Kwa wote tunaopinga mgomo wa madaktari

Tuwaunge au tuwapinge tutajijua wenyewe wananchi tuko kama matahira madaktari wanasema hospitali hawana hata tochi za kuchunguzia masikio,machine za x-ray hazifanyi kazi gozi za kufungia vidonda hazitoshi dawa za kuzuia wanawake wasimwage damu baada ya kujifungua  hazipo,nyuzi za kushonea hakuna vitambaa vya kufunga midomo yao au gloves za wao kusambaza maambukizi kati ya mgonjwa na mgonjwa hakuna sisi hatuoni na lwetu tufeeee tu ,hatujielewi hatujui wanachokisema ni shauri yetu mpaka hapo tutakapojitambua tutajua wanamaanisha nini
 
UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.
MADAI
1. Kuboresha Huduma za afya hospitalini kwa vifaa vya upimiaji, madawa.
2. Kuboresha Mazingira Ya kazi (ukarabati wa majengo, uongezaji wa vitanda)
3. Posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) 5% kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu 40% ( MEANING anayefanya kazi SAME, TANDAHIMBA, NYAMPULUKANO nk ni tofauti na akaaye MJINI)
5. Posho ya makazi 40% au nyumba kama ilivyo kisheria(since DOCTOR IS ENTITLED KUPATA, HII NI KATIKA SHERIA YAO WENYEWE)
6. Bima ya Afya(Green Card) kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya.
7. Kuwaondoa viongozi wa juu wa W/Afya kutokana na ubadhirifu.
8. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi 30% au Chanjo(Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)

MAKUBALIANO
1. Kuondolewa kwa viongozi na watendaji wa juu wa Wizara ya Afya
2. Kupewa nusu ya ombi la call allowance hadi pale baada ya mazungumzo(ktk kipindi cha mpito)
3. Kamati kujadili na kuona kiasi gani mshahara na posho zitaongezwa kwa kutengeneza(developing a formula)
4. Serikali kuongeza bajeti ya W/Afya ili kuongeza vifaa, na madawa.

HALI ILIVYO SASA
- HOSPITALINI: hakuna huduma za afya (matibabu, upimaji wala upasuaji), YAANI NI KWELI TUMEGOMA
- VYOMBO VYA HABARI: Kuna upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa umma.
- MTAANI:Hofu na mashaka kwa wananchi kutokana na kutoelewa matamko yanayopingana kati ya Serikali na Tamko la madaktari

MTAZAMO
HEBU ANGALIA KATIKA MAKUBALIANO NI LIPI LIMETEKELEZWA HADI SASA?? THEN SERIKALI INAONGEZA MISHAHARA YA WABUNGE, HIVI KARIBUNI UTASIKIA SABASABA!!!
- Jumla ya madaktari wote ni chini ya 15,000 (na hapa namaanisha General practitioners and Specialists). Kwa uchache au wingi wetu tumekwisha kuona madhara ya migomo miwili iliyokwishatokea.Nashangwazwa na kuona baadhi ya watu wanaosema madaktari hatuna utu wala huruma na tunaweka maslahi yetu mbele, hivi mnajua kuwa katika nchi za East and Central Africa, Tanzania ndiyo yenye kulipa mishahara midogo kwa watu wa sekta ya Afya?? Rwanda juzi juzi(1994) walikuwa na vita lakini daktari analipwa 1500USD, au mnadhani hatujui kuna nchi za jirani na mbali tunaweza kwenda kama wenzetu (Mf. Rwanda, Botswana, Zambia, Lesotho, Egypt, SA, nk)???mnadhani kubaki kwetu Tanzania tuteseke kwa kauli eti "UDAKTARI NI WITO?", "WATANZANIA -WATOTO, KINA MAMA, NA WAZEE WATAKUFA IWAPO TUKIGOMA", "OOOH?? HATUTAKIWI KUGOMA"…tumeonyesha uzalendo wetu kwa kubaki hapa hapa na mazingira yetu magumu, lakini sasa IMEFIKA MWISHO..
Pediatrics(wodi ya watoto):Hakuna vifaa vya kuongezea maji/damu mwilini(cannula), hakuna mitungi ya gesi, OBGYN(wodi ya kina mama);hakuna pamba, mipira ya mikojo(urine bags), MOI, Mwaisela hakuna vitanda, Operating Theatre,OT; Hakuna gloves ,mask, kofia za kutosha, Huduma ya mionzi ya CT SCAN ni mwezi wa saba haifanyi kazi(huku mmiliki akiwa anaidai Wizara ya Afya mil.800/=Tsh)na haitakuwepo hadi atakapolipwa.
Kwa madai hayo, si lazima serikali itekeleze all at once, lakini Mshahara unazungumzika, wale mnaofanya interview, huwa hamuulizwi ni kiasi gani unategemea kuanza nacho na waajiri wenu? Doesn't this make salary being negotiable?? Then kwanini isiwe kwetu?
Hivi ulishawahi kusikia MASS RESIGNATION????? It takes ATLEAST 12yrs kumpata huyo specialist after elimu ya sekondari, Halafu nasikia mnasema eti tufukuzwe kazi?Then what??? Kwa wale wenye mtazamo mfupi mnadhani Serikali inaweza ku-import madaktari toka nje..kwa mfano
1.Ni nchi gani itakuazima madaktari?? Kwa mshahara upi na vifaa gani? CUBA-3000USD, RWANDA-1500USD!!!
2.Hypothetically speaking, wakikusaidia madaktari, watakupatia wangapi??
3.Apartment na transport allowances utawapa kiasi gani?
4.Hivi bibi aliye Tandahimba, asiyejua Kiswahili vizuri ataweza kuongea kiingereza na hao doctors??ama utahitaji wakalimani(translators), if so wangapi??? Utawalipa??
5.Then hao madaktari watakaa hapa milele??
Then NASIKIA MTATUPELEKA MAHAKAMANI.
Utawakamata madaktari wote nchini?? Kumbuka huu mgomo hauna kikomo na hauna kiongozi!!!..hypothetically speaking ukitupeleka, tutawatibu tukiwa huko gerezani?? Waliobaki mnadhani watarudi makazini?tukirudi mnadhani tutafanya kazi? Tukifanya kazi unadhani itakuwa katika kiwango kinachotakiwa? With demoralization unategemea tutaponyesha ndugu zetu kweli, au mortality kuwa juu??? Then kwa wanafunzi walio vyuo vya tiba kama MUHAS, WBUCHS, KCMC, UDOM, HKMU, IMTU..watafanya kazi hapa nchini kwa hali hii, ama Brain drain ndiyo itazidi!!
SIASA.
Wananchi walishazoea kudanganywa, na hii imezoeleka na viongozi Fulani kushindwa kufanya wajibu wao kusingizia wanasiasa kadhaa..Hapa HAKUNA siasa ila mkiileta tutawaachia tu kwani huko hatupawezi ila viongozi mjue hakuna tena rufaa ya kwenda nje(mf. INDIA) MUHIMBILI
Hivi wananchi mnajua viongozi wanalipwa kiasi gani wanapoenda nje kutibiwa na familia???
Eti kwa sababu sekta nyingine hawawezi kugoma, ndio na sisi tusigome? Eti kwa sababu askari anayetumia SMG na kupambana na jambazi anayetumia AK47, eti kwa sababu mishahara ya walimu inacheleweshwa, ndio tusigome??? Nani kasema??
HITIMISHO:
HAPA KAZINI HATURUDI…HII IELEWEKE VIZURI…HATURUDI….MGOJA NIIWEKE VIZURI HATURUDI, ACHA MEDIA IENDELEE KUDANGANYA, LAKINI UKWELI TUNAUJUA, MWISHONI MTARUDI TU, NA THIS TIME SI TENA YA KUTUMIA BUSARA ZETU KUWASTAHI VIONGOZI NA KISHA KWENDA PALE KUONGEA NA ‘WAZEE WA DSM"
"Doctors we might be slow walkers, but we never walk back" ..Solidarity Forever
 
Umeanzisha kitu kizuri mkuu na umetoa hoja nzuri tu. Ila sijaridhishwa na heading yako. Ni vema ungekaribisha hata wale wale wanaounga mkono huu mgomo ili uweze kuzipima hoja zako dhidi ya wale wanaounga. Binafsi siungi mkono kwa sababu
1. Hii sekta hawatakiwi kugoma kwa mujibu wa sheria kama ilivyo sekta ya maji
2. Mahakama imezuia. Kama nchi yoyote ile lazima kuwe na ORDER ili mambo yaende
3. Kima cha mshahara cha 3m ni kikubwa kwa nchi maskini kama tz. Hoja ya kwamba wabunge wanalipwa hivi, mara vile haitoshi kuwa kigezo. Mazingira magumu ya kazi ni katika sekta nyingi sana. Walimu, polisi n.k.
Mimi nawachukulia kama wahaini na serikali katika hili inyooshe makucha ili watu waheshimu mamlaka



Anaekandamiza na anaekandamizwa wote huwa hawajui wanalolifanya mpaka mmojawapo atakapo-react. " THE PEDAGOGY FOR OPPRESSED"
 
Back
Top Bottom