Hiii ni Kariakoo Gerezani ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ni aibu kwa kweli

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464

Nimerekodi video hii jana asubuhi Machi 20, 2024 nilipokuwa napita mitaa ya Kariakoo, hapa ni jirani na kilipo Kituo cha Mwendokasi pale Gerezani, kama unavyoona mwenyewe hali ya barabara si nzuri.

Magari na watu wote kwa pamoja wanapata changamoto ya kupita, mvua ikinyesha hali ndio inakuwa mbaya zaidi, hay maji yametokana na mvua iliyonyesha siku moja iliyopita kabla ya kurekodiwa kwa video hiyo.

Serikali iangalie, Kariakoo ni sehemu ya katikati ya Jiji, kuna watu wengi wakiwemo wafanyabiashara wanaotoka nje wanafika hapo, wanapoona hali kama hii inashusha hadhi ya Jiji.
 
Kutupa taka hovyo ni miongoni mwa vyanzo vya kuziba mitaro 🐒

Suluhu namba moja kwa changamoto hiyo ni ustaarabu binafsi wa kila Mtanzania katika kuhifadhi hasa taka ngumu za plastics🐒
 
Hafiki mgeni hapo, hiko ni kipande cha kkoo kinachotubeba sisi waswahili kununua Kanzu za bei chee za kuvamia minuso na hijab za picha. Na kugombania daladala.
Back to the topic hapo pako kwenye mpango wa ujenzi kutoka hapo kupanda mpaka mtaa wa arusha.
 
Hapo ni mtaa wa Lindi, kipande kati ya Msimbazi street na Shaurimoyo?
 
Back
Top Bottom