Naomba nianzishe uzi mahsusi kwa ajili ya wale wote ambao tunapinga mgomo wa Madaktari ambao unaanza leo.
Hii itatupa fursa kujadili kwa nini tunapinga Madaktari kugoma na itasaidia wachangiaji wa fani mbalimbali kuelezea kwa nini hawaungi mkono wataalamu hawa kugoma.
Binafsi naamini kuwa si sahihi kugoma tena hasa baada ya ufafanuzi uliotolewa na Waziri Mwinyi,ni wazi kuwa nafasi ya mazungumzo ipo wazi.
Serikali imeshaonyesha kutikisika na hii inatosha kwa sasa rudini katika mazungumzo ili muibane serikali kwa hoja.Kauli kama mgomo usiokuwa na kikomo haina tija na inaondoa hadhi ambayo Madaktari wanapewa na jamii.Kauli hii maana yake ni kuwa binadamu wataachwa wateseke na wafe hadi hapo madaktari watakapopata wanachotaka, HAIKUBALIKI.
Kuna kauli ya kuwa huduma muhimu hazitasimama,hii si kweli kwani katika mgomo accountability itakuwa kwa nani?
Mapungufu katika vitendea kazi ni mambo ambayo yanazungumzika katika ngazi tofauti na wote tunayajua haya na mengi yanasababishwa na nyie wenyewe Madaktari na nitatoa mfano.Vifaa vinakosekana lakini pesa zinatumika katika mambo ambayo si ya muhimu na muidhinishaji akiwa ni mtu wa fani ya Udaktari.
Inawezekana kabisa kuwa serikali ina mapungufu yake lakini tuangalie ni nani ataathirika zaidi katika mgomo huu,ni wazi kuwa watu maskini wa kipato cha chini wataumia zaidi.
Ogopeni siku watu wa hali ya chini watakapoamua kuchukua hatua,hapatakuwa na pa kujificha.
He who fights and run away lives to fight another day.