Kwanini CCM iliwaacha wagombea bora ikatuletea Magufuli?

Kwanini CCM iliwaacha wagombea bora ikatuletea Magufuli?

Uncle magu kawashika makagali yenu, viva nagu, love you magu
 
Mafisadi Mkapa na Kikwete walitaka fisadi mwenzao ili aendelee kuwalinda huku akijilinda na yeye kwenye ufisadi wake. Augustino Ramadhani angewalipua na pia kuruhusu katiba mpya ya rasimu ya Warioba.

Kwanza naomba nikiri kuwa binafsi sikumchagua rais John Pombe Magufuli ingawa nilijua atashinda, sababu ni moja tu hakuwa mgombea bora.

Baada ya jina la Magufuli kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea, wazo la kwanza lililonijia kichwani ni kuwa wajumbe wa CCM walijali maslahi ya chama zaidi kuliko nchi, kuwa walichoangalia wao ni chama kwanza kibaki salama lkn si kuteua mgombea bora ili aje kuwa kiongozi wa watanzania wote na sio kiongozi wa CCM.

Nikajiuliza, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi kuzuia hili lisitokee, najua wasingeweza kupinga hadharani kutokana na maadili ya kazi lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia kwa vile walijua fika udhaifu wa Magufuli.

Nilitaraji CCM watuletee watu kama Balozi Mahiga, Asha Migiro au Membe wazoefu wa diplomasia za kimataifa. Nilitegemea watuletee watu waadilifu wasio na doa kama kina Agustino Ramadhan, Mizengo Pinda, mama Samia au Shein, angalau basi wangetuletea jasusi la kimataifa kama Kitine kupambana na hujuma za majirani zetu kwenye soko huria la uchumi.

Hivi kweli CCM walishindwa vipi kuteua angalau mmoja bora kati ya hawa wagombea 38 waliojitokeza?

1. Bernard Membe
2. Balozi Mstaafu Agustine Mahiga,
3. Mizengo Pinda,
4. January Makamba,
5. Balozi Amina Said Alli,
6. Profesa Mark Mwandosya
7. Mama Samia Suluhu
8. Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan,
9. Asha Rose Migiro.
10.Dk. Ali Mohamed Shein,
11.Dk. Hassy Kitine.

TUJISAHIHISHE, muda bado upo tusirudie makosa tena hapo 2020 tutajuta.

Mawazo huru kutoka kwa mwanaJF mzoefu Quinine.
 
Uncle magu kawashika makagali yenu, viva nagu, love you magu
Sema tumeshikwa....

kwani CCM mna maduka yenu 'free duty shops for CCM members only', ambayo mnapunguziwa bei ya vyakula au LUKU za CCM ni tofauti na za watu wa Chadema.
 
Hiyo ni mada tofauti kabisa na yangu ungekuwa ni mtihani ungepata 0%.
Ninyi n nyan msioona kunduzenu

Mnajua kumpaka magu udikteta,na kuimba demokrasia, ila hammuon mwenyekiti wa kudum wa chama chenu

Mnajua kuona maajab ya magu kuupata ridhaa ya kugombea urais ccm hamuon maajab ya watu waliosema mtu anaemuunga mkono fisad lowasa n mwehu, mwendawazim alaf baadae akapewa ridhaa ya chadema hyo hyo kugombea urais

Now tel me nan ambaye kama n mtihan angepata 0

Mmekuww makasuku ndan ya chama chenu mnageuzwa geuzwa tu yan
 
Nina furahi kuona kuwa hata Chadema wana amini kuwa Rais bora lazima atoke CCM .....Huyo unae muona si bora wana CCM tulimuona ni bora..kuliko hao ulio wataja...
Usijali lakini baada ya 2025 tutawaletea bora mwingine pengine atatoka kwa hao unao waona bora...Lakini kwa sasa kwetu Magufuli ni bora kabisa na alipatikana kwa demokrasia.

KIDUMU CHAMA BORA CHA MAPINDUZI
Mkuu hao jamaa yan huwa hawajielew
Wanaenda enda tu
 
Ni vigumu sana kuona kosa ukiwa ndani ya system bali tulio nje ya system.
Hebu tupe orodha ya wagombea wa ridhaa ya urais chadema



Mwenzio katoa list ya watu kadhaa waliokatwa hadi akapatkana magu

Sasa na ww tupe list ya walioshindanishwa hadi mkampata lowasa alyekatwa ccm
 
Mkuu sababu umeshaisema mwenyewe, CCM walitaka chama kibaki Salama/madarakani, Na dio madhumuni ya chama cha siasa, Kwa maana hiyo hao 11 ulio wataja wasingekiacha chama salama.
Unategemea upate sababu nyingine?
Ishu true ni usalama wa chama hao wengine wasingeweza kupambana na nguvu ya upande wa pili na kweli chama kimepona sio uchumi, ila maana system iliyopo haina madhara na maslai yao kwao ni sawa hata kama wananchi wanabatizwa kwa moto kuokoa chama
 
Kwann chadema ilinunuliwa na mtu waliyetuaminisba kuwa n fisad kwa takriban 10 yrs na kubadil gia angan kumpa ridhaa ya kugombea urais ikiwatelekeza makada wake jangwan??
Mliaminishwa kumbe....... Kwa hiyo na nyinyi mkaaamini? Mbona na nyinyi alipokuwa kwenu hamkumuona kuwa ni fisadi mpaka alipo ondoka ndio mnajifanya kumuita ni fisadi. Kama ni fisadi dola si mmeshika nyinyi mbona hamumkamati? Mpaka leo kuna mahakama ya mafisadi mbona hamjampeleka? Shame on you
 
Hebu tupe orodha ya wagombea wa ridhaa ya urais chadema



Mwenzio katoa list ya watu kadhaa waliokatwa hadi akapatkana magu

Sasa na ww tupe list ya walioshindanishwa hadi mkampata lowasa alyekatwa ccm
Mwenzangu nani katoa list,

mimi ndiye nimetoa list ya wagombea bora wa CCM walioachwa tukaletewa Magufuli.
 
Mimi nilikata tamaa na huyu bwana pale aliponena haya:-
  1. Nilipoingia madarakani sukari kilo ilikuwa 5000
  2. Mv Dar es Salaam nimewakabidhi JW sasa jadilini kifaru cha jeshi
  3. Nitauza majengo yote ya serikali yaliyopo Dar(sijui mteja atakuwa nani na waya huu)
  4. Saddam Hussein ni Rais wa Kuwaiti( hapa nilijua kimataifa tumeshabugi)
  5. Fyatueni watoto elimu bure( alijua elimu ndio chakula na makazi)
  6. Nimemtuma Kinana kwenda kutibiwa India!!!
 
Katiba ya Tanzania ndio tatizo. Katiba inayotoa nafasi kwa rais tabia zake binafsi kuwa ndio muongozo wa sheria hapo ndio tatizo lililipo. Halafu hicho kifungu cha kutoshishitakiwa akiwa madarakani au akiwa ametoka, hapo ndipo lilipo tatizo la msingi. Leo rais akiingia mwizi ataiba mpaka achoke, akiingia rais mwenye kisirani atafanya atajavyo, akiingia rais mdini au mkabila atafanya hivyo bila hofu kwa sababu ya katiba ilivyo. Hao uliowataja ni kwa mtazamo wako, ila nao wana mapungufu yao, na watakapopata hicho cheo, kupitia udhaifu wa katiba watafanya watakavyo.

Cha kufanya kwasasa njia ambazo sio nzuri ni kutokea machafuko au mapinduzi kwani box la kura haliheshimiwi tena. Baada ya hapo ni lazima tutaandika katiba mpya ambayo itafanya kila mtu kuwa chini ya sheria kuanzia rais. Hapo tutaona taasisi zenye nguvu na sio mtu mwenye nguvu isiyohojika kiuhalisia.
 
Kwa sababu walisikia kilio cha watanzania na upinzani kuwa tunataka rais dikteta na mkali..Asiyechekacheka na asiyependa safari..Mwenye kufanya maamuzi magumu na asiyeogopa mtu
 
Back
Top Bottom