RC Malima: Morogoro tayari kufanikisha kambi ya madaktari bingwa wa Dkt. Samia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
866
547
MOROGORO TAYARI KUFANIKISHA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA - RC MALIMA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Alhajii Adam K. Malima amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya uratibu wa kufanikisha kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kanda ya kati ikihusisha Hospital za Rufaa Mikoa ya Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma na Pwani .

Hatua hiyo ni katika kuhakikisha serikali inasogeza huduma za afya karibu na wananchi, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ambapo kambi kubwa ya matibabu ya magonjwa kadhaa linatarajiwa kuanza Mei 6 - 10, 2024 katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro itayoshirikisha madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kutoka Hospital za Rufaa kanda Taifa ikiwemo Benjamini Mkapa Hospital, Jakaya Kikwete Hospital, Hospital ya Mifupa MOI na hospital ya Muhimbili.

Aidha RC Malima pia alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa Habari kisha kutembelea ukarabati mkubwa unaondelea katika hatua za mwisho Hospital ya Rufaa Morogoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufakisha kambi hilo.

"Nitoe wito kwa wakaazi wa Morogoro na mikoa yote ya jirani kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kitabibu, tumejipanga vyema na wataalamu wetu kutoa huduma za wanawake, magonjwa ya watoto, magonjwa ya masikio, Meno, magonjwa ya upasuaji wa mifupa, magonjwa ya upasuaji wa jumla, magonjwa ya ndani (Moyo, Figo, Ini, na matumbo, magonjwa ya afya ya akili, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya macho, huduma za ganzi na usingizi, magonjwa ya mfumo wa mkojo huduma za uchunguzi za mionzi na picha, huduma za utegemao na mazoezi tiba ambapo huduma zote zitatokewa bila malipo"

"Tunamshukuru sana sana Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wema, imani na ungwana wake kuhakikisha kila mtanzania anahudumiwa popote pale alipo sio jambo dogo kikosi cha wataalam Bingwa na Bingwa Bobezi zaidi ya 54 kupiga kambi na kuhakikisha kila mwenye tatizo la kiafya anafikiwa bila kujali gharama na ukubwa wa tiba anayohitaji huu ni zaidi ya upendo mkubwa tutahakikisha tunaitumia vyema fursa hii" Adam Kigoma Malima RC Morogoro

Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya, Mbunge wa Jimbo la Kilombero Asenga Abuubakari kwa niaba ya wabunge wa majimbo ya mkoa wa Morogoro, madaktari wandamizi wa Hospital za Rufaa mikoa ya kanda ya kati, watumishi wa Hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro pamoja na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali.

📍Morogoro.
🗓️ 29 Aprili, 2024.
 

Attachments

 • IMG-20240429-WA0105.jpg
  IMG-20240429-WA0105.jpg
  494 KB · Views: 3
 • IMG-20240429-WA0100.jpg
  IMG-20240429-WA0100.jpg
  468.1 KB · Views: 2
 • IMG-20240429-WA0103.jpg
  IMG-20240429-WA0103.jpg
  343.9 KB · Views: 3
 • IMG-20240429-WA0096.jpg
  IMG-20240429-WA0096.jpg
  159 KB · Views: 2
 • IMG-20240429-WA0098.jpg
  IMG-20240429-WA0098.jpg
  365.7 KB · Views: 3
 • IMG-20240429-WA0097.jpg
  IMG-20240429-WA0097.jpg
  483.1 KB · Views: 2
 • IMG-20240429-WA0093.jpg
  IMG-20240429-WA0093.jpg
  369.7 KB · Views: 3
 • IMG-20240429-WA0104.jpg
  IMG-20240429-WA0104.jpg
  417.2 KB · Views: 2
 • IMG-20240429-WA0101.jpg
  IMG-20240429-WA0101.jpg
  400.5 KB · Views: 3
 • IMG-20240429-WA0099.jpg
  IMG-20240429-WA0099.jpg
  539.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom