Kwa wapenzi wa documentaries

Kwa wapenzi wa documentaries

Nitazipataje mkuu Na mm n mgojwa sana was doc
nyingi mi huwa nadownload torret na pc sijajua kwa smartphone. au kama unanet yenye nguvu unaweza cheki kupitia youtube. kutumia torrent kuna tuprocedure. unaweza kusoma net jinsi ya kutumia torrent.
 
kuna nyingine ya history chann inaitwa the true carrebean pirates. kumbe maharamia hao walianzishwa na waingereza kupambana na waspanish kama al qaeda walivyoanzishwa kupambana na wasoviet!. ina story nzuri sana ndani yake.
 
Mkuu kama umeipenda hiyo nakushauri pia utafute Bowling for Columbine, Sicko na Capitalism, a love story ambazo zote ni za Michael Moore.
nimeicheki sicko. ni nzuri sana michael ana guts sana na anajua kuorganize kazi yake. shukrani sana.
 
Air crash investigation (series) - imetengenezwa na National geographic - Inahusu uchunguzi wa vyanzo vya ajali za ndege (pamoja na simulizi kutoka kwa survivors) - kwa sasa siangalii tena kwani zilinifanya niwe naogopa kupanda ndege.

Hiyo nimeangalia daah ajari nomaa. Pia nazipenda documentary za BBC kuna moja nimeangalia inaitwa "life is race against time" hii inaelezea ni jinsi gani maisha yana badilika kulingana na muda unavyoenda.
 
nimecheki dokumentari mbili za history channel. moja inaitwa the true story of troy. inajaribu kutafuta ushahidi na kuelezea trojan war. nyingine inaitwa inside islam. hii inazungumzia historia na kile waislamu wanaamini.
 
nimeona nyingine inaitwa urbanized. hii inazungumzia ukuaji wa miji, matatizo yake na upangajji wake.
 
detroopia, hii inazungumzia jinsi mji wa detroit unakongoroka baada ya viwanda vya magari kuanza kufirisika.
Detropia.png
 
chimpanzee, inafuatilia maisha ya sokwe mdogo aliyefiwa na mamayake kwenye misitu ya ivory coast.
chimpanzee.jpg
 
ivory tower, inazungumzia bei ya elimu ya vyuo vikuu huko marekani.
20140428190004%21Ivory_Tower_poster.jpg
 
We Steal Secrets The Story of WikiLeaks(2013)
Hii inaelezea Maisha ya bwana Julius Assange mpaka kuanzisha mtandao wake wa wikileaks.
Kwa kweli ni nzuri sana.
We Steal Secrets The Story of WikiLeaks [GlowGaze.Com].jpg
Terms and Conditions May Apply (2013)
Hii inaelezea jinsi makampuni na serikali wanavyotumia taarifa zetu za kwenye mitandao kwa manufaa yao.
Hii nayo ni nzuri pia.
terms.jpg
 
hii niliwahi iona, zile ishu hata hapa zinaeza kutokea. niliona nyingine zina husu civil war huko sierra leone, ukiziona lazima ufreeze.

Niliwahi ona ya Sierra Leone inaitwa Cry Freedom inahusu ile civil war ya 1996 dah, vita isikie tuuuu
 
Mimi hupenda pia kuangalia True Stories ya DSTV. Zinamwelekeo wa kuwa dicumentary.
 
Hawking, hii imetoka 2013. inazungumzia maisha ya mwanafizikia stephen hawking ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza kwa motor neurons.
fisico.jpg
 
the central park five. watoto watano wa miaka 14-16 wanahukumiwa kwa kesi ya ubakaji mwaka 1989. miaka 13 baadaye wanagundulika hawana hatia.
CentralParkFiveBlog.jpg
 
Entebe Raid. Hii inahusu Israel soldier jinsi walivyowaokoa wayaudi wenzao waliotekwa na terrorists yani ni one of my favorite. Napenda documentary zinazohusu wars, terrorism, spying etc.

Nyingi huwa naangalia kupitia documentary heaven. http://documentaryheaven.com/
 
1. City of God, Guns and Gangs - Rio De Jeneiro - angalia uone mshike mshike wa huo mji.
2. How to rob africa- jinsi US na Ulaya wanavowashutumu wviongozi wa africa kwa ufisadi wakati pesa hizo za kifisadi zinatuzwa kwenye accounts za bank zao hukohuko.
3. bood coltan (damu ya wacongo inavyoneemesha dunia kwa smartphones)
4. the perfect vagina - jinsi wadada wa uingireza walivyo na inferiority na muonekano wa nyeti zao kuishia kufanyiwa plastic surgery.
5. blood diamonds - inaelezea vitu vilivyo nyuma ya umwagaji wa damu west africa
6. Ghosts of Rwanda - utaongeza kitu kuhusu rwanda,UN na marekani

kwa wapenzi tembeleeni Top Documentary Films - Watch Free Documentaries Online, hapo zipo za kutosha zikiwemo hizo hapo juu.
 
Back
Top Bottom