Kupitia hii post ya Askofu Mwamakula huenda askofu ana kikundi cha utesaji

Kupitia hii post ya Askofu Mwamakula huenda askofu ana kikundi cha utesaji

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
20,398
Reaction score
42,172
Mwenyewe anadai kuna watu walilipa gharama mara baada ya utawala wa Magufuli kwa kosa la kumtolea kauli chafu mtandaoni. Askofu amedai ana watu wake wa kumfanyia hiyo kazi ya kuwaadhibu watu waliomkosea. Je, Askofu Mwamakula sio mhusika wa genge la WASIOJULIKANA? Kwa maelezo yake ni kwamba genge lake lilidhibitiwa kwenye utawala wa Magu na pia sasa hivi pia ni kama limedhibitiwa. Ila mara baada ya awamu hii kwisha atawashughulikia wote kupitia watu wake. HII NI HATARI.

Mimi ninamsihi Askofu huyu wa CHADEMA afuate sheria kama huyu binti kamtukana mtandaoni kwa sababu sheria ya makosa ya mtandao ipo. Kutoa vitisho kama hivi haifai. Vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa wote walioshughulikiwa na watu wa Mwamakula kama mwenyewe alivyoandika.

Askofu kaandika hivi Facebook;

Gadson Irene!
Binti yangu! Amani iwe kwako!
Komenti zako zote toka uanze kusoma ukurasa huu tumesoma zikiwemo hata za matusi, kejeli, dharau na kubeza maandiko ya askofu. Hii ni haki yako na lazima ilindwe. Lakini imetulazimu tukujulisha taarifa ambayo pengine wewe hujui ili ukiijua ikusaidie leo, kesho na hata baadaye:

1. Mengi ya anayoandika na kuyatetea Askofu Mwamakula yanagusa hisia za jamii kubwa ya watu wakiwemo hata hao ambao wameshika maisha yako duniani kibinadamu kwa njia moja ama nyingine. Inaweza kuwa ni biashara, kazi, mahusiano au hata ujirani wa kawaida.

2. Wenzako wengi wanaofanya kama ambavyo wewe unavyofanya wamefungua akaunti feki au wanatumia majina bandia. Kwa hiyo si rahisi sana kwao kujulikana kazi zao, familia zao na hata historia za maisha yao.

3. Lakini wewe hutumii akaunti bandia na wala hutumii jina feki. Hviyo historia ya maisha yako inajulikana na ndugu zako pia wanajulikana.

4. Ni bahati mbaya sana wewe hujui sana kuwa kabla ya kufika hapa huyu askofu alipitia wapi na aligusa maisha ya watu wa aina gani na ya kuwa watu hao wako wapi sasa. Lakini huenda pia baadhi ya watu hao hukusoma hapa ingawa wewe hujui wana nafasi gani kwako na kwake.

5. Wakati wa Rais Magufuli wapo watu ambao walifanya kama unavyofanya wewe dhidi ya huyu askofu. Hata hivyo, baada tu ya Magufuli kuondoka, watu hao walilipa gharama kubwa sana ikiwemo kulazimika au kulazimishwa ili kumuomba msamaha Askofu Mwamakula kwa kupitia kuandika katika kurasa zao hadharani na wengine walipata shida sana kumpata kwa kuwa walilazimishwa wamtafute kibinafsi.

6. Tofauti na kipindi cha Magufuli, sasa hivi jamii ya watu wenye chuki na visasi imekuwa kubwa sana ila hawaonyeshi hadharani. Lakini ukiwa makini utawasikia wakisema vijiweni, mahali pa kazi, kwenye vikoba, nk.

7. Wengi wa wenzako wanaofanya hivi kama unavyofanya wewe ni wanufaika wakubwa wa mfumo uliopo. Hivyo ili waishi kwao ni lazima pia kupambania ufisadi hadi dakika ya mwisho. Wewe hauko hivyo, unaweza kuishi bila mikono ya mafisadi na connections zako zisidhurike.

8. Kesho ni jamhuri nyingine na ulimwengu mwingine. Tusingependa kesho uanze kujuta kwa kuandamwa na watu kwa sababu ulimtusi au ulimshambulia askofu wakati anatetea haki zao.

9. Hatutarajii kukuzimisha au kunyamazisha. Tunapenda sana uendelee kukosoa na hata kupingana na askofu na watu wengine lakini kwa hoja ili usiingie matatani na watu wengine.

10. Hatutarajii kama hataa itafikia hatua ya sisi kukutetea kama tuliwavyowatetea wale Ma DC au wale waandishi wa habari kadhaa baada ya Rais Magufuli kuondoka. Ikibidi tutafanya hivyo bila kinyongo ila wewe utakuwa mnyonge sana na utajisikia vibaya kwa kuwa utakumbuka ya kuwa ulitumia nguvu zako nyingi kumtusi mtu ambaye hana madhara yeyote kwako na wala hapambani na wewe.

11. Kuna watu wengine waliokuwa wakubwa sana kuliko hata wewe. Lakini tangu mwezi wa Novemba ulipoanza wao wanaishi katika hali ya upweke sana na kujilaumu. Wanajilaumu kwani wanakumbuka kuwa waliwatumikia watu ambao hawakuwa na shukrani. Sasa wameliwa vichwa na pia hawawezi kurudi tena kwa jamii.

Binti! Mungu akuongoze vema unapoendelea kujenga hoja, ili ujenge hoja bila kudhalilisha na kutwza utu wa wengine hasa kama watu hao wanagusa jamii. Askofu haogopi matusi, lakini kuna watu wengi wanakwazwa kwa yeye kutukanwa au kubezwa.

Kwa kukuandikia haya, askofu amekusamehe na hata ikitokea ukaja kuonana naye usijisikie vibaya kwa yale uliyoyafanya kabla ya ujumbe kukufikia. Lakini kama baada ya ujumbe huu utaendelea, basi kutakuwa na sababu ya wewe kujisikia vibaya kama utaonana naye.

Lakini ujumbe huu unaweza kuwa lulu pia kwa watu wengine wanaofanya hivyo pia kwa watu wengine (Zaburi 1:1-6).
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 27 Novemba 2025; Saa 11:40 alasiri


 
Aisee.... binadamu wengi hatupendi kukosolewa hivyo ni vema kuunga mkono au kunyamaza
 
Askofu amedai ana watu wake wa kumfanyia hiyo kazi ya kuwaadhibu watu waliomkosea.
Mama,
Nimesoma maelezo yako na andiko lote la huyo askofu, hakuna mahali ametishia kuuwa kama kmkm na polisiccm walivyoua Watanganyika.

Huo muda uliotumia kuandika uongo ungeweza kuutumia vizuri kwa jambo lingine lenye tija.

Sijui machawa wa ccm tatizo ni elimu, chuki..???
 
Back
Top Bottom