Ukiwa na miaka 50 na huna nyumba ya kupangisha kibiashara kama fremu (sio kuishi) au lodge basi wewe huna uzoefu ni hatari kuingia biashara hizo.
Chukua hela ya kula uzeeni kama ni milioni 50 nunua government bonds za miaka 20. Return yake ni kama 13% na coupon payments ni mara mbili kwa mwaka kwa hiyo utakuwa unapata kama milioni 6 na point hivi kwa mwaka. Ambavyo unalipwa nusu mara mbili, hivyo ni milioni 3 nusu ya kwanza milioni 3 nusu ya pili. Kwa mwezi ni kama laki 5 na elfu kadhaa hivi.
Hiyo ni hela ndogo sana ukiwa na miaka 50, ila kwenye 60 kwenda 70 matumizi ya fedha yanapungua. Na hapa kumbuka tunaweka options what if dunia itakukataa, si kwamba huna vitu vingine.
Kwenye hiyo bond ya miaka 20, unaweza kopea kiasi chake kisichosizidi 60% theoretically, ila tufanye 50% ya 50M ambayo ni 25M hapa ni mfano umeumwa sasa unataka operation na huna hela usiuze nyumba. Ila baada ya hapo coupon zitakuwa zinaenda benki kulipia deni.
Bond inatoa hela kidogo ila ya uhakika. Waliojenga nyumba za kupanga zikaungua, zikabomolewa, wakatapeliwa kiwanja, wakagombea mali kwenye taraka, wapangaji wakakosa, au nyumba ikalipa vizuri sana wapo. Ila tangu Tanzania ianzishwe haijawahi default kwenye debt obligations, ingawa inawezekana ikitokea kuna vita au sasa serikali iongozwe na mbumbumbu non-stop kwa miaka kama 20 hivi.
NB: Nimehariri kuongeza kuwa. Ukifanya hivyo na miaka 50, after 20 yrs una miaka 70 utapokea hela yako ileile 50M au kama haupo taratibu za urithi zipo. Ila utakuwa ndani ya miaka 20 umekusanya kama (kodi) ya 130M hivi. Same way na ukijenga ila sasa huku hakuna bomba kupasuka, mpangaji kufiwa, au dalali kusema hali ngumu.