki, haki gani ya kuuza watu watumwa, kuwatesa na kuwapora ardhi zao na mali zao ndio haki hiyo?! bado sijaeleza vita kubwa kubwa za jihad ambazo zimeua na kuangamiza malaki ya watu kwajina la dini, achilia mbali vikundi vya kidini kama Al shabab, Al Qaeda, Taleban, Isis (daesh), Izbollah, Boko haramu na huko msumbiji tunaona kinachoendelea achilia mbali kule mkuranga, kibiti na rufiji kilichotokea?!
Yote hayo ni matokeo ya hizo unazoziita kuwa ni dini/imani za haki??????!!!! Haki gani hapo?!
Kila imani au dini ina mapungufu yake au mabaya yake mkuu, so don't try to underestimate some beliefs into your perspective!
Tujadili hoja ya msingi, Tanzania ni secular country haina dini rasmini ya kitaifa, vipi dini/imani za asili zipuuzwe kwenye mikutano ya kitaifa badala yake dini tulizoletewa na wakoloni ndizo zipewe kipaumbele!