Kwakuwa alituvusha salama kutoka Awamu ya Tano, nashauri daraja la Tanzanite liitwe Samia

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,662
Ni shauri wangu

Kwanza linavuka bahari, ni ishara ya kuvuka awamu moja kwenda nyingine, pili in ishara ya upatanisho kati ya upande mmoja na mwingine, kisiasa, kiuchumi, kijamii, anapatanisha nchi, anaunganisha kama daraja linavyounga pande mbili.

Tanzanite ina asili ya huko ilikotoka, iwepo tozo maalum katika Tanzanite ili, kama ilivyo ya korosho, au nyingine, iwekezwe kwenye miundombinu ya huko, Dar isibebe fahari ya eneo jingine.
 
... kabisa; tena ni landmark ambayo ukitokea Znz kwao Samia unaiona vizuri. Hata wazanzibar na vizazi vyao vijavyo kila walionapo watajipiga vifua "hakika tulizaa kiongozi".
 
Jakaya Kikwete Oceania Bridge

Huyu mwamba anafaa kuenziwa kwa kuasisi mipango na miradi mingi inayotekelezwa
 
Hafai huyu Bibi

MwananchiHabari ZaidiKitaifa
#Siku100zaSamia: Rais Samia anavyotibu siasa za utapiamlo
THURSDAY JUNE 24 2021

Rais Samia Suluhu Hassan akikaribishwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alipowasili ikulu jijini Nairobi nchini humo. Picha ya maktaba

Rais Samia Suluhu Hassan anaelekea kutimiza siku 100 tangu kuapishwa kushika wadhifa huo Machi 19, mwaka huu, baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Rais Samia Suluhu Hassan anaelekea kutimiza siku 100 tangu kuapishwa kushika wadhifa huo Machi 19, mwaka huu, baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Ndani ya siku 100 za awali katika utumishi wa umma tumeona mengi yenye mkondo chanya wa kulivusha taifa hili kutoka tulipokuwa awali kuelekea kwenye siasa za utu, usawa, demokrasia na uwajibikaji.

Sharti kupitia makala hii tukubaliane kuwa siasa za awamu ya tano ziligubikwa na “utapiamlo kisiasa”, hivyo afya yake ilikwenda harijojo na ni sharti sasa tupate daktari wa kuliponya taifa letu kiafya.

Makala hii kwa ufupi na kwa kuzingatia utafiti wa hali ya siasa za kabla ya kifo cha Magufuli na baada ya kifo chake itaangazia kwa undani ufanisi wa Rais Samia katika utendaji wake kisiasa na kwa namna anavyozingatia na kuitumikia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwazi, weledi sambamba na kurudisha imani kwa Watanzania juu ya mifumo ya kisiasa na utawala bora iliyokuwa imekwenda likizo isiyo na mwisho.

Nikirejea kwa ufupi na kwa muhtasari, Serikali ya awamu ya tano iliyokuwa inaongozwa na hayati Magufuli ilifanya mazuri yake kadri ilivyoweza, lakini ombwe lililojitokeza wakati wa utawala wake ilikuwa ni pamoja na kubana misuli ya upumuaji wa “uhuru wa maoni”.

Ukosefu wa uhuru wa maoni ulizalisha mifumo ovu ya ukosefu wa demokrasia, uminywaji wa haki, viongozi wa umma kujichukulia sheria mkononi na ufisadi ulichukua hatamu ndani ya baadhi ya ofisi za umma. Waliotenda yote haya walijua hakuna wa kupaza sauti, aidha, aliyejaribu kupaza sauti hakusikilizwa kamwe na pengine cha mtema kuni alikipata.

Yote haya yalijitokeza kwa sababu mifumo iliyokuwepo katika utawala ilijikita ndani ya mfumo wa mkono wa chuma ili kutawala na kuleta maendeleo, jambo ambalo wasaidizi wa hayati Magufuli walishindwa kutambua na kushauri mamlaka husika ni kuwa nadharia ya utawala wa kibabe na kiimla huzalisha jamii yenye usugu na upinzani imara.

Kisiasa na kiutawala hakuna nadharia inayoonyesha hadi sasa kuwa utawala unaotumia mabavu ulifanikiwa kujenga misingi imara ya maendeleo ya watu na vitu zaidi ya kujenga chuki, hofu na machafuko ya ndani baina ya kabila moja kwenda jingine, mtu na mtu, kikundi kwa kikundi na hivyo kuhatarisha amani ya wananchi na mali zao.

Afrika baada ya kupata uhuru wa bendera kutoka kwa mkoloni, uhuru mamboleo wa mwana wa Afrika ni uhuru wa kujieleza na kuishi huru ndani ya taifa lake bila nongwa ya watawala waliopo madarakani.

Muhtasari wa tafakuri hii unaonyesha wasaidizi wa rais walipuuza na kudharau mantiki ya nguvu ya umma na kusimama katika nguvu ya dola. Kisiasa kuna tofauti kubwa kinzani kati ya nguvu ya umma na dola, mara zote umma ni imara kuliko dola.

Turejee sasa kwenye kiini cha hoja yetu ya msingi ndani ya makala haya tukiangazia ufanisi wa Rais Samia kwa utawala wake wa siku 100 akiwa mkuu wa nchi. Makala hii imefanya utafiti wake na kugundua hadi sasa kiongozi huyo amegusa “kero kuu na kuntu” ambazo Watanzania wengi walikuwa wakizililia kwa takribani miaka mitano iliyopita. Kero hizo ni uhuru wa maoni, kujieleza na utawala wenye kufuata misingi ya haki na utawala bora.

Kimantiki hili ni eneo ambalo Rais Samia amechagua kuanza nalo, hadi sasa amefanikiwa kwa asilimia 90 kukonga nyoyo za Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao kurejesha tumaini jipya la utawala wenye kuzingatia sheria, utu na nidhamu katika utumishi wa umma.

Hadi sasa tuna viongozi wa umma wanaotumikia umma na si kujitutumua kama kifutu “Puff Adder”.

Bila shaka hili kwa Rais Samia halifanyiki kwa bahati mbaya, bali anatambua misimamo na falsafa za mtangulizi wake zilisimamia nini, wapi na lipi na kwa lengo gani?

Inawezekana maswali haya yasieleweke kwa sababu Mama Samia alikuwa msaidizi wa Karibu wa hayati Magufuli, lakini hoja na jibu ya swali hili iwe ni kuwa mabadiliko ya sasa ndani ya Serikali ya awamu ya sita ni matokeo ya kile ambacho Mama Samia kifalsafa hakukubaliana nacho hata kidogo, ndio maana tupo hapa tulipo kwa mabadiliko haya yanayoendelea kufanywa naye.

Ndani ya siku 100 kaonyesha kuwa ni kiongozi anayeshauriwa na kukubali kupokea ushauri si kutoka kwa watendaji na wasaidizi wake wa karibu ndani ya mifumo ya Serikali, bali pia kutoka hata nje ya mifumo hiyo kwa maana ya vikundi vyenye uwakilishi wa watu tofauti, ikiwemo vyama vya siasa, wazee na vijana.

Mara kadhaa tumemsikia akipokea ushauri na kwenda kuufanyia kazi pale anaposhauriwa na baadhi ya makundi yatokanayo na umma wa Watanzania. Kwa dhana hiyo ni msikivu na anayeonyesha nia ya kusikiliza, kutatua na kutenda kadri alivyoguswa na kero iliyowasilishwa mbele yake na mezani kwake.

Kisiasa hii ni mojawapo ya sifa kuu ya uongozi, kiongozi sio malaika wala mjukuu wa Mungu kutokubali kushauriwa, hivyo kupata ushauri na kusikiliza raia anaowaongoza wanataka nini ni utimamu na tafsiri ya uongozi uliotokana na watu na ndio mantiki ya uwajibikaji wa kiongozi yeyote yule wa umma.

Kiongozi huyu ni mwana demokrasia wa kweli anayetawala ulingo wa siasa kwa vitendo na si kwa porojo za kisiasa, hadi sasa ndani ya siku 100 za utawala wake upo utashi wa kisiasa unaolenga kurudisha “amani ya kisiasa” kati ya chama tawala CCM na vyama vya upinzani.

Awamu ya tano ilionyesha udhaifu mkubwa katika kusimamia mifumo na fursa sawa kati ya chama tawala na siasa za upinzani, wapinzani kuna wakati waliishi kama mashetani na watu wasiostahili kupata haki zao za kikatiba kama ilivyo kwa Mtanzania yeyote yule, wakati mwingine ilionekana kuwa mpinzani Tanzania ni sawa na “uhaini”.

Hoja hii ina mashiko kwa mantiki dhuluma dhidi ya upinzani zilitendeka kwa uwazi na mchana kweupe. Hata hivyo kwa kipindi hiki cha siku 100 za Mama Samia upepo wa kisiasa umebadilika kabisa, wapinzani wamepumua na siasa zinafanyika bila hiana wala ghiliba au ubaguzi wa aina yoyote ile.

Vyama vya upinzani vinafanya siasa zao bila bughudha wala nongwa ya aina yoyote ile. Kwa nchi inayofuata mfumo na sera za vyama vingi, hili ni jambo la heri kabisa na la kupongezwa.

Hata hivyo, jicho la Mama katika siasa za usawa, uhuru na haki zimetamalaki, kusudio lake la kutaka kukutana na vyama vya siasa na kuzungumza nao juu ya mustakabali wa taifa letu kisiasa, kiuchumi na kurejea misingi ya amani yetu kwa kufanya siasa safi, ni nia njema na mafanikio ya kimkakati kwa Rais Samia katika jitihada zake za kuirejesha nchi kwenye mikono ya utawala wa kidemokrasia na kisheria kwa maslahi ya Watanzania wote kwa maana ya kizazi cha sasa na hapo baadaye.

Mama Samia ameonyesha weledi wa kusimamia mifumo ya ukusanyaji wa kodi kwa kutumia njia rasmi na zinazoeleweka bila kutumia mabavu na “dhuluma”. Awali taasisi za kikodi zilikusanya kodi kwa nguvu na dhuluma isiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Ukusanyaji wa kodi kwa kutumia dola ulijenga hofu na hivyo baadhi ya wawekezaji kukimbilia nje ya nchi na kwenda kuwekeza kwingine na hivyo taifa kukosa mapato, ndani ya siku 100, wawekezaji wanaanza kurejea nchini.

Uongozi wa Rais Samia umeleta tija, ustawi wa kiuchumi na kidiplomasia kwa maana ya diplomasia ya kikanda na kimataifa kwa mantiki ya kusaka fursa za kuwasaidia Watanzania kujikomboa kiuchumi na kiteknolojia.

Imeandikwa na Deogratias Mutungi

Mwananchi
 
Kazi ipo, uhuru wa maoni, basi tumpe atawale mpaka atakapochoka mwenyewe maana si kwa mahaba haya.
 
We msukuma uwezi kuyaona mazuri aliyoyafanya

MwananchiHabari ZaidiKitaifa
#Siku100zaSamia: Rais Samia anavyotibu siasa za utapiamlo....
Nimesoma gazeti lako loooote lakini kwa bahati mbaya sijaona bado jambo la maana,unajua watanzania tuna matatizo yetu ambayo tunatamani yashughulikiwe, mi nilidhani utaniambia kwamba mama samia.

1. Kajenga Barabara km kadhaa
2. Kajenga hospitali kadhaa
3. Kaajiri vijana kadhaa
4. Labda kanunua ndege au kaagiza ndege kadhaa
5. Bajeti imeongezeka kwa asilimia kadhaa
6. Labda mapato ya TRA yameongezeka kwa kiasi kadhaa
7. Pabda kuna miradi kadhaa ya maji kaianzisha n.k

Katika hilo gazeti lako naona tu malalamiko ya aliyekuwa raisi wa awamu ya 5, wakati huohuo hizo Siku 100 mnazozizungumzia za Huyo mama amekuwa busy kuzindua na kuendeleza miradi aliyeianzisha raisi aliyepita, huyu mama apewe muda labda atafanya kitu lakini kwa sasa mchumba bado hatuwezi kumsifia labda tu uwe shabiki wa kisiasa, na ukiwa shabiki wa kisiasa mrembo umepotea..na kama ulikuwa hujui Uhuru wa kujieleza uliminywa tangu enzi za nyerere labda ulikuwa bado hujazaliwa..
 
Hama Nchi basi!!!!
Huna hoja mrembo...ni kawaida yenu bavicha,nyie ni wanaharakati uchwara,mkishindwa hoja mnakimbilia kuhama nchi,yaani ni type ya Lissu, Mange, Roma n.k. Sisi wengine ni wazalendo hatusifii sifiii ovyo wala hatuchukii chukii ovyo..mwenye sifa tunamsifu akiboronga tunamchana..

Mimi nilishakuelewa,wewe ni shabiki wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom