Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

nzaghamba

nzaghamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Messages
348
Points
250
nzaghamba

nzaghamba

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2017
348 250
Kuna ishu ya damu hapa kizalia kinahusika sana
kwa hiyo kama wazazi au mababu zangu walifanya maora hata kama mimi sijahusika na sijui inawezekana nikapata madhara...vipi kuhusu wakoloni waliotesa watumwa hichi kizazi chao cha leo kinaweza kuwa kina madhara kinayapata kutokana na hayo waliofanya mababu zao(dhulma na mateso kwa watumwa hasa wa Africa)
 
Bess

Bess

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
295
Points
500
Bess

Bess

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
295 500
Okay nikiri sijui maandiko kama ww ndio maana nikaleta mada hapa ili wajuzi mnisaidie interpretation maana najifunza je unaweza kunielewesha kwanini canaan alilaaniwa sio Ham.... Tumeskia maoni ya wengi je yako ni yapi ili tusipotoke tena.

Karibu
Umechukua nadharia(ambazo sio zako wala za biblia)kuelezea hoja yako dhaifu(sorry to say).
Kanaan alimkuta baba yake kalewa(hakumnywesha yeye pombe) na kwenda kuita wenzake waje washangae uchi wa baba yao. Wenzake wakachukua nguo wakaenda kinyumenyume na kumfunika baba aliekuwa uchi. Pombe ilipoisha kichwani mzee akajua alichofanya mwanae, akamlaani.

Ukifuatilia kizaz cha Kanaan waliishi Ethiopia na nchi nyingine kaskazini kwa Afrika., japo biblia haisemi wala kutaja mahali popote kwamba huyu jamaa aliye laaniwa alikuwa mweusi.

Biblia inataja mataifa mawili na kabila mbili za watu zikitofautishwa na rangi sehemu moja tu --Esau na Jacob. Hivyo tukitumia biblia kama chanzo cha kujua asili ya muAfrika na MTU mweupe tuangalie WAP bible imetaja watu/kabila/taifa walio tofautishwa na rangi zao
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000

Mkuu ni wapi kaanani alimchungulia baba yake?? Biblia inasema Ham ndio alichungulia ila laana ndio kwa Ham ndio maana mada imeletwa hapa kama sasa sielewi umetoa wapi hii hoja yako

Kingine HAM kuwa mweusi sio mpaka biblia iseme upo ushahidi wa kisayansi kuelezea hamites nature yao ni weusi na weupe walitokana na caucasoids ambao ni uzao wa japhet na hata pote walipoishi uzao wa Ham na japhet kuna wazungu na waafrika na pote walipoishi Semites yaani watoto wa SHEM utakuta waarabu wanaishi

Ni vizuri kabla ya kukosoa uwe umejiandaa kuliko kumislead watu...... Sasa kaanani aliishi ethiopia lini?? Duh
 
Minor correction, Ham ndiye aliyeona uchi wa babaye, Kanaani ni uzao wa huyu ndugu

Ninachopinga ni hoja yako kwamba hapa ndiko Mu afrika alikotoka
 
Hapana mkuu sijasema Ham alikuwa mweusi ila kote nimesema MKE WA HAM ndio alikuwa mweusi ndio maana watoto wote wa Ham walikuwa weusi Ethiopia misri na libya hawa ndio watoto wa kwanza wa Ham na wote nchi zao ni za wati weusi kihistoria ila nakataa kuwa laana ndio ilimfanya awe mweusi soma hapo kwenye HITIMISHO

Barikiwa
 
Bess

Bess

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
295
Points
500
Bess

Bess

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
295 500
Mkuu ni wapi kaanani alimchungulia baba yake?? Biblia inasema Ham ndio alichungulia ila laana ndio kwa Ham ndio maana mada imeletwa hapa kama sasa sielewi umetoa wapi hii hoja yako

Kingine HAM kuwa mweusi sio mpaka biblia iseme upo ushahidi wa kisayansi kuelezea hamites nature yao ni weusi na weupe walitokana na caucasoids ambao ni uzao wa japhet na hata pote walipoishi uzao wa Ham na japhet kuna wazungu na waafrika na pote walipoishi Semites yaani watoto wa SHEM utakuta waarabu wanaishi

Ni vizuri kabla ya kukosoa uwe umejiandaa kuliko kumislead watu...... Sasa kaanani aliishi ethiopia lini?? Duh
Unafaham 'Kush' inayotajwa na bibilia kwenye habari hii ni nchi gani kwa sasa? Ni vizurr kabla ya kuanzisha hoja ujue misingi inayoshikilia hoja
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Unafaham 'Kush' inayotajwa na bibilia kwenye habari hii ni nchi gani kwa sasa? Ni vizurr kabla ya kuanzisha hoja ujue misingi inayoshikilia hoja
Kush siongelei nchi ila jamii.... Na waliishi mashariki ya kati huko Yemen/bahrain ya sasa ndio baadae migration na mambo mengineyo pamoja na vita na falme za mesopotamia ilipelekea wamigrate afrika na kusettle kaskazini mashariki mwa afrika wakateka kuanzia sudan mpaka eritrea enzi hizo na ndio mwishoni walasettle huko huko kwenye pembe ya afrika ila nature yao ni KUSH huyo huyo huyo wa biblia
 
KijanaHuru

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
964
Points
1,000
KijanaHuru

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2017
964 1,000
Ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Nishakumbuka Sasa Kwanini Filamu Ya Noah ile mpya ilipingwa sana
maana kuna baadhi ya picha zinazochezwa mle zipo sawasawa kabisa na baadhi ya ukweli uliousema anyway
acha tuone hoja zingine
 
SALA NA KAZI

SALA NA KAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2015
Messages
1,090
Points
2,000
SALA NA KAZI

SALA NA KAZI

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2015
1,090 2,000
View attachment 775662
Habari za jioni wanajukwaa....kama kichwa cha uzi kinavyosema ningependa tujadili mada hii Kutokana na hili swali swali kuulizwa mara nyingi kwenye thread zangu nimeona nifungue uzi wake ili tujaribu kulitatua hili swali

Je ni kwanini aliyetenda dhambi ya kumuangulia uchi wa babake ni HAM ila laana ikaenda kwa mwanaye ham aliyeitwa CANAAN....

STORI YENYEWE
Mwanzo 9
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake

Mpaka hapa tunaona anayetajwa kuchungulia uchi ni Ham ila laana inaenda kwa Canaan why?? Embu tusome nadharia hii

NADHARIA #1
Kutoka vyanzo tofauti vya kihistoria na kidini vinaelezea kisa hiki kwamba Nuhu alipolewa Ham hakuona uchi kama uchi ila inaelezwa Ham alilala na Mke wa Nuhu yaani Ham alilala na mama yake mzazi na mwisho wa siku akabeba mimba na akazaliwa Canaan na hii ilipelekea Nuhu amlaani Canaan na sio Ham sababu alikuwa kizazi cha dhambi haramu kabisa..... Na vitabu hivi vinaenda mbali na kusema Ham alimuhasi baba yake alipokuwa amelewa hiyo nayo ikapelekea Nuhu kushindwa kuzaa mtoto mara baada ya gharika!!!

VITABU VYA DINI
Nadharia hii sio tu nje ya vitabu vya dini ila hta vitabu vya dini hasa biblia inaweza kutumika kuijengea hoja embu tuangalie tafsiri yake

Mambo ya walawi 20
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao

Walawi 18:8
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako

NB:Kitabu cha mwanzo na mambo ya walawi vyote viliandikwa mwanzoni na Nabii Musa hivyo kama tutachukua tafsiri yake ya ''KUANGALIA UCHI WA BABA YAKO'' inamaanisha kuna ukweli juu ya nadharia hii kuwa Ham alimlala mama yake mzazi/mke wa Nuhu

Na sio kwa baba tuu Musa alielezea zaidi

Walawi 20
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana

Biblia haikuishia hapo ila ukisoma kitabu cha habakuki kinakataza mtu kulewesha jirani yake ili KUMCHUNGULIA UCHI.... Ikimaanisha kama ambayo Ham alimfanyia baba yake alipokuwa amelewa basi ndio hiko anachokataza habakuk ila sio kuchungulia kwa macho kama wengi tulivyoaminishwa

Habakkuk 2:15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Mistari iko mingi zaidi ya 10 inayoeleza kwamba kumchungulia kaka baba au mjomba wako ni kulala na mke wake hivyo wa waliouliza swali hili naona tunaweza conclude kwa nadharia hii kuwa HAM alimlala mke wa NUHU ndio baada ya kuja kujua alichofanya na mimba aliobeba akamlaani Canaan sababu ndio zao la dhambi hiyo iliotendeka

NADHARIA #2
Ukisoma vitabu vya dini ya kiyahudi kma midrash vinasema Canaan aliona Nuhu akiwa uchi hivyo akaenda kumuhasi kwa kutumia kamba na alipotoka ndio baadae Ham alikuta Nuhu akiwa amevuliwa nguo yeye akaishia kucheka tu badala ya kumfunika na mwisho wa siku ndipo laana akapewa Canaan kwa kufanya hicho kitendo

NADHARIA #3
Hapa inadaiwa na wanatheolojia kuwa mwandishi wa kitabu hiki alikuwa anatafuta sababu ya kuhalalisha uvamizi wa israel kwenye nchi ya Canaan so akapachika jina Canaan badala ya HAM ili ahalalishe uvamizi wa israel kwa kigezo cha kwamba NENO LA MUNGU LILIANDIKA!!!

NADHARIA #4
Inasema Canaan hakuwa mtoto wa Nuhu ila ndio alirudisha damu ya wanefili baada ya gharika baada ya Malaika aliyeitwa SHAMAEL siku chache kabla ya gharika alimlala mke wa HAM aliyeitwa Neitamuk na kumpa mimba ya mnefili CANAAN na ndio alisababisha maasi na roho ya shetani kupata nguvu upya immediately baada ya gharika na ndiye alipelekea kuzaa wanefili kama wale wa kabla ya gharika hivyo kwa kuona uovu wa HAM aliofanya, hasira za Nuhu zikaishia kwa CANAAN sababu ndio alikuwa uzao wa roho ya kishetani (SHAMAEL) iliosababisha hadi dhambi kurudi baada ya gharika

BAADA YA LAANA
Tunaona canaan akizaa watoto walioishi miji kama sodoma Gomorrah na Gaza zote israel ya sasa na walikuwa na falme zenye nguvu sana ila kwa kuwa laana hii ya Nuhu iliwafuata ilikuja kutimizwa na watoto wa yakobo (uzao wa SHEM) waliokuja kuwapora nchi yao ya CANAAN na wakawachinja takribani kizazi chote rejea kitabu cha joshua na kumbukumbu la torati na hata wachache waliobaki waliendelea kuteswa sana na waisrael na BIFU hili lilienda hadi kwa Yesu alipokataa kumponya mwanamke wa kanaani

Mathayo 15:22
22 Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa

CANAAN NA WANEFILI
Hoja ya kwamba canaan huenda alikuwa uzao wa malaika shamael ama uzao wa ajabu wa Ham na mama yake watoto wake wote walikuwa wanefili yaani majitu ya futi mpaka 28..... Kati ya watoto wote wa ukoo wa Nuhu hakuna mtu aliyezaa wanefili kuliko Canaan na makabila yote ya warefai kipindi hicho walitoka familia ya canaan wawe wayebusi wagilgal waamori wahiti wahivi n.k je huu unaweza kuwa ushahidi kuwa hakuwa mtoto wa uzao wa kawaida ndio maana akazaa wanefili watupu huku na yeye akiwa mnefili???

HAM KWENYE UISLAM
Sijapata popote kwenye Quran inapoandikwa kuhusu laana hii ya Canaan ila kwenye ukristo ma uyahudi ndipo imetajwa. Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan

HITIMISHO
Mada hii imetumiwa sana na wazungu wakoloni hasa karne ya 19 kuhalalisha ukoloni wa watu weusi kwa kigezo kuwa mwafrika alilaaniwa ila hoja hii naipinga sababu canaan alilaaniwa peke yake na kizazi chake kwa ukubwa kilishafutwa ila waafrika 80% walitokana na kizazi cha wale watoto 3 wa HAM ambao laana hii haikuwahusu hivyo natumia fursa kupinga propaganda hiyo rasmi na ni vizuri waafrika tupende kusoma historia yetu ili wahuni wachache wasipotoshe ukweli

Naomba kuwasilisha

Karibuni wanajukwaa wote tusaidiane kujadili kuhusu nadharia hizi,
mpendwa zitto junior
kwanza hongera sana kwa mada tamu na fikirishi namna hii nikuweke wazi tu kuwa mada zako zote nimezipata kupitia TAGS zako ahsante na ninakuomba usichoke kuniTAG tena na tena kila upandishapo nyuzi za aina hiyo kumbuka kuniTAG........ahsante sana kwa hilo

pili mpendwa zitto junior kwenye hii mada yako nimejaribu kuifatilia pamoja na nadharia ulizoziambatanisha na kugundua kuwa kuna vitu viwili vinahitaji majibu ya kina yasio ya kutumia nguvu nyingi wala kulazimisha na yasio na mashaka kabisa

1. kwanini Mungu alimlaani canaan badala ya ham (mwenye hatia)
2. kwa nini laana laana laana kizazi kimoja mpaka cha tatu au nne ?

mpendwa kimsingi hivo vitu ni maswali fikirishi sana na vinavoitaji majibu kwa faida ya wengi

kuna maelezo kadhaa nilitaka niyatoe lakini naona hayajitoshelezi na maswali ya msingi hasa la kwanza yatabaki palepale. hivyo ninaomba muda ili tuendelee kutafiti na kujifunza zaidi

pamoja sana na barkiwa sana mpendwa
 
Nmefurahi sana kuona umerudi jukwaani naada ya muda mrefu..... Nikiri tu tokea ule uzi wa CHRISTMAS nimegundua una kitu kikubwa sana sana ambacho Mungu amekupa ili ulete impact kwenye jamii hivyo nkuombe ujitahidi angalau uwe unapita pita mitandaoni huku uendelew kumwaga elimu nzito kila upatapo muda

Kuhusu mada ucjal ntaendelea kukutag maana najua utaziona tu at ur convenient time pia kuna mada nyingine nmeandaa nmekutag nasubiri mods waiachie i hope hiyo pia utaipitia utupe elimu adimu

Barikiwa
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,658
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,658 2,000
mtu anapoleta mada kama hii ya nuhu huwa nakumbuka gharika feki
sijui lini watu weusi wataamka na kurealize everything narrated in the bible is just a fairytale
 
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
689
Points
1,000
Age
49
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
689 1,000
mtu anapoleta mada kama hii ya nuhu huwa nakumbuka gharika feki
sijui lini watu weusi wataamka na kurealize everything narrated in the bible is just a fairytale
gharika feki unayokumbuka ni ipi na hiyo orijino yake itakua ipi maana kwenye feki kutakua na orijino
 
original(which was actually a mythology) ni epic of gilgamesh ambamo yamesimuliwa mafuriko ambayo miaka elfu kadhaa wazungu wakacopy na kupesti kwenye kitabu chao kinachoitwa biblia
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
original(which was actually a mythology) ni epic of gilgamesh ambamo yamesimuliwa mafuriko ambayo miaka elfu kadhaa wazungu wakacopy na kupesti kwenye kitabu chao kinachoitwa biblia
Unanikumbusha mbali sana kina enkidu,shamash na utnapishtim.... Hatari sana
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
mtu anapoleta mada kama hii ya nuhu huwa nakumbuka gharika feki
sijui lini watu weusi wataamka na kurealize everything narrated in the bible is just a fairytale
Mkuu nliwahi leta mada kuhusiana na hilo nafkiri unakumbuka matusi niliyotukanwa..... Humu wafia dini ni wengi so inatakiwa niende na spidi yao otherwise patakuwa hapatoshi humu
 
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
689
Points
1,000
Age
49
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
689 1,000
original(which was actually a mythology) ni epic of gilgamesh ambamo yamesimuliwa mafuriko ambayo miaka elfu kadhaa wazungu wakacopy na kupesti kwenye kitabu chao kinachoitwa biblia
kwaio hata wana israel kutoka utumwani walicopy simulizi gani?
 
Forum statistics

Threads 1,295,408
Members 498,303
Posts 31,211,193
Top