Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Caanan ndio wewe muafrika ila ndio ulikuwa unakaa pale Israel ya leo....
Na Ham alimjua baba yake ukisoma bible kwa mbele kuna makatazo yanatajwa kuwa ukimjua mama yako basi umemjua baba yako theoretically....
So wadadavuzi wanasema Ham alimjua mama yake ndo akatoka Caanani ( so huyu alikuwa ni laana)
Kabla ya hapo ni kama hawakuijua dhambi....bible ilitumia kiswahili mnyumbuluko ili kuficha hii situation eti" according to wadadavuzi"
 
Mkuu mitale na midimu kwenye nyuzi yangu mbona nimeweka source kutoka vitabu vya kiyahudi MIDRASH na kwenye uislam nmetoa kwenye waandishi wa HADEETH za kiislam na source nimeweka hivyo mada haijabase kwenye biblia tu...... However nimeweka biblia sababu ndio kirefu inajadili laana hii kwenye maandiko yake mengine
Hoja yako kusema alimchungulia je tueleze kivipi HAM amchungulie alafu alaaniwe CANAAN what's the logic kma aliyechungulia mwingine na aliyelaaniwa mwingine?? Huoni biblia itakua inajichanganya yenyewe??
Na ndio maana kwa sintofahamu hii nikaona tujiulize je kwanini canaan na sio HAM ndio nikasoma DEFINITION ya KUMCHUNGULIA MJOMBA BABU BABA maana yake ni nini.... Ndio Manabii habbakuk musa na Ezekieli wote wanasema KUMCHUNGULIA mtu maana yake ni kulala na mke wake ndio maana nikajengea hoja huenda MUSA kama alivyomaanisha KUMCHUNGULIA baba yako kwenye WALAWI na TORATI basi pia kwa kuwa aliandika kitabu cha mwanzo alimaanisha hivo hivo kuwa HAM alilala na mama yake ndio maana mimba ya mtoto aliyezaliwa yaani CANAAN akalaaniwa
Ukisoma pia Quran Surat ya Hud.... Inamtambua Nabii Nuhu kama ana watoto wanne na jina lake ukilibadilisha kiebrania inakuwa Kahnan same as CANAAN hivyo huoni bado kama CANAAN alitambuliwa na QURAN kama mtoto wa NUHU (sababu ni mtoto wa mke wa Nuhu) haiwezi elezea pia scenario hii
However kwa hoja yako siwezi kupinga ila naomba tusaidie kwa faida ya Jukwaa zima
KWANINI HAM ASILAANIWE KWA DHAMBI ALIYOFANYA ILA AKALAANIWA CANAAN
Barikiwa
Mwana atauchukua uovu wa baba yake
 
View attachment 775662
Habari za jioni wanajukwaa....kama kichwa cha uzi kinavyosema ningependa tujadili mada hii Kutokana na hili swali swali kuulizwa mara nyingi kwenye thread zangu nimeona nifungue uzi wake ili tujaribu kulitatua hili swali

Je ni kwanini aliyetenda dhambi ya kumuangulia uchi wa babake ni HAM ila laana ikaenda kwa mwanaye ham aliyeitwa CANAAN....

STORI YENYEWE
Mwanzo 9
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake


Mpaka hapa tunaona anayetajwa kuchungulia uchi ni Ham ila laana inaenda kwa Canaan why?? Embu tusome nadharia hii

NADHARIA #1
Kutoka vyanzo tofauti vya kihistoria na kidini vinaelezea kisa hiki kwamba Nuhu alipolewa Ham hakuona uchi kama uchi ila inaelezwa Ham alilala na Mke wa Nuhu yaani Ham alilala na mama yake mzazi na mwisho wa siku akabeba mimba na akazaliwa Canaan na hii ilipelekea Nuhu amlaani Canaan na sio Ham sababu alikuwa kizazi cha dhambi haramu kabisa..... Na vitabu hivi vinaenda mbali na kusema Ham alimuhasi baba yake alipokuwa amelewa hiyo nayo ikapelekea Nuhu kushindwa kuzaa mtoto mara baada ya gharika!!!

VITABU VYA DINI
Nadharia hii sio tu nje ya vitabu vya dini ila hta vitabu vya dini hasa biblia inaweza kutumika kuijengea hoja embu tuangalie tafsiri yake

Mambo ya walawi 20
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao

Walawi 18:8
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako

NB:Kitabu cha mwanzo na mambo ya walawi vyote viliandikwa mwanzoni na Nabii Musa hivyo kama tutachukua tafsiri yake ya ''KUANGALIA UCHI WA BABA YAKO'' inamaanisha kuna ukweli juu ya nadharia hii kuwa Ham alimlala mama yake mzazi/mke wa Nuhu

Na sio kwa baba tuu Musa alielezea zaidi

Walawi 20
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana


Biblia haikuishia hapo ila ukisoma kitabu cha habakuki kinakataza mtu kulewesha jirani yake ili KUMCHUNGULIA UCHI.... Ikimaanisha kama ambayo Ham alimfanyia baba yake alipokuwa amelewa basi ndio hiko anachokataza habakuk ila sio kuchungulia kwa macho kama wengi tulivyoaminishwa

Habakkuk 2:15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Mistari iko mingi zaidi ya 10 inayoeleza kwamba kumchungulia kaka baba au mjomba wako ni kulala na mke wake hivyo wa waliouliza swali hili naona tunaweza conclude kwa nadharia hii kuwa HAM alimlala mke wa NUHU ndio baada ya kuja kujua alichofanya na mimba aliobeba akamlaani Canaan sababu ndio zao la dhambi hiyo iliotendeka

NADHARIA #2
Ukisoma vitabu vya dini ya kiyahudi kma midrash vinasema Canaan aliona Nuhu akiwa uchi hivyo akaenda kumuhasi kwa kutumia kamba na alipotoka ndio baadae Ham alikuta Nuhu akiwa amevuliwa nguo yeye akaishia kucheka tu badala ya kumfunika na mwisho wa siku ndipo laana akapewa Canaan kwa kufanya hicho kitendo

NADHARIA #3
Hapa inadaiwa na wanatheolojia kuwa mwandishi wa kitabu hiki alikuwa anatafuta sababu ya kuhalalisha uvamizi wa israel kwenye nchi ya Canaan so akapachika jina Canaan badala ya HAM ili ahalalishe uvamizi wa israel kwa kigezo cha kwamba NENO LA MUNGU LILIANDIKA!!!

NADHARIA #4
Inasema Canaan hakuwa mtoto wa Nuhu ila ndio alirudisha damu ya wanefili baada ya gharika baada ya Malaika aliyeitwa SHAMAEL siku chache kabla ya gharika alimlala mke wa HAM aliyeitwa Neitamuk na kumpa mimba ya mnefili CANAAN na ndio alisababisha maasi na roho ya shetani kupata nguvu upya immediately baada ya gharika na ndiye alipelekea kuzaa wanefili kama wale wa kabla ya gharika hivyo kwa kuona uovu wa HAM aliofanya, hasira za Nuhu zikaishia kwa CANAAN sababu ndio alikuwa uzao wa roho ya kishetani (SHAMAEL) iliosababisha hadi dhambi kurudi baada ya gharika

BAADA YA LAANA
Tunaona canaan akizaa watoto walioishi miji kama sodoma Gomorrah na Gaza zote israel ya sasa na walikuwa na falme zenye nguvu sana ila kwa kuwa laana hii ya Nuhu iliwafuata ilikuja kutimizwa na watoto wa yakobo (uzao wa SHEM) waliokuja kuwapora nchi yao ya CANAAN na wakawachinja takribani kizazi chote rejea kitabu cha joshua na kumbukumbu la torati na hata wachache waliobaki waliendelea kuteswa sana na waisrael na BIFU hili lilienda hadi kwa Yesu alipokataa kumponya mwanamke wa kanaani

Mathayo 15:22
22 Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa


CANAAN NA WANEFILI
Hoja ya kwamba canaan huenda alikuwa uzao wa malaika shamael ama uzao wa ajabu wa Ham na mama yake watoto wake wote walikuwa wanefili yaani majitu ya futi mpaka 28..... Kati ya watoto wote wa ukoo wa Nuhu hakuna mtu aliyezaa wanefili kuliko Canaan na makabila yote ya warefai kipindi hicho walitoka familia ya canaan wawe wayebusi wagilgal waamori wahiti wahivi n.k je huu unaweza kuwa ushahidi kuwa hakuwa mtoto wa uzao wa kawaida ndio maana akazaa wanefili watupu huku na yeye akiwa mnefili???

HAM KWENYE UISLAM
Sijapata popote kwenye Quran inapoandikwa kuhusu laana hii ya Canaan ila kwenye ukristo ma uyahudi ndipo imetajwa. Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan

HITIMISHO
Mada hii imetumiwa sana na wazungu wakoloni hasa karne ya 19 kuhalalisha ukoloni wa watu weusi kwa kigezo kuwa mwafrika alilaaniwa ila hoja hii naipinga sababu canaan alilaaniwa peke yake na kizazi chake kwa ukubwa kilishafutwa ila waafrika 80% walitokana na kizazi cha wale watoto 3 wa HAM ambao laana hii haikuwahusu hivyo natumia fursa kupinga propaganda hiyo rasmi na ni vizuri waafrika tupende kusoma historia yetu ili wahuni wachache wasipotoshe ukweli

Naomba kuwasilisha

Karibuni wanajukwaa wote tusaidiane kujadili kuhusu nadharia hizi,
Thambi hairithiwi .
 
Hii kweli ina ukakasi..ila Mungu alisema "...nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne..." Sasa sielewi kwa nini wana wapatilizwe maovu ya baba zao.


Yawezekana hata Kanaani alilaaniwa kwa sababu ya maovu ya baba yake Hamu.
Hivi inakuwaje kosa afanye mtu mwingine then adhabu apewe mwingine? hii imekaaje? Sometimes Bible huwa siielewi yani
 
Vitu mnavyojadili naona sivielewi yani. hafu tofauti na mimi navyotazama ili mistari.. Ham anawakilisha mataifa yaliolaaniwa.
 
Umechambua vyema japo unaruka kipengele kinachosema ndugu zake ham walichuku shuka wakarud kinyume nyume wakamfunika baba yao....ili wasimwone pia...so kama issue ni kutembea na mke wa baba yake.....kwann kuwe na kumfunika baba
 
Umechambua vyema japo unaruka kipengele kinachosema ndugu zake ham walichuku shuka wakarud kinyume nyume wakamfunika baba yao....ili wasimwone pia...so kama issue ni kutembea na mke wa baba yake.....kwann kuwe na kumfunika baba
Kwa muktadha wa kuona uchi wa Babako kutoka kwenye sheria za Torati na Nabii Habakkuk zinaonyesha ina maana ya kumlala mke wa Baba yako..... Basi kwa maelezo hayo tunaweza sema kurudi kinyume nyume ina maana walikataa kuona uchi wa baba yao (Kumlala mke wa baba yao) na kumfunika itamaanisha walizuia kitendo cha Ham kuona uchi wa babake hivyo walienda either kumkemea au kumzuia kuendelea kufanya kitendo hicho.

Najaribu kuwaza tu kama inaleta maana..... Sababu mafumbo kwenye Biblia ni relative mfano wakisema wana wa Mungu ni kama kondoo itamaanisha opposite ya kondoo yaani Mbwa mwitu n.k ni wana wa shetani.

Sijui inaleta maana??
 
Hivyo ndio vituko vya mungu wenu wa kwenye biblia,kosa la kuzini kafanya daudi lakini anaadhibiwa mwanae...hovyo kabisa aliyeandika hizi hekaya
Lakini mkuu nafikiri hii principle ipo kwa miungu wote rejea tablets za sumeria kuhusu miungu wao ambapo ilipanga kuiangamiza watu wote wa kizazi chao ila ni Utnapishtim pekee alitonywa na mungu mmojawapo Shamash hivo kuepuka gharika lile lilioua kizazi kizima.

Hata hekaya za miungu wa kigiriki (Greek mythology) unaweza ona Zeus licha ya kumuadhibu Medusa kwa kumsaliti lakini aliweka laana kwa mwanaume yeyote atakayemtamani hivyo ukimuangalia tu unageuka jiwe.... Kosa la mtu mwingine ila adhabu hata kwa wasiohusika.

Je kwa maoni yako tukiachana na uhalali wa ''hekaya'' hizi je shida ipo kwa mungu wa biblia yaani "YHWH" pekee au hii kanuni ni ya miungu wote??

Let alone wanadamu pia ambao ukifanyiwa tatizo na mtu wa jamii fulani basi unaweka bias na jamii nzima.....

Nipe mtazamo wako assuming hizi hekaya ni za kweli....
 
Lakini mkuu nafikiri hii principle ipo kwa miungu wote rejea tablets za sumeria kuhusu miungu wao ambapo ilipanga kuiangamiza watu wote wa kizazi chao ila ni Utnapishtim pekee alitonywa na mungu mmojawapo Shamash hivo kuepuka gharika lile lilioua kizazi kizima.

Hata hekaya za miungu wa kigiriki (Greek mythology) unaweza ona Zeus licha ya kumuadhibu Medusa kwa kumsaliti lakini aliweka laana kwa mwanaume yeyote atakayemtamani hivyo ukimuangalia tu unageuka jiwe.... Kosa la mtu mwingine ila adhabu hata kwa wasiohusika.

Je kwa maoni yako tukiachana na uhalali wa ''hekaya'' hizi je shida ipo kwa mungu wa biblia yaani "YHWH" pekee au hii kanuni ni ya miungu wote??

Let alone wanadamu pia ambao ukifanyiwa tatizo na mtu wa jamii fulani basi unaweka bias na jamii nzima.....

Nipe mtazamo wako assuming hizi hekaya ni za kweli....
Nashukuru uliposema "hata kwenye mythology za miungu wengine" ...wale wengine waliweka wazi kuwa zile ni myth,hawa biblia wanataka kuwaaminisha wajinga kuwa zile hadithi zilitokea kweli..
Back to your topic,..katika mythology zote moral of the story ni kuwa usitende ovu sababu litakiletea shida kizazi chako..it seems huko nyuma family love ilikuwa juu sana ndio maana vitisho vilielekezwa kwenye kuteketeza familia na kizazi chako
 
Nimesoma mawazo ya watu tu,,ila kwa kusema kidogo,, Bado naona biblia inajisimamia yenyewe ukiishirikisha kunatokea confusion.
Basi tusaidie hapo kipi kilisababisha Dhambi afanye mwingine na laana apewe mwingine?? Je hiyo ni haki?? Au ilikuwa janja ya wayahudi ili wapate uhalali wa kuivamia Canaan??
 
Ni haki maana hukumu hutokana na sheria,,,na hio ni mojawapo ya sheria ama kanuni.Huyo alietenda dhambi alikuwa akimalizia kusudi la kuwepo kwake,,hivyo adhabu yake ilianzia kwa kizazi chake.Kama unaamini Mungu yupo basi uamini yupo kwenye ulimwengu usioonekana na wenye sheria zake na viumbe wengi kushinda huu.
Basi tusaidie hapo kipi kilisababisha Dhambi afanye mwingine na laana apewe mwingine?? Je hiyo ni haki?? Au ilikuwa janja ya wayahudi ili wapate uhalali wa kuivamia Canaan??
 
Ni haki maana hukumu hutokana na sheria,,,na hio ni mojawapo ya sheria ama kanuni.Huyo alietenda dhambi alikuwa akimalizia kusudi la kuwepo kwake,,hivyo adhabu yake ilianzia kwa kizazi chake.Kama unaamini Mungu yupo basi uamini yupo kwenye ulimwengu usioonekana na wenye sheria zake na viumbe wengi kushinda huu.
Hiyo sheria imeandikwa kwenye mstari gani maana kila jibu lazima litoke kwenye maandiko/reference.

Je kama hii ndio procedure kivp Mungu alimuadhibu Adam na sio wanawe kina Abel??

Sijaelewa hii exception imetoka wapi.... Embu tusaidiane
 
How to Read the Bible

A Guide to Scripture, Then and Now

READ AN EXCERPT

Scholars from different fields have joined forces to reexamine every aspect of the Hebrew Bible. Their research, carried out in universities and seminaries in Europe and America, has revolutionized our understanding of almost every chapter and verse. But have they killed the Bible in the process?

In How to Read the Bible, Harvard professor James Kugel leads the reader chapter by chapter through the “quiet revolution” of recent biblical scholarship, showing time and again how radically the interpretations of today’s researchers differ from what people have always thought.

The story of Adam and Eve, it turns out, was not originally about the “Fall of Man,” but about the move from a primitive, hunter-gatherer society to a settled, agricultural one. As for the stories of Cain and Abel, Abraham and Sarah, and Jacob and Esau, these narratives were not, at their origin, about individual people at all but, rather, explanations of some feature of Israelite society as it existed centuries after these figures were said to have lived. Dinah was never raped — her story was created by an editor to solve a certain problem in Genesis. In the earliest version of the Exodus story, Moses probably did not divide the Red Sea in half; instead, the Egyptians perished in a storm at sea. Whatever the original Ten Commandments might have been, scholars are quite sure they were different from the ones we have today. What’s more, the people long supposed to have written various books of the Bible were not, in the current consensus, their real authors: David did not write the Psalms, Solomon did not write Proverbs or Ecclesiastes; indeed, there is scarcely a book in the Bible that is not the product of different, anonymous authors and editors working in different periods.
Such findings pose a serious problem for adherents of traditional, Bible-based faiths.

Hiding from the discoveries of modern scholars seems dishonest, but accepting them means undermining much of the Bible’s reliability and authority as the word of God. What to do? In his search for a solution, Kugel leads the reader back to a group of ancient biblical interpreters who flourished at the end of the biblical period. Far from naïve, these interpreters consciously set out to depart from the original meaning of the Bible’s various stories, laws, and prophecies — and they, Kugel argues, hold the key to solving the dilemma of reading the Bible today.

How to Read the Bible is, quite simply, the best, most original book about the Bible in decades. It offers an unflinching, insider’s look at the work of today’s scholars, together with a sustained consideration of what the Bible was for most of its history — before the rise of modern scholarship. Readable, clear, often funny but deeply serious in its purpose, this is a book for Christians and Jews, believers and secularists alike. It offers nothing less than a whole new way of thinking about sacred Scripture.
 
Nawapatiliza wana maovu YA BABA zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao""""

Suala la Adam aliadhibiwa na wanawe wote walirithi adhabu yake,,,mfano magonjwa,,kupata mahitaji kwa kustrugle na kifo,,haya yote wanawe waliyapata kutokana ma kosa la baba yao.
Hiyo sheria imeandikwa kwenye mstari gani maana kila jibu lazima litoke kwenye maandiko/reference.

Je kama hii ndio procedure kivp Mungu alimuadhibu Adam na sio wanawe kina Abel??

Sijaelewa hii exception imetoka wapi.... Embu tusaidiane
 
Nawapatiliza wana maovu YA BABA zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao""""

Suala la Adam aliadhibiwa na wanawe wote walirithi adhabu yake,,,mfano magonjwa,,kupata mahitaji kwa kustrugle na kifo,,haya yote wanawe waliyapata kutokana ma kosa la baba yao.
Mkuu sijui umeelewa swali langu??

Yaani kwanini laana ya Ham haikuanzia kwake ndio iendelee kwa kizazi cha 4..... Ila Haikuanzia kwa mkosaji kama ilivyo kwa Adam.

Mfano kwanni Mungu hakusema NA ALAANIWE ABEL....... Ila akaanza adhabu directly kwa Adam!! Hapo ndio naweka swali kwanini contradiction hii??

Ukinisaidia hapa mada imeisha
 
Lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni litakuwa limefungwa,,na lolote mtakalolifungua duniani na mbinguni litakuwa limefunguliwa"""

Hio pia ni kanuni.

Aliemlaani caanan ni babu
yake kwa hio kwa kuwa alikuwa na IMANI neno lake likatake effect kama alivyotamka.

Aliemlaani caanan ni babu yake,,ila Adam aliadhibiwa na Mungu.
Mkuu sijui umeelewa swali langu??

Yaani kwanini laana ya Ham haikuanzia kwake ndio iendelee kwa kizazi cha 4..... Ila Haikuanzia kwa mkosaji kama ilivyo kwa Adam.

Mfano kwanni Mungu hakusema NA ALAANIWE ABEL....... Ila akaanza adhabu directly kwa Adam!! Hapo ndio naweka swali kwanini contradiction hii??

Ukinisaidia hapa mada imeisha
 
Back
Top Bottom