Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Unajua mkuu umekerekwa na kitu ndio Maana umeziona Habari za Mungu hazikufurahishi.Japo kwa kuwa ulipata bahati ya kuhudhuria hata sunday school nawaomba wakristo wakukumbuke kwenye sala utaiona tena nuru.
Nikirudi kwenye maada hivi mtu akimuua mwanao hajakuadhibu,,hajakuumiza moyo,,Mbona ukiwa una bifu na mtu utawaambia wanao wasicheze hata kula kwake...Mungu kumuua mwanawe David ni adhabu tosha kwa David au ulitaka amuue David??
Labda naweza sema Umeamua tu kukosoa hio adhabu pasipo na kujua ilitolewa kwa haki na kuzingatia Mambo mengi tusioyajua.
Alipompeleka mstari wa mbele askari wake ili auliwe halafu amle mke wa huyo askari,adhabu ilitolewa kwa mtoto aliyezaliwa(at least ni hekaya tu hakijawahi kutokea kitu kama hicho)
Characters zote za kwenye yale maandishi ni za kufikirika tu..
 
Once again umenikosha sana kwa uchambuzi wako murua kabisa..... Ila mkuu ungetusaidia pia kwanini dhambi afanye mwingine alafu alaaniwe mwingine utakuwa umetusaidia kumaliza sintofahamu yetu humu
Nimemsikia muhibiri mmoja akisema kuwa huenda Caanan ndio alikuwa kipenzi cha baba yake, hivyo itamuuma zaidi kuliko angemlaani yeye, yaani ndio alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Ham na Nuhu alilijua hili.
 
Sisi
NB:Mods naomba msihamishe mada hii kwenda jukwaa la dini sababu licha ya kuwa nimequote baadhi ya mistari ya vitabu vya dini ila uzi huu ni mtiririko wa mada zilezile nilizoanza humu JF intelligence kuhusu wanefili na wanadamu wa kale so mkihamisha mtaharibu mtiririko wa mijadala yangu kwa wanaofuatilia.... Ntashkuru kwa ushirikiano wenu

Cc JamiiForums Innovator Invisible Reserved
Wengine hatupo ktk majukwaa ya dini ila tunafaidika na hii mada kwa hivo mods usiiondoe kabisa
 
K
Mkuu zitto junior ili uweze kuelewa ni kwanini Nuhu alimlaani Caanan na siyo Ham aliyetenda kosa, kwanza unatakiwa ulielewa na kuliamini NENO la MUNGU. Ili ulielewe NENO la MUNGU, kwanza lazima uliamini. Binadamu hatuwezi kumwelewa MUNGU, lakini tunaweza kulielewa NENO lake ambalo ametupa ili litusaidie katika maisha ya sasa na yale yajayo.

Tatizo linakuja pale ambapo watu walio wengi hawataki kuielewa Biblia wala kuiamini, wengi wanaona kile kilichoandikwa kwenye Biblia ni kama hadithi tu, ni kama porojo tu ambazo hazina maana. Ukweli ni kwamba, Biblia ni zaidi ya hadithi, ni zaidi ya Historia, na ni zaidi ya Unabii ambao umekuwa ukitimia kila siku. Kwa kulitambua hili, mimi nitakupa majibu ya Kibiblia ni kwanini Nuhu alimlaani Caanani badala ya Ham. Majibu yote yapo ndani ya Biblia na nje ya Biblia huwezi kupata majibu.

Iko hivi; zamani zile Wazazi hasa baba walikuwa wanatoa baraka au laana kwa kizazi cha watoto wao na siyo kwa mtu mmoja peke yake. Kama ni baraka, baba alikuwa anatoa baraka hizi kwa watoto wake wa kiume na vizazi vyao vyote vinavyofuata kwa sababu walikuwa wanaamini kuwa kizazi hakiishii kwa watoto, bali kinaendelea na kuendelea. Pia huu ndiyo ulikuwa utaratibu waliojifunza kutoka kwa BWANA MUNGU, pale alipotoa laana ya kwanza kwa mwanadamu na nyoka;


"nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino". MWANZO 3:15







Hapo juu utaona hiyo laana siyo kwa Eva na nyoka peke yao, bali ni kwa uzao wao wote utakaotokea duniani. Hii inaonekana kuwa wazee wale wa kale walijifunza pia kutoa laana au baraka kwa kizazi na kizazi. Hebu tuone baraka ya Isaka kwa Yakobo.

"Mataifa na wakutumikie, na makabila wakusujudie. Uwe bwana wa ndugu zako, na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakaye kulaani, alaaniwe na atakayekubariki, abarikiwe". MWANZO 27:29







Hapa pia utaona Yakobo anabarikiwa na baba yake, tena siyo baraka kwa ajili yake tu katika maisha yake yeye kama Yakobo, bali ni kwa ajili yake na uzao wake wote utakaofuatia baada yake. Hivi ndivyo ilivyokuwa, hivi ndivyo wanadamu walijifunza kutoa baraka kwa wana wao au laana. Pia unaweza ukasoma kitabu hicho cha MWANZO sura ya 49, na utaona jinsi ambavyo na yeye Yakobo alivyotoa baraka kwa watoto wake 12.

Tukirudi upande wa BWANA MUNGU, pia tutaona jinsi alivyombariki mzee Ibrahimu, hakumbariki yeye tu kwa wakati ule, bali alimbariki yeye na uzao wake wote utakaofuatia baadaye.


"Nami nitakufanya wewe kuwa Taifa kubwa na kukubariki, na kulikuza jina lako nawe uwe baraka. Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa". MWANZO 12:2-3








Mpaka hapa tutakuwa tumeona jinsi baraka na laana zilivyokuwa zinatolewa na inaonekana wazi kabisa namna ya kutoa baraka au laana, Wanadamu wa kale akiwemo mzee Nuhu walijifunza kutoka kwa MUNGU. Tukumbuke kuwa Nuhu alikuwa ni Nabii wa MUNGU, na aliongea na MUNGU mara nyingi tu katika njozi na maono. Hivyo basi Hamu alipokosea kwa kumwangalia baba yake akiwa uchi na kumcheka, alilaaniwa Caanani ambaye alikuwa ni uzao wa Hamu, yaani kizazi chote cha Hamu kikawa kimelaaniwa.

Huo ndiyo ulikuwa utaratibu wa kutoa laana au baraka, tena ni utaratibu ambao ulikuwa na baraka zote toka kwa MUNGU. Caanan hakumcheka Nuhu, lakini alilaaniwa sababu yeye alikuwa ni uzao wa Hamu, Caanan alikuwa anabeba damu ya Hamu ndani yake na alipaswa kulaaniwa. Pia tukumbuke jinsi MUNGU alivyosema katika zile Amri kumi;


".........nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu". KUTOKA 20:5-6








Nuhu hakukosea kumlaani Caanan, nasema hakukosea sababu Nuhu alifuata utaratibu uliokuwepo. Utaratibu ambao hata BWANA MUNGU aliutumia kwa mara ya kwanza pale Eva alipokula matunda ya mti aliokatazwa asile. Tukihoji kwanini Nuhu Nabii wa MUNGU alimlaani Caanan kwa makosa ya baba yake, itakuwa kama tunataka kuhoji pia ni kwanini sisi leo hii tunabeba laana ya Eva na Adamu wakati siyo sisi tuliokula tunda. Nafikiri hakuna mwanadamu anayeweza kusimama na kumuuliza MUNGU kwanini ulifanya hivyo, kwanini ulitulaani sisi? (Soma ISAYA 45:9 au WARUMI 9:14-21)

MUNGU hakosei na wala MUNGU hamuonei mtu wala kumpendelea mtu. Nuhu alikuwa ni Nabii wa MUNGU, hivyo basi laana ya Nuhu kwa Caanan ilipata baraka zote toka kwa MUNGU. Kama Nuhu angekuwa ametoa laana kwa uonevu bila kufuata utaratibu unaokubalika na MUNGU; basi MUNGU asingekubali Caanan alaanike, angeizuia hiyo laana isitokee.

Nina imani kwa maelezo hayo, utakuwa umeelewa ni kwanini Caanan alibeba laana ya baba yake, tena siyo Caanan tu, bali ni yeye na uzao wake wote uliofuatia. Hata sisi Waafrika tunabeba laana hiyo mpaka leo, lakini tukumbuke kwamba MUNGU aliyetupiga kwa laana, ndiye YEYE huyo huyo aliyetuletea UKOMBOZI kupitia kwa Mwanawe YESU KRISTO.


"Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam Mimi ndiye, wala hapana MUNGU mwingine ila Mimi; naua Mimi, naponya Mimi, nimejeruhi tena nimeponya; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu". KUMBUKUMBU LA TORATI 32:39







Mkuu zitto junior hatuwezi kumwelewa MUNGU hata siku moja, akili zake, wala mawazo yake, hayachunguziki na Mwanadamu wala Malaika. Lakini tunaweza kulielewa NENO lake, kuliamini na kumtii Yeye kama MUUMBA wetu.
Kwann haikusemwa alaaniwe Ham pamoja na vizazi vyake na badala yake akasema alaaniwe canaani? Hapo ndipo panatatiza.
 
Unajua mkuu umekerekwa na kitu ndio Maana umeziona Habari za Mungu hazikufurahishi.Japo kwa kuwa ulipata bahati ya kuhudhuria hata sunday school nawaomba wakristo wakukumbuke kwenye sala utaiona tena nuru.
Nikirudi kwenye maada hivi mtu akimuua mwanao hajakuadhibu,,hajakuumiza moyo,,Mbona ukiwa una bifu na mtu utawaambia wanao wasicheze hata kula kwake...Mungu kumuua mwanawe David ni adhabu tosha kwa David au ulitaka amuue David??
Labda naweza sema Umeamua tu kukosoa hio adhabu pasipo na kujua ilitolewa kwa haki na kuzingatia Mambo mengi tusioyajua.
Vipi misri alipoua watoto wachanga wa kiume wote eti tu kumkomoa farao,..
Yani anashinda na farao kwa kuwapa mateso wengine!!!
Hivi kabisa hadi umri uliofikia unaziamini hekaya za kwenye biblia!!black men wake up
 
Watoto wa kiume wa kwanza wa kila mmisri.Kuanzia kwa farao hadi mtu alie ndani ndani kijijini misri.Kwa hio kufiwa watoto wa kiume ilikuwa kwa wamisri wote sio kwa farao pekee.

Zaidi pale ni somo hata kwa siku zijazo.Maana yako mapigo kumi mazito kwa ajili ya watu watakaopokea chapa ya mnyama.Damu iliopakwa milangoni ina maana,, ilikuwa ishara pia kwa mambo yajayo.....


Kwa hio hizi sio hekaya bali ni mambo ya kuaminika
Vipi misri alipoua watoto wachanga wa kiume wote eti tu kumkomoa farao,..
Yani anashinda na farao kwa kuwapa mateso wengine!!!
Hivi kabisa hadi umri uliofikia unaziamini hekaya za kwenye biblia!!black men wake up
 
Kuna mambo ukiyatizama katika sura ya kimwili huwezi kuyaelewa kabisa ua unaweza usipate picha halisi.

Mimi sikuzote nilikuwa najua sababu kubwa iliyomfanya Mungu aupasue mto jordan ni ili waisrael wavuke pale maana bila hivyo wasingeweza kuvuka huo mto, katika sura ya kibinadamu ndio, Ila ila katika picha ya ulimwengu wa kiroho inakupa picha tofauti na hii inapewa uzito kwa kuwa mbona wapelelezi wavuka huo mto kwenda na kurudi bila mto kupasuka.

Pamoja na kwamba unaweza kusoma biblia, Ila lli kupata tafsiri halisi ya kilichoandikwa nilazima uitazame bible katika sura ya ulimwengu wa kiroho.
 
Watoto wa kiume wa kwanza wa kila mmisri.Kuanzia kwa farao hadi mtu alie ndani ndani kijijini misri.Kwa hio kufiwa watoto wa kiume ilikuwa kwa wamisri wote sio kwa farao pekee.

Zaidi pale ni somo hata kwa siku zijazo.Maana yako mapigo kumi mazito kwa ajili ya watu watakaopokea chapa ya mnyama.Damu iliopakwa milangoni ina maana,, ilikuwa ishara pia kwa mambo yajayo.....


Kwa hio hizi sio hekaya bali ni mambo ya kuaminika
Hiyo ni hekaya tu ndani ya novel inayoitwa biblia,it never happened historically
 
Mkuu mitale na midimu kwenye nyuzi yangu mbona nimeweka source kutoka vitabu vya kiyahudi MIDRASH na kwenye uislam nmetoa kwenye waandishi wa HADEETH za kiislam na source nimeweka hivyo mada haijabase kwenye biblia tu...... However nimeweka biblia sababu ndio kirefu inajadili laana hii kwenye maandiko yake mengine

Hoja yako kusema alimchungulia je tueleze kivipi HAM amchungulie alafu alaaniwe CANAAN what's the logic kma aliyechungulia mwingine na aliyelaaniwa mwingine?? Huoni biblia itakua inajichanganya yenyewe??

Na ndio maana kwa sintofahamu hii nikaona tujiulize je kwanini canaan na sio HAM ndio nikasoma DEFINITION ya KUMCHUNGULIA MJOMBA BABU BABA maana yake ni nini.... Ndio Manabii habbakuk musa na Ezekieli wote wanasema KUMCHUNGULIA mtu maana yake ni kulala na mke wake ndio maana nikajengea hoja huenda MUSA kama alivyomaanisha KUMCHUNGULIA baba yako kwenye WALAWI na TORATI basi pia kwa kuwa aliandika kitabu cha mwanzo alimaanisha hivo hivo kuwa HAM alilala na mama yake ndio maana mimba ya mtoto aliyezaliwa yaani CANAAN akalaaniwa

Ukisoma pia Quran Surat ya Hud.... Inamtambua Nabii Nuhu kama ana watoto wanne na jina lake ukilibadilisha kiebrania inakuwa Kahnan same as CANAAN hivyo huoni bado kama CANAAN alitambuliwa na QURAN kama mtoto wa NUHU (sababu ni mtoto wa mke wa Nuhu) haiwezi elezea pia scenario hii

However kwa hoja yako siwezi kupinga ila naomba tusaidie kwa faida ya Jukwaa zima

KWANINI HAM ASILAANIWE KWA DHAMBI ALIYOFANYA ILA AKALAANIWA CANAAN

Barikiwa
Alimchungulia uchi ndo mana wale wenzake wakaja kinyumenyume wakamfunika shuka,,angelala na mamake wangekujaje kinyumenyume
 
Alimchungulia uchi ndo mana wale wenzake wakaja kinyumenyume wakamfunika shuka,,angelala na mamake wangekujaje kinyumenyume
Mkuu kama kumchungulia Baba kwa definition ya Torati ni kulala na mke wake inamaanisha wao kuja kinyume ni reverse ya alichofanya Hamu.... Yaani wao hawakushiriki hicho kitendo na walikipinga.
 
Hapana,,,haikuji kabisa,,,
Mkuu Biblia ndio ipo hivo ngoja nkupe mstari huu
Ufunuo 22:15
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya

Je ni kweli Mbwa wataenda kuzimu?? Je hao wanaoitwa mbwa ni mbwa hawa wa kawaida??

Na sio mimi nayesema Bible ni mafumbo bali Manabii na Yesu ndio walisema hivo soma Zaburi 78:2 na Mathayo 13:10-11.

Anyway kama hiyo sio definition ya kumchungulia Baba Je Nabii Hosea alimaamisha nini kusema unamlewesha jirani ili "umchungulie"?? Ina maana unampa mtu bia ili umuangalie uchi wake alafu umuache aondoke??? Does it make sense

Karibu kwa maoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom