Zembea yote lakini siku za uzee wako usiwe omba omba. KIUFUPI UWEZE KUJIMUDU. Uhakikishe una usafiri unaoweza kukupeleka popote (kama siyo humu Tz basi angalau hata hapo Dar au mkoa wowote uliomo), uwe na uwezo wa kumlipa dereva akuendeshe, uwe na uwezo wa kujigharamia matibabu, ikitokea shida kijijini ukatoa salio usibaki na mawazo kichwani. kwa sisi RC, ukienda kanisani ushiriki kikamilifu kwenye UWAKA, Jumuiya nk. Ikitokea michango ya ghafla, mwanaume uweze kusimama na kutoa kauli bila kuyumba nk. Ukichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya uweze kumudu majukumu.....
Wanaume wengi tunaondoka duniani kwa sababu ya msongo wa mawazo na uchumi hafifu. Tuliobahatika kufika kwenye 40+, tujitahidi sana kutengeneza uchumi imara. Maana ukweli usiopingika ni kwamba, tunakokwenda ni mbali zaidi kuliko tulipotoka. Bila pesa, maisha hayana ladha kabisa.
Mwisho mwanaume ukiwa na uchumi imara, hata nyumba yako itakuwa na upendo. Mama mtaheshimiana na mtaishi kwa upendo. Watoto mtatembeleana vizuri.
Sasa wewe jichanganyanye! Utatamani dunia uikimbie kabla ya mda wako uliopangiwa.