Acha kuweweseka wee!
Mada hapa...ni kwanini Pope/s walisali/wanasali na kufanza ibada nyanginezo kisirisiri na Waislam!?
Je kuna nini kinachoendelea!? Pope na Vatican mna siri gani na Waislam, ambazo Wakatoliki/waumini wenu wa kawaida hawazijui au hamuwaruhusu kuzijua/ku-question!? Daah! Teeeh! Teeeh! Teeeh!
Jana katika msikiti wa Idrisa uliopo
kariakoo Dar es salaam zimezuka
vurugu kubwa, baada ya muumini
mmoja kumzimia kipaza sauti Sheikh
Maalim Ally Basaleh na kupinga
nafasi aliyopewa ya kuongea na
kuwaombea dua waislamu
waliohudhuria msikitini hapo.
Akizungumza na Blogu ya ahbaabur
rasuul muumini aliyeshuhudia tukio
hilo bwana Ramadhani Issa alisema,
Sheikh basaleh alipewa nafasi hiyo
baada ya kumalizika kwa swala ya
Ijumaa na Imamu msaidizi wa
msikiti huo.
Sheikh Basaleh aliombwa
kuwasalimia Waislamu na
kuwaombea dua baada ya kurudi
toka Saudi Arabia kwa ajili ya ibada
ya Hijja.
Anasema Ramadhani aliposimama
Sheikh Basaleh na kuanza
kuzungumza ndipo muumini mmoja
ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja, akasimama na
kwenda kuzima kipaza sauti ili
Sheikh Basaleh asizungumze.
Baada ya tukio hilo zikazuka vurugu
kubwa na sintofahamu msikitini
hapo ambapo ilibidi waitwe polisi
kutuliza vurugu hizo ambao
walimchukua mtu huyo na kuondoka
nae. Haijafahamika kama mtu huyo
amefunguliwa mashtaka ama la.
Kutokana na vurugu hizo Sheikh
basaleh hakuweza kuzungumza wala
kuwaombea dua waislamu
waliokuwepo msikitini hapo. Hakuna
mtu yeyote alijeruhiwa katika vurugu
hizo.
Msikiti wa Idrisa katika siku za hivi
karibuni umekumbwa na vurugu za
hapa na pale baada ya watu
wanaodaiwa ni waumini wa msikiti
huo kufanya mapinduzi ya kiuongozi
kwa madai kuwa uongozi uliokuwepo
madarakani umeshindwa kuendesha
msikiti na kupelekea uduni wa
huduma za msikiti huo kwa waumini
wanaosali msikitini hapo.
Jitihada za kumtafuta Sheikh Basaleh
na upande unaopinga uongozi
kupata maelezo yao zinaendelea
kufanywa.