tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,241
- 4,466
Hivi karibuni kumejengeka tabia ya shule nyingi za msingi, hasa za binafsi kuanzisha masomo ya ziada yanayoitwa CRASH PROGRAM.
Programu hii huhusisha masomo ya ziada kwa wanafunzi wa shule za msingi wa darasa la nne na la saba (hata la sita) kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya madarasa husika.
Katika mipango hii watoto kuwawahishwa darasani asubuhi na mapema (kwa day scholars na boarders) na kuwaachia usiku, huku shule nyingine zikikaa na wanafunzi darasani hadi saa mbili usiku.
Muda wote huo wanafunzi hubaki darasani ili wajifunze vitu vinavyoitwa vya ziada ati kwa nia ya kumaliza mitaala.
Hii ikimaanisha kuwa wanafunzi wa madarasa haya, wakisoma kwa utaratibu wa kawaida, hawawezi maliza mitaala yao.
Kwa watoto wa darasa la nne, ambao wengi wana miaka kati ya 8 hadi 10, kuwakalisha zaidi ya masaa tisa darasani kunaweza leta athari za kudumu.
Kipindi hiki watoto wanapaswa wapate elimu, lakini muhimu pia wanahitaji muda wa kutosha wa kupumzika na kufanya mambo mengine ya kijamii yatakayo kuza ujuzi muhimu, kuongeza uwezo wa kufikiri, kujenga hamu ya kujua jinsi mambo yanavyofanya kazi na jinsi yanavyotengenezwa n.k.
Bahati mbaya sana shule zinawaandaa watoto wafaulu mtihani kwa kuwakalisha madarani kwa masaa zaidi ya 9 kitu ambacho hata ubongo wao unazidiwa.
Hivi kuna umuhimu gani wa mtoto wa darasa la nne kukaa crash program? Kitu gani cha msingi anafundishwa ambacho hakiwezi tolewa katika masaa ya kawaida ya shule? Huyo mtoto atapumzika saa ngapi?
Tuna mifano yoyote ya watoto waliopita katika mfumo huo ambao walifanya vizuri zaidi walipoingia kwenye soko la ajira?
Hizi crash program zimekuwa ni chanzo cha mapato kwa walimu na shule, maana mambo waliyopaswa kuwafundisha watoto wa shule ya msingi ndani ya muda uliopangwa na serikali, hufanyika nje ya muda.
Mimi naamini elimu ya watoto inapaswa kuwasaidia watoto kuwakuza haiba, vipaji na uwezo wao. Isiwe elimu ya kuwalazimisha wafaulu kwa viwango fulani.
Inapaswa kuwafundisha kuelewa haki zao wenyewe, na kuheshimu haki, tamaduni na tofauti za watu wengine.
Hii kitu ikatazwe mashuleni. Watoto wapate muda wa kupumzika na kucheza.