Kwa wote tunaopinga mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wote tunaopinga mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MIGNON, Jun 23, 2012.

 1. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Naomba nianzishe uzi mahsusi kwa ajili ya wale wote ambao tunapinga mgomo wa Madaktari ambao unaanza leo.

  Hii itatupa fursa kujadili kwa nini tunapinga Madaktari kugoma na itasaidia wachangiaji wa fani mbalimbali kuelezea kwa nini hawaungi mkono wataalamu hawa kugoma.

  Binafsi naamini kuwa si sahihi kugoma tena hasa baada ya ufafanuzi uliotolewa na Waziri Mwinyi,ni wazi kuwa nafasi ya mazungumzo ipo wazi.

  Serikali imeshaonyesha kutikisika na hii inatosha kwa sasa rudini katika mazungumzo ili muibane serikali kwa hoja.Kauli kama mgomo usiokuwa na kikomo haina tija na inaondoa hadhi ambayo Madaktari wanapewa na jamii.Kauli hii maana yake ni kuwa binadamu wataachwa wateseke na wafe hadi hapo madaktari watakapopata wanachotaka, HAIKUBALIKI.

  Kuna kauli ya kuwa huduma muhimu hazitasimama,hii si kweli kwani katika mgomo accountability itakuwa kwa nani?


  Mapungufu katika vitendea kazi ni mambo ambayo yanazungumzika katika ngazi tofauti na wote tunayajua haya na mengi yanasababishwa na nyie wenyewe Madaktari na nitatoa mfano.Vifaa vinakosekana lakini pesa zinatumika katika mambo ambayo si ya muhimu na muidhinishaji akiwa ni mtu wa fani ya Udaktari.


  Inawezekana kabisa kuwa serikali ina mapungufu yake lakini tuangalie ni nani ataathirika zaidi katika mgomo huu,ni wazi kuwa watu maskini wa kipato cha chini wataumia zaidi.
  Ogopeni siku watu wa hali ya chini watakapoamua kuchukua hatua,hapatakuwa na pa kujificha.

  He who fights and run away lives to fight another day.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hujasikia ma bilions yanaliwa kiwira?madaktari wakiboreshewa ndio mwanzo wa kuboreshewa wafanyakazi wa fani zingine
   
 3. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi akili yako umeificha kwapani au ndo unatumia miguu kufikiria? Usitegemee kuungwa mkono kwa huu ujinga wa Mwigulu.
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Muanzisha uzi huelewi, wewe huijui serikali ya jk kuwa ni dhaifu na wasanii? Katika mazungumzo ambayo yalijadiliwa na wawakilishi wa serikali na madaktari ni kuwa ni tofauti na yale ambayo Hussein Mwinyi kasema ni yale ambayo kamati ya serikali iliyagomea, sasa Mwinyi anahangaika baada ya kuona maji yamefika shingoni, kikubwa tunachotaka ni kuwa serikali iwe committed kujadili swala hili na iwe na dhamira ya kweli na siyo usanii ambao wanataka kuufanya sasa ambao utawacost.
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Umeanzisha kitu kizuri mkuu na umetoa hoja nzuri tu. Ila sijaridhishwa na heading yako. Ni vema ungekaribisha hata wale wale wanaounga mkono huu mgomo ili uweze kuzipima hoja zako dhidi ya wale wanaounga. Binafsi siungi mkono kwa sababu
  1. Hii sekta hawatakiwi kugoma kwa mujibu wa sheria kama ilivyo sekta ya maji
  2. Mahakama imezuia. Kama nchi yoyote ile lazima kuwe na ORDER ili mambo yaende
  3. Kima cha mshahara cha 3m ni kikubwa kwa nchi maskini kama tz. Hoja ya kwamba wabunge wanalipwa hivi, mara vile haitoshi kuwa kigezo. Mazingira magumu ya kazi ni katika sekta nyingi sana. Walimu, polisi n.k.
  Mimi nawachukulia kama wahaini na serikali katika hili inyooshe makucha ili watu waheshimu mamlaka
   
 6. w

  wikolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu mleta mada, wewe ni daktari? Unajua wakati mwingine mtu anapokuwa na shida na analalamika yule asiyekuwa na shida huchukulia kama kawaida tu. Mtu huyu huona kama shida za mwenzake ni za kawaida na zinaweza kuvumilika au kusubiri majadiliano! Hebu jiweke kwenye nafasi ya madaktari halafu ufikirie mara ya pili mkuu!
   
 7. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Mimi ni Daktari na naelewa fika unachozungumza ila nashindwa kuelewa daktari anaposema mgomo usio na kikomo.
  Pia kama umesoma vizuri nimejaribu kueleza kuhusu kuhusika kwa madaktari wenyewe katika mambo yanayotokea.Mkuu wa Muhimbili ni Dakatari na anaacha kuhangaikia CT scan ifanye kazi lakini tujiulize ameidhinisha malipo mangapi amabayo hayakuwa na umhimu kama CT scan.
  Pili idara za Afya katika mikoa na wilaya zinaoongozwa na madaktari na kuna vitu kama basket na revolving funds,nenda kaangalie matumzii ya hizo pesa kama kweli yana justify kusimamisha operations kwa sababu nyuzi za kushonea hakuna?
  Mkapa aliwahi kuuliza kuwa watu katika fani mbalimbali wanajisimamiaje katika suala la rushwa na napenda madaktari wenzangu tujitizame,wote waliongia kwenye utawala fani ya udaktari wameiacha nje na hawa ndo adui mkubwa kuliko hiyo serikali.
   
 8. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Ni bahati mbaya ndani ya jamiiforum hatuweki vyeo kama wanajeshi au askari.Naamini ungenipigia saluti si kwa mkono mmoja ila miwili.Jiheshimu.
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  haki haipatikani ila kwa ncha ya upanga, hii keki ya taifa lazma tugawane wote si wachache wale kubwa wkt hawafanyi kazi ngumu, wengine wahenyeke usiku na mchana halafu wapewe kidogo. WAKATI MWINGINE UBABE UNATAKIWA ILI MAMBO YAKAE SAWA
   
 10. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hapo ndo kabisa umetumia tumbo kufikiria! Cheo JF cha nini? Mi unanijua? Hapo unaonesha jinsi gani ulivyo hujiamini unaamua kutumia "authority protection"
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kumbe we mwanajeshi. Siku zote mtu akiingia jeshini huwa anaacha akili zake getini zinaendelea kuoza. Hivi unadhani bajeti anayopelekewa marina inatosha kununua ct? Mbona umesahau kwamba hospitali za wilaya zinaagiza dawa msd miezi sita bila kuletewa? Siku zote mkishakuwa kwenye neema huwa mnasahau wenye shida. Hivi hayo mazungumzo yanawezekana leo na walikuwa na miezi mitatu? Kwa nini waje kuanza kuomba mazungumzo dakika za mwisho? Huu ni utani na udhaifu ambao hatutaki wauendeleze.
   
 12. j

  jigoku JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  POLISI,kuna mambo huyajui wewe,ukisoma volume za jeshi la wananchi jwtz,INAKATAZA KUGOMA NA MOJA YA ADHABU YA MWANAJESHI ANAEGOMA AMRI HALALI ZA KIJESHI NI KUPIGWA RISASI,Lakini miaka ya 96/97 kikosi cha 942 KJ ni kikosi cha mizinga ya 122 mm howtzer na wanatumia pia mizinga ya 130 mm,askari private waliwahi kugoma pamoja na ukubwa wa adhabu hiyo pale ambapo walipoona wamekandamizwa haki zao.na askari private hao walikuwa ni single namaanisha walikuwa wakiishi kwenye mahanga,na ni vijana ambao walikuwa wametoka mashuleni ambao walikuwa walikuwa wanalitizama jeshi kisayansi zaidi.
  Hoja yangu ni sheria zingine zimliwekwa ili kuwakandamiza watu,mfano sheria haiwaruhusu madaktari kugoma,fine lakini je mnawatimizia mahitaji yao,je mnatimiza wajibu wenu kama mwajiri?au mnawafanya ndondocha tegemezi kama mlivyowafanya waalimu?maana walimu ni waoga,hawana confidence na wengi ni wa kuunga uunga,sasa kada hii ya madaktari kuweka kigezo cha kutokuruhusiwa kugoma wakatia wewe mwajiri huwajibiki kwangu naona ni upuuzi wala hatuwezi kutatua jambo hili kwa vitisho,kugoma watagoma na vifo vitaongezeka.
  Polisi usirudie tena kusema nchi hii ni masikini hivyo haiwezi kulipa sh millioni 3,hoja yangu ni kusema TZ ni masikini,usiongee hivyo kwa watu wenye uelewa wao na wale wasio mafisadi,maana imekuwa ni wimbo wa mafsiadi kuwa nchi hii ni masikini,wakati wao wanazidi kuneemeka kwa kushirikiaana na cd inayoitwa uwekezaji,nchi hii sio masikini ila ni masikini wa fikra za viongozi wa chama tawala Nyinyiemu.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kugoma kisheria. Na mahakama imetoa ufafanuzi.

  Kama wanaona kazi hiyo haina manufaa watafute kazi zingine za kufanya.
   
 14. s

  sahini Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana kusema kuwa hawatakiwi kugoma unakosea,hawa watu wanahitaji basics katika maisha yao.Ningekushauri ukasome historia ya utabibu ndo ungeweza kuwaelewa wanaishije leo. Lakini kwenye msafara wa mamba hata kenge wanakuwemo sishangai.
   
 15. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kuna usemi unasema kuwa anayevaa kiatu ndo anaejua kama kinambana au la. Kwa taarifa yako, watu wengi tu wanakufa kila siku mahospitalini hata kama madaktari tuko kazini kwa sababu ya kukosekana madawa na vifaa muhimu kwa ajili ya tiba. Madaktari wa Tanzania tumeshazoea kuona watu wanakufa kila siku, it happens a lot, na sio kwa sababu hatuna utaalamu au ujuzi wa kuokoa maisha ya watu, la hasha. Mtu anakufia mikononi simply because hakuna adrenaline, a very affordable and cheap but necessary rescusitation drug. Juzi tu hapa hospitali ya taifa ya muhimbili iliishiwa urine bags for days....... just imagine the so called hospitali ya taifa inaishiwa urine bags, na inabidi ile mirija ya mkojo(catheters) iunganishwe kwenye gloves!!!!!!
  Watu tumeshapiga surgeries kwa kutumia simu za tochi,in the worst environment ever, nimeshawahi kushuhudia wagonjwa wanakufa ICU kwa sababu tu kulikuwa hakuna mitungi ya oksijeni to sustain their lives. Anyways...... my point hakuna daktari wa bongo anaetetemeka kwa kauli za "mama zetu na baba zetu watakufa kwa kukosa huduma zenu kipindi cha mgomo" because they die anyway whether tumegoma or not kutokana na ukweli kuwa serikali imeipuuza sana sekta ya afya....... TUNATAKA TUTOKE HUKO KWA GHARAMA YEYOTE ILE!!!!!
   
 16. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
   
 17. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo tunacopy sheria kutoka nchi zilizoendelea , halafu tunazitumia vibaya kukandamiza wananchi wakiwamo madakitari, niambie kama kweli tuna healthy and safety law hapa tz, na kama ipo haina nguvu, unatakata madakitari wajipinde chini kumhudumia mgonjwa aliyelala chini, kutokana na ukoseu wa vitanda, ila inawezekana kwa serikali kununua mashangingi kwa ajili ya kuendea ofisini, ila haiwezekani kununua vitanda mahosipitalini, halafu unaleta mujibu wa sheria, Je huo mujibu wa sheria nao unawatendea haki madakitari kwa yale wanayopaswa kupewa ??
   
 18. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Madai yote ya madaktari nayaona ya msingi isipokuwa hili la mshahara milioni 3.5!!
   
 19. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Najua baadhi hawaelewi Madaktari wana nia gani na nchi hii,kama ilivyokuwa wakati harakati za kugombea uhuru zilizoongozwa na Late J.Nyerere,baadhi ya watz walimpinga,hata hawa wanaowapinga now, watakuja kuwaelewa,.Madaktari daima mbele nyuma mwiko,ninyi ndio tegemea na chachu ya mabadiliko ya nchi hii inayozama..
   
 20. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Naomba niandike kwa upole mkubwa.Yote unayosema ni ya kweli lakini ninakumba usome thread hii kwa makini.Nimeeleza ya kuwa serikali imetikisika na ni kwa advantage ya madaktari kwani tayariwan upper hand katika jambo hili.Hoja yangu kuu ni kuwa waitumie fursa hii vizuri,wa retreat,wajadialiane ili waweze kupata wanchohitaji.
  Jambo la pili ni kuhusu watu tunavyoyachukulia mambo kirahisi.Hebu fikiria mwanao mpenzi anaumwa hoi na madaktari wamegoma muhimbili wapo canteen wankunywa chai,soda na wanajadiliana,je utakwenda kuwapa offer?Tuwe realistic ndugu zanguni ni maskini ndo wanaoumia zaidi na tusijiweke katika mazingira ya kuwa sisi ni indispensable.
   
Loading...