Dr. Mollel: Tanzania ina madaktari bingwa wazalendo 2469 waliosajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 7, leo Septemba 6, 2023.


Madaktari Bingwa wazalendo Nchini Tanzania
Akijibu swali la Angelina Malembeka, Mbuge wa viti maalumu (CCM), Naibu Waziri wa Aya Dr. Mollel amesema Tanzania ina madaktari bingwa wazalendo 2469 ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) kwa fani mbalimbali za udaktari.

Kati ya hao, madaktari 2098 wapo sekta ya umma na 371 wapo sekta binafsi. Wote wamegawanyika katika maeneo 28 ya ubingwa.

Utoaji wa Vitambulisho vya NIDA
Hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2023 jumla ya Watanzania 11,242,736 wamepewa vitambulisho sawa na asilimia 55 ya lengo la kuwapatia wananchi 20,294,910 wanaostahili kupewa. Mpango wa Serikali ni kuwagawia vitambulisho watanzania 9,052,174 waliobaki ifikapo mwezi Machi, 2024.

Upungufu wa mashine za kutoa vitambulisho hivyo ndio sababu ya kuchelewesha zoezi hili, hata hivyo kwa sasa Serikali imepata mashine bora zinazoweza kukamilisha zoezi hili kwa ufanisi.

Aidha, upo mpango wa kuuunganisha vitambulisho vyote kuwa kitambulisho kimoja kinachoweza kutumika sehemu mbalimbali ikiwemo NIDA, Benki, paspoti n.k

SERIKALI HAITAMBUI GUNIA KUWA KIPIMO BALI NI KIFUNGASHIO

Waziri wa Viwanda na Biashara amesema Kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo “The Weights and Measures Act (Amendment) Order, G.N. No. 725 of 2018”, kifungu cha (2) (b) cha Jedwali hilo ambacho kinasema Mazao ya Mashambani yatafungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu 100 pamoja na kuelekeza Wauzaji/Wanunuzi wa Mazao kutumia Mizani

Ameeleza, Serikali haitambui Gunia kuwa kipimo bali ni kifungashio. Hivyo, wadau wote waepuke matumizi ya Gunia kama kipimo kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Vipimo.
 
kuna wakati nikiliangalia hili bunge wakivaa manguo yao na kujifanya kujadili mambo, nakubaliana na waliosema DP WORLD wangepepaswa wabinafsishwe hili bunge waliongoze au hata wakitaka walipeleke Dubai poa tu. wanakera kupita maelezo.
 
Tatizo lililopo kwa sasa sio la hawa madaktari wa kupima malaria na typhoid (parasitic deseases)
Tatizo liko sana liko kwenye diagnosis ya magonjwa ya mmeng'enyo (metabolic deseases) na magonjwa ya mifumo ya hormoni na neva za fahamu.
Serikali sasa inapaswa kujengea uwezo madaktari kwa kuzalisha madaktari finyishi (super specialist) kwa kutumia kati ya Bilioni mbili hadi tano kwa mwaka kugharamia mafunzo katika nchi za India, Marekani na Ulaya.
 
Back
Top Bottom