Kwanini CCM imekubali kudhalilika? Kwamba bandari imebaki na Kitenge na Mwijaku kama watetezi? Na tunaona tupo njia sahihi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Thamani ya rasilimali zetu imeshushwa chini kutoka kwenye utetezi wa watu makini hadi kutetewa na chawa; chawa hawana hoja wana matusi na tunaamini tutapiga hatua ?

Ni fedhea kubwa sana kuona baraza la maaskofu na watetezi wengine wa rasilimali zetu wanakosa wasome wakuwajibu badala yake wazalendo wamebaki kitenge na Mwijaku. Nakubali wanayo haki kama watanzania ila siamini kama kwenye population ya watu milioni 60 hawa ndio wanaoonekana na serikali kwamba niwatetezi.

Hii ni kadhia kubwa sana kwa chama tawala kwamba hakina tena watu wanaofikiri sawasawa; hii yakukosa watu imeenda mbali zaidi pale ambapo mbunge anajiuzulu ubunge ili akagombee ubunge. Chama kikubwa kama CCM kimakosa watu wenye sifa za kugombea hata ubunge kwenye jimbo ? Tujiulize chawa wanatupeleka tunapotakiwa kwenda? Lini tutaanza kuandaa viongozi kama wanavyofanya vyama vingine vya siasa?
 
Wasomi wazalendo na wanaojitambua hawawezi kukosoa waraka wa Maaskofu maana upo upande wa wananchi. Mwijaku na Kitenge Wana chembechembe za upinde wa mvua, Kuna kiungo Cha mwili ambacho wanakitumia kufikiri,sio kichwa.
 
Thamani ya rasilimali zetu imeshushwa chini kutoka kwenye utetezi wa watu makini hadi kutetewa na chawa; chawa hawana hoja wana matusi na tunaamini tutapiga hatua ?

Ni fedhea kubwa sana kuona baraza la maaskofu na watetezi wengine wa rasilimali zetu wanakosa wasome wakuwajibu badala yake wazalendo wamebaki kitenge na Mwijaku. Nakubali wanayo haki kama watanzania ila siamini kama kwenye population ya watu milioni 60 hawa ndio wanaoonekana na serikali kwamba niwatetezi.

Hii ni kadhia kubwa sana kwa chama tawala kwamba hakina tena watu wanaofikiri sawasawa; hii yakukosa watu imeenda mbali zaidi pale ambapo mbunge anajiuzulu ubunge ili akagombee ubunge. Chama kikubwa kama CCM kimakosa watu wenye sifa za kugombea hata ubunge kwenye jimbo ? Tujiulize chawa wanatupeleka tunapotakiwa kwenda? Lini tutaanza kuandaa viongozi kama wanavyofanya vyama vingine vya siasa?

Inashangaza mno!

Hata Mwijaku vituko?!
 
Back
Top Bottom