Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
678
Points
1,000
Age
49
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
678 1,000
labda nikukumbushe tu kuwa na mimi nilikuwa brainwashed sunday school kama wewe mpaka nilipostuka
mi ni tofauti nawewe mi sijafundishwa sunday school sikuwa mwendaji kanisani mzuri nilikua nasubiria kuna visherehe vya mikaeli na watoto nikapige wali neema imenijia wakati najitambua...sikushangai nyie mlikua mnafundishwa lugha za kitoto ili mwelewe kwaio pole kwa kipindi icho na pole sasa kwa kipindi hiki
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,657
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,657 2,000
mi ni tofauti nawewe mi sijafundishwa sunday school sikuwa mwendaji kanisani mzuri nilikua nasubiria kuna visherehe vya mikaeli na watoto nikapige wali neema imenijia wakati najitambua...sikushangai nyie mlikua mnafundishwa lugha za kitoto ili mwelewe kwaio pole kwa kipindi icho na pole sasa kwa kipindi hiki
nipe pole kwa kipindi kile na nipongeze kwa kipindi cha sasa(in fact ni miaka mingi sasa tokea nilipokataa utumwa wa mawazo wa wazungu
 
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Messages
823
Points
500
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined May 2, 2018
823 500
Mada nzuri,kabla kuangalia kwann kanaan alilaaniwa inabidi tujue kanaan nani na hamu nani na zipi asili zao?

Je hamu alikuwa mtu wa aina gani?
Hamu alikuwa ni phoenician ambaye alipewa laana na baba yake nuhu baada kuona utupu wa nuhu mwanzo 9:22,lakini Hamu ni jina lenye asili ya kiebrania likiwa na maana blackened,burnt or hot

Je neno kanaan lina maana gani?
Jina kanaan limetokana na neno la kiebrania likiwa na maana low land embu jiulize unawezaje mwita mtoto aliyezaliwa leo jina kama hilo! Jibu jina kanaan si lake la kuzaliwa hili jina alipewa badae alipokuwa akiishi akitoka kutoka milimani kuja low land

Je lipi jina alilopewa kanaan baada ya kuzaliwa
Jina lake alipozaliwa ni Lebana ambalo asili yake ni kiebrania likiwa na maana nyeupe
itaendelea ....
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
10,305
Points
2,000
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
10,305 2,000
Halafu kuna mpuuzi mmoja anataka kuleta ujinga kuifunga JF, nasema ashindwe na atakayepata wazo la kuifunga JF kufa na afe yeye hata na uzao wake wote
EIMEN nimeitikia kwa herufi kubwa
Nalog off
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Mada nzuri,kabla kuangalia kwann kanaan alilaaniwa inabidi tujue kanaan nani na hamu nani na zipi asili zao?

Je hamu alikuwa mtu wa aina gani?
Hamu alikuwa ni phoenician ambaye alipewa laana na baba yake nuhu baada kuona utupu wa nuhu mwanzo 9:22,lakini Hamu ni jina lenye asili ya kiebrania likiwa na maana blackened,burnt or hot

Je neno kanaan lina maana gani?
Jina kanaan limetokana na neno la kiebrania likiwa na maana low land embu jiulize unawezaje mwita mtoto aliyezaliwa leo jina kama hilo! Jibu jina kanaan si lake la kuzaliwa hili jina alipewa badae alipokuwa akiishi akitoka kutoka milimani kuja low land

Je lipi jina alilopewa kanaan baada ya kuzaliwa
Jina lake alipozaliwa ni Lebana ambalo asili yake ni kiebrania likiwa na maana nyeupe
itaendelea ....
Mkuu we hatari sana kwa uchambuzi wa aina hii hadi nageuka mwanafunzi kwenye uzi wangu mwenyewe..... Tunakusubiri urudi umwage nondo zaidi maana uko deep si kitoto
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
110,223
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
110,223 2,000
mpendwa zitto junior
kwanza hongera sana kwa mada tamu na fikirishi namna hii nikuweke wazi tu kuwa mada zako zote nimezipata kupitia TAGS zako ahsante na ninakuomba usichoke kuniTAG tena na tena kila upandishapo nyuzi za aina hiyo kumbuka kuniTAG........ahsante sana kwa hilo

pili mpendwa zitto junior kwenye hii mada yako nimejaribu kuifatilia pamoja na nadharia ulizoziambatanisha na kugundua kuwa kuna vitu viwili vinahitaji majibu ya kina yasio ya kutumia nguvu nyingi wala kulazimisha na yasio na mashaka kabisa

1. kwanini Mungu alimlaani canaan badala ya ham (mwenye hatia)
2. kwa nini laana laana laana kizazi kimoja mpaka cha tatu au nne ?

mpendwa kimsingi hivo vitu ni maswali fikirishi sana na vinavoitaji majibu kwa faida ya wengi

kuna maelezo kadhaa nilitaka niyatoe lakini naona hayajitoshelezi na maswali ya msingi hasa la kwanza yatabaki palepale. hivyo ninaomba muda ili tuendelee kutafiti na kujifunza zaidi

pamoja sana na barkiwa sana mpendwa
Naomba niseme neno hapa
1. Kuna siri kubwa kwenye neno la kiungu.. Kuna wakati inahitaji tafakuri jadidi ya kiroho kuweza kuelewa
2. Hili la laana lina mlolongo mrefu... Yaani kwanini laana inaenda mpaka vizazi vine!? Hii tuitafsiri kidunia namna hii... Kinapotokea kishindo uzito wake ndio utasababisha kiwango cha madhara na sauti yake itaenda mbali kulingana na uzito wa kishindo husika... Laana si kitu kidogo hata maramoja inapiga kizalia ni kama bomu la nyuklia kule Hiroshima Japan mpaka leo madhara yapo
3. Kuna neno ndani ya Biblia nadhani kwenye kitabu cha ufunuo linasema.... Watakutwa watu wawili kondeni mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.... Baada ya hapo yanatajwa na maeneo mengine, huwa najiuliza sana kwanini wawili? Kwanini mmoja aachwe? Je hata wale wafu kuna mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa?
4. Kwenye hesabu na matendo ya roho huwa kuna vitu vya ajabu vyenye kuacha maswali mengi maswali fikirishi sana....
Ngoja nitoe mifano rahisi ya kidunia labda inaweza kutupa mwanga fulani

.Kwenye martial art kuna nguvu inaitwa chi power (vital energy power)... Ni very damaging power isiyo na madhara ya nje.. Kwa mfano mtu anapanga tofali tatu zinazofanana anapiga ya huu lakini inakatika ya katikati huku ya chini na ya huu zikibaki salama..

. Kwa wale wacheza pool... Kete anayotarajia kupiga iko kushoto mwisho lakini anaipigia hesabu kwa kupiga kete ya kupigia iende kulia kwanza ikagonge mahali fulani ndio irudi kushoto na kugonga target....

. wacheza mpira hasa wafungaji na wapiga penalty.. Kuna namna wamefunzwa kupiga mpira ili golikeeper auone unatoka nje kumbe unakuja kuingilia kwenye pembe... Ama ile ya kuruka kushoto na mpira kwenda kulia
 
SALA NA KAZI

SALA NA KAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2015
Messages
1,088
Points
2,000
SALA NA KAZI

SALA NA KAZI

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2015
1,088 2,000

mpendwa kuhusu iyo namba 1 TUPO PAMOJA,

namba 4 sijakuelewa na kuhusu wafu hapo namba 3 sijakurlewa

kuhusu namba 2 kiukweli hata mimi bado inanipashida kwa sababu mpaka sasa ninachokifahamu kuhusu LAANA bado hakijibu maswali ya msingi ya ndugu zitto junior

ijapokuwa ninajua na ninatambua kuwa
LAANA ni Apizo atoalo Mtu kwa mwingine. Yaweza kuwa mtu au kitu ili kufikwa na uovu, msiba au hasira ya Mungu

kwa lugha nyingine LAANA Ni kinyume cha baraka, yaani ni kuondoa bahati au neema katika Mtu au kitu fulani.

pia mpendwa nijuacho binafsi kuhusu laana ni kuwa kweli laana zilikuwepo katika agano la kale lakini zilikomeshwa na Mungu mwenyewe katika agano hilohilo la kale (rejea ezekieli 18:1-20, yeremia 17:10, yeremia 32:19, zaburi 62:12, ufunuo 22:12) nk na ndio maana huwezi kukuta katika agano jipya mambo ya sijui mtoto au mjukuu au vitukuu eti wamebeba dhambi za baba na babu zao katika agano jipya huwezi kuona.

ezekieli 18:1-20
1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,

2 Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?

3 Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hamtakuwa na sababu ya kuitumia tena mithali hii katika Israeli.

4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.

5 Bali kama mtu ni mwenye haki, na kuyatenda yaliyo halali na haki;

6 hakula juu ya milima, wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakumkaribia mwanamke wakati wa kutengwa kwake;

7 wala hakumdhulumu mtu, bali amemrudishia mdeni wake rehani yake, wala hakumnyang'anya mtu mali yake kwa nguvu, naye amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwavika nguo walio uchi;

8 ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yo yote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake;

9 tena ikiwa amezifuata sheria zangu, na kuzishika hukumu zangu; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana MUNGU.

10 Walakini akizaa mwana aliye mnyang'anyi, mmwaga damu, atendaye mambo hayo mojawapo;

11 wala hakutenda mojawapo la mambo hayo yampasayo, bali amekula juu ya milima, na kumtia unajisi mke wa jirani yake,

12 na kuwadhulumu maskini na wahitaji, na kuwanyang'anya watu mali yao kwa nguvu, wala hakurudisha rehani, naye ameviinulia macho vinyago, na kufanya machukizo,

13 naye amekopesha watu ili apate faida, na kupokea ziada; je! Ataishi baada ya hayo? La, hataishi; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.

14 Na kama yeye huyo akizaa mwana, naye ameona dhambi zote za baba yake alizozitenda, akaogopa, asifanye neno lo lote kama hayo;

15 hakula juu ya milima, wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake,

16 wala hakumdhulumu mtu, wala hakutwaa kitu kiwekwe rehani, wala hakumnyang'anya mtu mali yake kwa nguvu, bali amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwafunika nguo walio uchi;

17 tena ikiwa ameuzuia mkono wake asimwonee maskini, wala hakupokea faida na ziada, naye amezifanya hukumu zangu, na kuzifuata sheria zangu; hatakufa huyu kwa sababu ya uovu wa baba yake, hakika ataishi.

18 Kwa habari za yule baba yake, kwa sababu aliwaonea watu kwa ukali mwingi, na kumnyang'anya ndugu yake mali yake kwa nguvu; na kuyatenda yasiyo mema kati ya watu wake, tazama, atakufa katika uovu wake.

19 Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi.

20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

zab 62:12
Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake.

ufunuo 22:12
Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Yeremia 17:10
Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

Yeremia 32:19
mkuu wa mashauri, mweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,

mpendwa kuhusu namba 3 hao wawili wawili ninafikikiri utakua una maanisha mathayo 24:40-41 (sio ufunuo) unayotaka kujua ni kwa nini wawili ? na ni kwa kwanini nini mmoja aachwe ?

naomba nipanukuu kabisa
math 24:40-41
40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa
41wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

kwanza tunapaswa kujua kuwa Yesu katika kufundisha kwake mara nyingi alitumia mifano, mifano ambayo kiuhalisia ilikuwa ni maisha na shughuli za watu wa wakati wake (hasa kilimo na ufugaji sababu ndizo zilikuwa shughuli kuu za watu wa wakati wake hasa maskini ndio maana katika biblia utasikia habari za mimi ni mchungaji mwema......, kondoo mia akapotea mmoja......, zizi na mlinda lango la zizi......, mimi ni mzabibu wa kwel...., mpanzi wa mbegu....., mtu mmoja alikodisha shamba kwa wakulima akaenda nchi za mbali....., mkulima aliyeshika jembe kwenda kulima then akageuka nyuma....., nk)

hivyo mimi na wewe tunaoishi leo karne ya 21 mifano hiyo na mafundisho ya Yesu vinaweza kutuchanganya na kuumiza vichwa vyetu ila kwa wayahudi wa wakati wa Yesu wao walimuelewa vizuri pasipo shaka bila tabu kabisa sababu mifano aliyokuwa akitumia Yesu ndio yalikuwa maisha yao halisi ya kila siku

kumbe mpendwa ili kujua ni kwa nini wawili ni lazima turudi kwenye mazingira ya wakati wa maisha ya Yesu kimwili hapa duniani yaani masuala ya kilimo, uvunaji na hatua za uandaaji chakula hasa usagaji wa ngano (zao maarufu israeli wakati wa Yesu) ondoa mawazo ya kilimo cha kisasa au cha kikwetukwetu

sasa kwa wayahudi wa wakati wa Yesu ngano ikishavunwa ilipitia hatua kadhaa ili kupata unga na moja ya hatua hizo ni usagaji wa hiyo ngano.

mtindo uliotumika katika usagaji wa hiyo ngano ndio anaoutumia Yesu katika huo mfano wa hiyo math 24:41 kwa sababu wakati wa usgaji wa ngano, yalitumika mawe maalumu mawili yalioshikiliwa na watu wawili kila mmoja jiwe lake, jiwe moja liliwekwa chini na jingine juu yake, jiwe la juu lilikuwa na tundu kubwa katikati (tundu hilo lilitumika kuwekea ngano iliotakiwa kusagwa) na jiwe la chini ndilo lililotumika kuisaga iyo ngano.

hivyo mpendwa kazi ya mtu wa kwanza ilikuwa ni kushikila jiwe la juu lenye tundu na kazi ya mtu wa pili aliyeshikilia jiwe la chini ilikuwa ni kusaga na kukusanya unga unaopatikana. hivyo nadhani mpaka hapo utaona kuwa ni watu wawili tu walioitajika kuifanya kazi hiyo ya kusaga ngano na mara nyingi kazi hiyo ilifanywa na wanawake na ndio maana pia Yesu katumia neno wanawake (kumbe kwa wayahudi wa wakati wake walimwelewa kwa nini wawili na kwa nini mwanamke)

kumbe basi mpendwa isingeliwezekana Yesu kusema "walikuweko wanawake watatu au wanne au mmoja au saba wakisaga nafaka" wasikilizaji wa mazingira yake wangelimshangaa sana kwa sabahu kawaida ngano ilisagwa na watu wawili tu kama nilivoelezea huko juu ni sawa na leo nikwambie eti "watu watatu au watano walikuwa wakicheza pool table" au "watu wanne au mmoja walikuwa wakicheza bao" au "watu 18 au 25 walikuwa wakicheza mpira wa miguu" bila shaka utanishangaa mpendwa kwa sababu katika mazingira yetu haya kila mmoja anajua kuwa pool table na bao huchezwa na watu wawili, mpira wa miguu huchezwa na watu 22 pekee.

ninafikiri kwa upande wa kwanini wawili nitakuwa nimeeleweka

sasa kwa nini mmoja atwaliwe na mmoja aachwe ?
hapo mpendwa ukisoma kwa umakini kabisa hiyo mathayo sura ya 24 yote unaweza elewa mantiki nzima ya Yesu kuhusu namna baadhi ya watu watavopata uzima wa milele huku wengine wakiukosa, haijarishi ninyi ni ndugu kiasi gani, haijalishi ninyi ni marafiki kiasi gani, haijarishi mnaishi au kufanya kazi pamoja, haijarishi ukaribu wenu kazini ni wa namna gani nk ila ni kila mmoja kwa kadiri ya matendo yake, matendo ya mtu ndio yatakayo amua yeye kutwaliwa au kuachwa yaani kuokoka au kuangamia, kuupata uzima wa milele au kuupoteza (bila kujali undugu au ukaribu wa jumuiya unayoishi au inayokuzunguka)

kiufupi kila mmoja atabeba msalaba wake.
 
Last emperor

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Messages
5,067
Points
2,000
Last emperor

Last emperor

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2015
5,067 2,000
nadharia zote zimejikita kwenye chanzo kimoja cha imani yaani bibilia.
nilitegemea mkuu utuwekee vyanzo vya talmud au maandiko mengine ya kiyahudi ambayo hayapo kwenye bibilia,quran(umesema hakuna chanzo), Jashar, Enoch, na vya historia nyingine zinazozungumzia sakata hilo. nasema kwa sababu stori uliyoitoa umeitoa kuktoka katka mwanzo 9, na Sababu ya laana imeandikwa hapohapo. ungetoa na vyanzo vingine mtambuka vyenye sababu hizo nyingine ili msawazo wa mada usiegemee kwwnye bibilia tu.

ili litoe sura ya kwamba nadharia zako zote zina biblical support.

Mchango.
Binafsi kwa msingi wa chanzo bibilia, naamini alilaaniwa kwa sababu ya kuona uchi wa baba yake. na ndivyo ilivyoandikwa na kuelezwa humo. kwa mtiririko wa matukio ya bibilia, sio ajabu mtu na dada yake au ndugu yake kufanya mapenzi mara tu baada ya Uumbaji na Gharika ili kuendeleza vizazi na kuijaza nchi. hivyo sioni sababu ya kulinganisha laana za kipindi cha walawi ambacho tayari watu walikuwa wameshakuwa wengi tuiseme itumike kuhukumu watu wa kizazi cha nuhu au adam.
Ikiwa hoja zote zitajengwe kwenye bibilia fact ni moja tu. Ham alilaaniw kwa kuangalia uchi wa baba yake.
maoni mkuu.
Unajichanganya,unasema Ham alilaaniwa kwa kuangalia uchi wa baba yake,wakati ukisoma biblia inaandika wazi aliyeona uchi wa baba yake ni Caanan na si Ham.Soma vizuri biblia yako.Hoja ya msingi sasa, kwanini aone uchi mwingine,alaaniwe mwingine ambae hata kwenye tukio hakuwepo?
 
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Messages
823
Points
500
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined May 2, 2018
823 500
Tuichunguze nadharia ya kwanza hapo juu

Je hamu alilala na mama ake?

Hapana,ukisoma ktk mwanzo 9:22 neno uchi ktk andiko la kiebrania limetumika ERVAH likiwa na maana AIBU,CHUKIZO,SUMBUFU

Pia neno ERVAH linaweza kutumika uhusiano wa kimapenzi lakn halitumiki peke yake mpaka kuwe na neno lingine mfano walawi 18:7 usifunue uchi (GALAH ERVAH ) Hapo inamaanisha kufunua uchi kuwa Na uhusiano wa kimapenzi

Je neno kusex kwa kiebrania linatumikaje?

Kwa kiebrania neno hutumia neno YADA likiwa na maana kumjua mfano mwanzo 4:1 Adam akamjua hawa mkewe naye akapata mimba

Pia kuna neno lingine lenye kumaanisha kusex SHAKABA likiwa Na maana kulala Na Mtu mfano mwanzo 19:33 wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule akaondoka huyo mkubwa akalala nae

Hivyo Kama hamu angesex lingetumika neno YADA Au angelala na mama ake lingetumika neno SHAKABA
 
Once again umenikosha sana kwa uchambuzi wako murua kabisa..... Ila mkuu ungetusaidia pia kwanini dhambi afanye mwingine alafu alaaniwe mwingine utakuwa umetusaidia kumaliza sintofahamu yetu humu
 
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Messages
823
Points
500
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined May 2, 2018
823 500
Once again umenikosha sana kwa uchambuzi wako murua kabisa..... Ila mkuu ungetusaidia pia kwanini dhambi afanye mwingine alafu alaaniwe mwingine utakuwa umetusaidia kumaliza sintofahamu yetu humu
Mkuu ngoja tuangalie nikirudi tena namalizia
 
Inferior Complex

Inferior Complex

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Messages
3,591
Points
2,000
Inferior Complex

Inferior Complex

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2014
3,591 2,000
Mida hii ya saa 7 ndiyo nakuwa free kwa saa za huku
 
wilbard athanass

wilbard athanass

Member
Joined
Feb 28, 2014
Messages
66
Points
125
wilbard athanass

wilbard athanass

Member
Joined Feb 28, 2014
66 125
Nisoma japo ni muda mrefu nikaona leo kidogo nitolee majibu ni kwann ham hakulaaniwa uzao wa nuhu ulikuwa umebarikiwa na Mungu
Ndio maana nuhu alishindwa kumlaani mtoto na laana zake zikaenda kwa mjukuu wake canan
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
31,174
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
31,174 2,000
ukweli ni kuwa Caanan ilikuwa ni jimbo kati ya majimbo matatu ya utawala wa misri maeneo ya mashariki ya kati, kuna Caanan kuna Ammuru la tatu limenitoka kidogo,hakuna mtu alieitwa caanan ambae ndo mwazilishi wa eneo la caanan
 
Z

z12f

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
243
Points
250
Z

z12f

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
243 250
Canaan ndie alie fanya kosa hilo (la kuuona uchi wa Noah), na Canaan ndie alie laaniwa. Ham hakufanya kosa hilo.

Ham alikua actual first born wa Noah. Ila haki za mtoto wa kwanza akapewa Shem. Ndio maana wana orodheshwa kama Shem, Ham na Japheth.

Ina elekea Shem alikuwa mtakatifu kuliko Ham. Na alichokifanya Canaan kilichangia pia Ham kukosa haki za mtoto wa kwanza. Ham inaelekea alikuwa anafikiria zaidi dunia hii. Na ndio maana uzao wake ulikuwa ndio wa kwanza kujenga mahimaya makubwa ya dunia hii baada ya gharika la Noah e.g. Nimrod na Babel.

Mfano mwingine ni Cain, alikuwa actual first born wa Adam. Cain hakuwa mtakatifu na alimuua Abel. Haki za mtoto wa kwanza akapewa Seth.
 
Forum statistics

Threads 1,293,761
Members 497,728
Posts 31,152,646
Top