Mkwawa mnyalukoro
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 232
- 136
Baada ya kifo cha Rais Magufuli Chama cha Mapinduzi kimeingia katika Mtego mzito sana katika Siasa yake.
Mtego huu unatokana na Kifo cha Rais Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano akiwa Madarakani na kumpata Rais aliyetokana na Katiba.
Kisheria na taratibu za vyama vya Siasa Viongozi wa Kisiasa wanatakiwa wapitie katika mchakato wa chaguzi za ndani ya Chama kisha waje wagombee katika Uchaguzi unaoratibiwa na Tume ya Uchaguzi dhidi ya wagombea wengine wa vyama vya Siasa.
Rais Samia ameingia kwenye Kiti cha Urais bila kupitia mchakato huu wa chaguzi za ndani ya Chama dhidi ya wagombea wengine.
Mchakato huu wa chaguzi za ndani unasaidia Vyama kuchuja na kuruhusu wanachama kugombea ili kumpata mgombea bora zaidi miongoni mwao.
Kwa mfano
Mwaka 2015 ni miongoni mwa miaka migumu mno kwa Chaguzi za ndani ya CCM kwasababu wagombea walikuwa na nguvu kubwa ya kupitia makundi waliyoyatengeneza kwa fedha hata kufikia hatua ya Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kuimba jina la Lowassa badala ya kuimba jina la Mwenyekiti wa CCM wa kipindi hicho.
Uongozi wa CCM ulisimama imara na kuwaengua wagombea waliotengeneza umaarufu kwa rushwa na hatimaye wakamchagua mgombea bora miongoni mwao ambaye ni John Pombe Magufuli ili aende kupeperusha bendera yao,
Kuelekea Uchaguzi wa ndani wa CCM ili kupata wagombea watakaogombea katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 CCM itafuata Sheria ama utaratibu ili kumpata mgombea Urais?
Kama CCM itafuata Demokrasia na sheria basi tutegemee Rais Samia kupata washindani wake ndani ya Chama katika kuwania nafasi ya Urais ambapo Kidemokrasia itakisaidia Chama cha Mapinduzi kumpata mwanachama bora zaidi wa kugombea nafasi hii,
Kama CCM itafuata utaratibu tutegemee kuona hakuna Uchaguzi wa ndani ya Chama katika nafasi ya Urais kwasababu Fomu itatolewa moja tu ama zitawekwa fomu za geresha na baadae kuwaengua.
Kwasababu Rais wa anayetokana na CCM ndiye Mwenyekiti wa Chama cha CCM na akishakuwa Mwenyekiti anakuwa na nafasi kubwa ya kupanga watu wake kwenye Chama kuanzia Kamati kuu, Halmashauri kuu na Sskretarieti ya CCM hivyo inafanya Chama kwa kiasi kikubwa kimtumikie Rais.
Kama CCM itafuata utaratibu wa kumuacha Rais aliyepo Madarakani agombee peke yake kwa muhula mwingine itakuwa imeweka rekodi ya aina yake na kuvunja Katiba yake kwa kuwa na Rais ambaye hajapitia mchakato wa Uchaguzi wa ndani ya Chama.
Na hili linaonekana kabisa kwa asilimia kubwa linaweza kutokea na kama likitokea litaifanya CCM itegemee dola zaidi kushinda kuliko kura za wananchi.
Una maoni gani juu ya hili?
Unaishauri CCM itumie Utaratibu ama Demokrasia kumpata mgombea Urais 2025?