NABII NUHU(a.s) NA GHARIKA

NABII NUHU(a.s) NA GHARIKA

Zerock

Senior Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
147
Reaction score
234
Nabii Nuhu (a.s) kama ilivyo kawaida kwa mwenyezi Mungu kutuma mitume kwa waja wake waliokishirisha madhambi.

NUHU baba yake aliitwa Lamik ibin Matushalakh.
Alianza kazi ya utume akiwa na miaka 40 na alifanya kazi ya utume kwa miaka 950.
Alitumia kila njia ya kufanya kazi aliotumwa,kwa siri,kwa dhahiri .
Ilifika kipindi watu wakimuona wanamkimbia na wengine wanatia vidole kwenye masikio yao
Kila baada ya miaka mia tatu alikuwa anapata watu 10.
Akamuomba mwenyezi Mungu akamwambia;hawa watu wako hawataki,nishawahubiria sana lakini hawataki hata kuniona.
Mwenyezi Mungu akamwambia; Rudi ukawambie tena.
Baada ya miaka mia tatu hali ndo ile ile.
Hadi alipofikisha miaka mia tisa mwenyezi Mungu akamwambia waliokuamini ndio hawo hawo hatatokea mwingine tena wa kukuamin,akamuamrisha atengeneze safina (meli kubwa)
Akiwa anatengeneza lile safina wakawa wanapita watu wanamcheka
Akawambia,;kama nyie mnatucheka ,na sisi tunawachekeni hivo hivyo kam mnavyotucheka sisi.
Baada ya kumaliza, mwenyezi akamwambia;
Pandisha humo dume na jike kutoka kila wanyama na wale waliomuamini tu!
Katika watu ambao hawakumuamini alikuwepo mke wake na mtoto wake mmoja

Na wote waliomuamini walikuwa maskini na watu wanyonge.

Mwenyezi Mungu akamwambia
Husinisemeshe kitu kuhusu watu ambao hawakukuamini .

Wingu likatanda,manyunyu,mvua kuuuubwa (gharika)
Mtoto wake akakimbilia juu ya mlima
Nuhu akamwambia
Njoo twende
Dogo akasema
Nitakimbilia juu ya mlima wala mvua haitonifikia
Nuhu akamwambia
Mvua ya leo hutoboi

Mvua ikakaza,maji yakajaa kila pahali,kila kitu/mtu wkaangamia
Mvua ilikamua kwa siku 40 ndipo ikazima
Na maji yalikaa kwenye ardhi kwa miezi 6 hadi mwaka 1... Ye$
Ndipo mwenyezi Mungu akaiamrisha ardhi imeze maji
Na ile safina ikasimama juu mlima al judiy (Ararat) uturki

Baada ya hapo mwenyezi alianzisha kizazi kingine
Kutoka kwa watoto wa nabii Nuhu tu ..!!

1: SAM (waarabu, wayahudi,waajemi)
2: HAM (Waafrika)
3: YAFETH (Warumi,Waturuki,Wazungu)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom