Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Kama ni mpenzi wa documentaries share nasi baadhi kati ya ulizoangalia. Itapendeza ukitueleza kidogo inahusu nini. Mimi naanza na darwins niightmares.
Hii imetengenezewa Mwanza Tanzania na inazungumzia jinsi samaki wasivyo nufaisha wenyeji.
wewe umeona zipi?
Hii imetengenezewa Mwanza Tanzania na inazungumzia jinsi samaki wasivyo nufaisha wenyeji.
wewe umeona zipi?
Kumbe JF pia kuna wapenzi wa documentaries. Huu mimi ni ugonjwa wangu, napenda zaidi Documentaries kuliko hata movies. Kali nilizoziona mpaka sasa ni :
1.Bowling for Columbine (Kuhusu wanafunzi wa Columbine high school, huko Colorado USA walivyowaua wenzao na gun culture huko
Marekani kwa ujumla)
2.Inside Job (Kuhusu nani hasa walihusika kusababisha global financial crisis mwaka 2008)
3.AIDS Inc. (Kuhusu jinsi ambavyo tatizo la Ukimwi limegeuzwa kuwa la kisiasa na si la kiafya)
4.Fahrenheit 911 (Kuhusu jinsi wamarekani walivyoongopewa na serikali yao mpaka wakakubali kuvamia Iraq baada ya matukio ya 9/11)
5.The smartest guys in the room (Kuhusu jinsi Kampuni kubwa ya nishati ya ENRON ilivyoporomoka)
6.Capitalism - a love story (Hii ni kama Inside Job hapo juu)
7.Religulous (Bill Maher ana-exprole imani za dini mbalimbali kubwa duniani)
8.Sicko (Inahusu jinsi gani mfumo wa huduma za afya nchini Marekani ulivyokuwa mbovu)
9.How to get rich selling drugs (Hii inajieleza yenyewe, utakutana na wataalamu wa shughuli hizo)
10.Inside the American Mob (Part 1-6) (Kwa wale wanaopenda kujua kuhusu historia ya American Mafia hizi zitawafaa)
11.The Grizzly Man ( Timothy treadwell aliwapenda sana Grizzly Bears wa huko Alaska, akaenda kuishi sehemu wanazoishi ili kufuatilia
maisha ya na "kuwalinda". Akaja kuuawa, na Bears hao hao aliokuwa anawalinda!)
12.Documentaries zoote kuhusu Tupac
13.Something from nothing: The art of Rap ( Hii inahusu history ya muziki wa rap)
14.Welcome to Deathrow ( Historia ya mojawapo ya hip hop record label zilizopata umaarufu mkubwa)
15.Beef (Part 1-4) (Huhusu historia ya beef (malumbano) kwenye muziki wa rap)
16.Chasing Maddoff (Whisleblowers waliokuwa wakimfuatilia tapeli Bernard Maddoff)
17.The Carter Documentary (Maisha ya Lil Wayne)
18.Living with Michael Jackson ( Mwandishi wa habari Martin Bashir alipewa nafasi ya kuishi na Michael Jackson kwa miezi 6)
19.Backstage (Roc-a-fella, Ruff Ryders Hardknock Life Tour)
20.Street is watching ( Documentary ya kwanza ya Jay Z)
21.Fade to black ( Pia ya Jay Z)
Na nyingine nyingi siwezi kutaja zote.