Kwanini CCM iliwaacha wagombea bora ikatuletea Magufuli?

2015 nilikuwa nawashangaa wanaodai CCM imewauzia silaha muhim (Lowassa) CDM. Kwangu Mimi silaha muhim kuelekea uchaguzi ule ilikuwa ni kashfa za kifisadi. Ufisadi ndio ilikuwa silaha ya chama kuelekea ikulu. Kwa kumchukua Lowassa CDM iliitupa silaha hii muhim sana kwao,,, kama Dr. Slaa angegombea na Lowassa awe sapota mkubwa wa CDM JPM asingetoboa maana ana kashfa kadhaa za kifisadi lakin CDM kwa kuwa walimsimamisha Lowassa walikosa cha kusema kuhusu ufisadi na mpaka sasa hivi hawajui wafanye nini.
N huu ndio ukweli mchungu ambao CHADEMA hawautaki
 
Baada ya kusema hayo, hatukumsikia tena mpaka kifo chake kilipo fika - kilicho sababishwa na kushambuliwa na mbwa wake mwenyewe. Wakati mwingine kuweni na akiba ya maneno. Usije ukalipwa hapa hapa duniani kwa kuchongewa na mdomo wako.
Siyo kweli
 
Kwani kwenye huo mchakato Lowasa hakuwa CCM ..!!
Wewe mada yako inaongelea mambo ya nyuma hata kabla ya Lowasa hajaenda CDM....kutokumjumuisha hapo kunaonyesha ni jinsi gani uzi wako umeutoa kimahaba....na sio kiweledi.....!!
Wagombea wa CCM walikuwa zaidi ya 30 mbona huwaulizi unauliza Lowassa tu.
 
Membe aliyesema eti tusitumie maji ya Ziwa Victoria eti Kwa kuwa Misri wanayahitaji kuliko sisi ndo ulitaka awe raisi?.

Nilishangaa Membe kutuambia eti sisi tunapata mvua nyingi Kwa mwaka eti tusitumie maji ya Ziwa Victoria
 
Nina furahi kuona kuwa hata Chadema wana amini kuwa Rais bora lazima atoke CCM .....Huyo unae muona si bora wana CCM tulimuona ni bora..kuliko hao ulio wataja...
Usijali lakini baada ya 2025 tutawaletea bora mwingine pengine atatoka kwa hao unao waona bora...Lakini kwa sasa kwetu Magufuli ni bora kabisa na alipatikana kwa demokrasia.

KIDUMU CHAMA BORA CHA MAPINDUZI
Tatizo ni tume huru na si kwamba wagombea wa CCM pekee ndio wagombea wanaofaa.
 
Ali mohamed shein yupi unaye mzungumzia hapo!??

Huyu aliegombea kiti cha urais Zanzibar 2015 na kushinda!?

Au wapo wawili hawa watu!?
 
Kwanza naomba nikiri kuwa binafsi sikumchagua rais John Pombe Magufuli ingawa nilijua atashinda, sababu ni moja tu hakuwa mgombea bora.

Baada ya jina la Magufuli kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea, wazo la kwanza lililonijia kichwani ni kuwa wajumbe wa CCM walijali maslahi ya chama zaidi kuliko nchi, kuwa walichoangalia wao ni chama kwanza kibaki salama lkn si kuteua mgombea bora ili aje kuwa kiongozi wa watanzania wote na sio kiongozi wa CCM.

Nikajiuliza, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi kuzuia hili lisitokee, najua wasingeweza kupinga hadharani kutokana na maadili ya kazi lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia kwa vile walijua fika udhaifu wa Magufuli.

Nilitaraji CCM watuletee watu kama Balozi Mahiga, Asha Migiro au Membe wazoefu wa diplomasia za kimataifa. Nilitegemea watuletee watu waadilifu wasio na doa kama kina Agustino Ramadhan, Mizengo Pinda, mama Samia au Shein, angalau basi wangetuletea jasusi la kimataifa kama Kitine kupambana na hujuma za majirani zetu kwenye soko huria la uchumi.

Hivi kweli CCM walishindwa vipi kuteua angalau mmoja bora kati ya hawa wagombea 38 waliojitokeza?

1. Bernard Membe
2. Balozi Mstaafu Agustine Mahiga,
3. Mizengo Pinda,
4. January Makamba,
5. Balozi Amina Said Alli,
6. Profesa Mark Mwandosya
7. Mama Samia Suluhu
8. Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan,
9. Asha Rose Migiro.
10.Dk. Ali Mohamed Shein,
11.Dk. Hassy Kitine.

TUJISAHIHISHE, muda bado upo tusirudie makosa tena hapo 2020 tutajuta.

Mawazo huru kutoka kwa mwanaJF mzoefu Quinine.
Bavicha linaulizia mambo ya sisiemu na kuilaumu sisiemu, kituko.
Jiulize kwa nini nyie mliweka mtu mliyemuita fisadi?? Ndiye aliyesababisha JPM awe rais maana watanzania hawakutaka fisadi.
 
Nafuu wangetuletea Yule mkulima mkulima wa darasa la Saba CCM wangeonekana wanajali maslahi ya nchi na siyo maslahi ya chama.
 
Nina furahi kuona kuwa hata Chadema wana amini kuwa Rais bora lazima atoke CCM .....Huyo unae muona si bora wana CCM tulimuona ni bora..kuliko hao ulio wataja...
Usijali lakini baada ya 2025 tutawaletea bora mwingine pengine atatoka kwa hao unao waona bora...Lakini kwa sasa kwetu Magufuli ni bora kabisa na alipatikana kwa demokrasia.

KIDUMU CHAMA BORA CHA MAPINDUZI
2025 ni Makonda, aje kuwanyoosha kabisa kama rula.
 
Membe aliyesema eti tusitumie maji ya Ziwa Victoria eti Kwa kuwa Misri wanayahitaji kuliko sisi ndo ulitaka awe raisi?.

Nilishangaa Membe kutuambia eti sisi tunapata mvua nyingi Kwa mwaka eti tusitumie maji ya Ziwa Victoria

Mbona Yohana alisema yeye ajaleta teteko hivyo kila muhanga apamabane na hali yake, au umeyasahau ya wananchi anaowatawala atahakikisha baadhi wanaishi kama mashetani!?
 
Kwanza naomba nikiri kuwa binafsi sikumchagua rais John Pombe Magufuli ingawa nilijua atashinda, sababu ni moja tu hakuwa mgombea bora.

Baada ya jina la Magufuli kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea, wazo la kwanza lililonijia kichwani ni kuwa wajumbe wa CCM walijali maslahi ya chama zaidi kuliko nchi, kuwa walichoangalia wao ni chama kwanza kibaki salama lkn si kuteua mgombea bora ili aje kuwa kiongozi wa watanzania wote na sio kiongozi wa CCM.

Nikajiuliza, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi kuzuia hili lisitokee, najua wasingeweza kupinga hadharani kutokana na maadili ya kazi lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia kwa vile walijua fika udhaifu wa Magufuli.

Nilitaraji CCM watuletee watu kama Balozi Mahiga, Asha Migiro au Membe wazoefu wa diplomasia za kimataifa. Nilitegemea watuletee watu waadilifu wasio na doa kama kina Agustino Ramadhan, Mizengo Pinda, mama Samia au Shein, angalau basi wangetuletea jasusi la kimataifa kama Kitine kupambana na hujuma za majirani zetu kwenye soko huria la uchumi.

Hivi kweli CCM walishindwa vipi kuteua angalau mmoja bora kati ya hawa wagombea 38 waliojitokeza?

1. Bernard Membe
2. Balozi Mstaafu Agustine Mahiga,
3. Mizengo Pinda,
4. January Makamba,
5. Balozi Amina Said Alli,
6. Profesa Mark Mwandosya
7. Mama Samia Suluhu
8. Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan,
9. Asha Rose Migiro.
10.Dk. Ali Mohamed Shein,
11.Dk. Hassy Kitine.

TUJISAHIHISHE, muda bado upo tusirudie makosa tena hapo 2020 tutajuta.

Mawazo huru kutoka kwa mwanaJF mzoefu Quinine.
Mkuu, matumaini yako bado yapo CCM?.Je upinzani walituletea mgombea bora?.Au nao waliangalia maslahi yao?
 
Kwann chadema ilinunuliwa na mtu waliyetuaminisba kuwa n fisad kwa takriban 10 yrs na kubadil gia angan kumpa ridhaa ya kugombea urais ikiwatelekeza makada wake jangwan??
Mbona unatoka nje ya mada? Rudi kwenye mada
 
Nina furahi kuona kuwa hata Chadema wana amini kuwa Rais bora lazima atoke CCM .....Huyo unae muona si bora wana CCM tulimuona ni bora..kuliko hao ulio wataja...
Usijali lakini baada ya 2025 tutawaletea bora mwingine pengine atatoka kwa hao unao waona bora...Lakini kwa sasa kwetu Magufuli ni bora kabisa na alipatikana kwa demokrasia.

KIDUMU CHAMA BORA CHA MAPINDUZI
Hakuwa bora, ila mazingira ya kutaka kukomeshana yalipelekea apewe... KUNA WATU WALIMWAGA MBOGA, WENGINE WAKAONA ISIWE TABU, NAO WAKAMWAGA UGALI.... AKINA FUATA UPEPO WAKAAMUA KUMWAGA MAJI YA KUNAWA...
 
Baada ya kusema hayo, hatukumsikia tena mpaka kifo chake kilipo fika - kilicho sababishwa na kushambuliwa na mbwa wake mwenyewe. Wakati mwingine kuweni na akiba ya maneno. Usije ukalipwa hapa hapa duniani kwa kuchongewa na mdomo wako.
Mkuu umefanya Nicheke Kwa sauti. Akina ya maneno ni suala muhimu Sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom