Kwanini CCM iliwaacha wagombea bora ikatuletea Magufuli?

Sababu si hiyo mkuu ,magufuli aliuokota urais bila kutarajia,kilichotokea ni baada ya Lowassa kukatwa jina makusudi na kikwete,kikwete alikuwa anamtaka membe,sasa alipokatwa jina Lowassa ,usalama wa taifa waliokuwa kambi ya Lowassa wakatoa siri juu ya mil 750 zilizokuwa zimejaa kwenye mabegi zilizokuwa zimeletwa Dodoma na mhasibu wa manji maalumu kwa ajili ya kuwahonga wajumbe wa NEC ambao 85% walikuwa upande wa Lowassa ili wampitishe membe.
Baada ya siri kuvuja,mpango wa kikwete ukawa umeharibika,yakabaki majina matatu tu,1.Magufuli2.Amina 3.Migiro ndo kina mzee mwinyi na mkapa wakaona ni bora wampe magufuli tu,ila nyuma ya pazia ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa mkapa ambaye alikuwa akimtaka magufuli ila hakuwa na uwezo wa kuchezesha karata zaidi ya kupendekeza jina lake ktk mchujo wa awali.
Kwa kikwete ilikuwa ni siku mbaya sana kuwahi kumtokea maishani mwake,kikwete anamjua magufuli vizuri mno,hampendi kabisa,na hata kumpatia uwaziri ilikuwa ni shinikizo la mkapa tu,na utakumbuka jinsi alivyokuwa akimtupa wizara tofauti tofauti.
Dhambi inayomtesa kikwete ni kumkata Lowassa makusudi,kwanza kashfa ya Richmond ilikuwa ni ya kutengeneza tu,ili kumchafua Lowassa mapema akose hadhi na mvuto wa Kugombea urais,kikwete ni mtu mbaya sana,usimwone na tabasamu lake hilo,nina mengi ya kuongea,nikisema niweke uzi maalumu wa hili jambo,mods watafuta tu.
Masikini Manji.
 
Binafsi nilipofika kuchagua Rais niliacha wazi sikuona mtu anayefaa kuwa Rais jamaa waliyempa ni mbinafi sana na mpenda sifa mtu kama huyo hafai kabisa
 
Na safari ya Dodoma ndio imeanza rasmi. Ukitaka visa ya kwenda nje ya nchi panda bombardier au basi kuelekea Dodoma.

Wanasema usiyempenda kaja.
 
nadhani wanajuta wameingiza jini maana nchi sasa ni varu varu jamaa amelosto
 
Na jamaa mwenyewe anajua hakuwa CHAGUO LA WanaCCM, kwasasa yuko BUSY anatengeneza CCM YAKE TU NDANI YA CCM ( KUNDI LAKE TIIFU ) halafu anawapigia na kampeni kabisa. Refer Mahiga IRINGA.

Kilele ni 2019 kura ya MAONI CCM. Watu WATAKATWAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Kuna mwalimu mmoja alikuwa anafundisha darasa la vichaa , ulipofika muda wa kurudi watoto nyumbani yule mwalimu akafunga mlango halafu akachora ukutani mlango kwa chaki upande wa nyuma, akawaambia wanafunzi wake tokeeni mlango ule wa nyuma . Basi wale wanafunzi wakakimbili na kujazana pale mlango wa kuchorwa kila mmoja akilalamika nipishe nipite . Lakini mwanafunzi mmoja alibaki kwenye dawati. mwl akadhani yule aliyebaki kwenye dawati atakuwa amepona, akamsogelea na kumuuliza mbona wewe umekaa tu kwenye dawati hutaki kwenda nje.mwanafunzi Akamjibu unafikiri wale wanaweza kupita pale mlangoni, mwalimu akamuuliza kwa nini wasipite. Yule mwanafunzi akajibu funguo za ule mlango wa nyuma ninazo mimi.
Kuna wakati unaaweza ukamdhania mtu ndivyo sivyo
 
Walimjua fika Dr. John Magufuli - Kuwa Haambiliki!
Walimjua kabisa kuwa Daktari Jiwe hatishiki!
Walifahamu JP ni Mkali na Si Mpole!
Walijua kuwa Ni Mtu mwenye Caliber ya kipekee sana! - Get things done by any means necessary!
Walijua kuwa hapendi kupingwa pingwa hivi!
Walifahamu fika kuwa si rafiki sana wasiasa za mijadala!
Walifahamu kuwa Haipendi CCM!
Walifahamu kuwa yeye wapinzani kwake ni Rafiki zake wakubwa ...Hasa pale inapotokea hawampingi yeye.
Lakini bado Halmashauri Kuu ikamteua na Kumwamini kuipaisha CCM Juu!
JPM Tunyooshe Baba! we do feel The HEAT!
 
Yaan unatutajia membe?? Huna akili na hazikutoshi, alafu unataja Mark mwandosya, aliyeihujumu TTCL??? Unaumwa ukapimwe akili
 
Walimjua fika Dr. John Magufuli - Kuwa Haambiliki!
Walimjua kabisa kuwa Daktari Jiwe hatishiki!
Walifahamu JP ni Mkali na Si Mpole!
Walijua kuwa Ni Mtu mwenye Caliber ya kipekee sana! - Get things done by any means necessary!
Walijua kuwa hapendi kupingwa pingwa hivi!
Walifahamu fika kuwa si rafiki sana wasiasa za mijadala!
Walifahamu kuwa Haipendi CCM!
Walifahamu kuwa yeye wapinzani kwake ni Rafiki zake wakubwa ...Hasa pale inapotokea hawampingi yeye.
Lakini bado Halmashauri Kuu ikamteua na Kumwamini kuipaisha CCM Juu!
JPM Tunyooshe Baba! we do feel The HEAT!
Labda shetani kwenye alimashaur kuu ya ccm alkua kazni effectively
 
Kwann chadema ilinunuliwa na mtu waliyetuaminisba kuwa n fisad kwa takriban 10 yrs na kubadil gia angan kumpa ridhaa ya kugombea urais ikiwatelekeza makada wake jangwan??
Hivi wewe CDM inakuwasha sana pa unyeo? Maana mleta mada wala hajaitaja, Ila wewe, kama huna cha kuchangia kamtikisie unyeo jamaayako, nadhani yeye anauhitaji. Wanaume tukijadili mambo ya msingi utuache.
 
Kwanza naomba nikiri kuwa binafsi sikumchagua rais John Pombe Magufuli ingawa nilijua atashinda, sababu ni moja tu hakuwa mgombea bora.

Baada ya jina la Magufuli kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea, wazo la kwanza lililonijia kichwani ni kuwa wajumbe wa CCM walijali maslahi ya chama zaidi kuliko nchi, kuwa walichoangalia wao ni chama kwanza kibaki salama lkn si kuteua mgombea bora ili aje kuwa kiongozi wa watanzania wote na sio kiongozi wa CCM.

Nikajiuliza, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi kuzuia hili lisitokee, najua wasingeweza kupinga hadharani kutokana na maadili ya kazi lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia kwa vile walijua fika udhaifu wa Magufuli.

Nilitaraji CCM watuletee watu kama Balozi Mahiga, Asha Migiro au Membe wazoefu wa diplomasia za kimataifa. Nilitegemea watuletee watu waadilifu wasio na doa kama kina Agustino Ramadhan, Mizengo Pinda, mama Samia au Shein, angalau basi wangetuletea jasusi la kimataifa kama Kitine kupambana na hujuma za majirani zetu kwenye soko huria la uchumi.

Hivi kweli CCM walishindwa vipi kuteua angalau mmoja bora kati ya hawa wagombea 38 waliojitokeza?

1. Bernard Membe
2. Balozi Mstaafu Agustine Mahiga,
3. Mizengo Pinda,
4. January Makamba,
5. Balozi Amina Said Alli,
6. Profesa Mark Mwandosya
7. Mama Samia Suluhu
8. Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan,
9. Asha Rose Migiro.
10.Dk. Ali Mohamed Shein,
11.Dk. Hassy Kitine.

TUJISAHIHISHE, muda bado upo tusirudie makosa tena hapo 2020 tutajuta.

Mawazo huru kutoka kwa mwanaJF mzoefu Quinine.
Hebu sema shida yako ni nini, wenye uwezo wa kusaidia japo kwa mawazo waje front wakufariji kwasababu hii thread imekaa kama vile no.1 ameshaingilia mishe zako.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom