Kwa wanaume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanaume

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Jun 7, 2010.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  Naomba kuuliza kwa w/ume hasa waliooa

  Sisi uwa hatuna vitu kama kitchen Party za kufundishwa, Je tuishije na hawa wenzetu?

  1. Kwa kumpa uhuru m/mke wa kupanga mambo yote ya kifamilia?
  2. Mwanaume kuwa ndie sauti ya mwisho katika familia?
  3. Mfumo wa kidikteta (baba akisema ndio linalofuata na hamna kupinga)
  4. N.k (mifum mingine)

  hebu tujadili hapa ni mfumo gani mzuri wa kuishi na hawa wenzetu maana ukimpa mamlaka sana tatizo, ukimnyima mamlaka tatizo tufanyeje?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kweli hapa ni kwa wanaume ..natanguliza shukrani kwa heri FD
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HAKUNA MFUMO wa moja kwa moja!
  kwa namna ile ile watu wanavyotofautiana status kuanzia uchumi,akili,namna walivyotongozana,siku ya kwanza waliongea nini,ahadi walizopeana n.k n.k NDO IVO IVO mapenzi/maisha ya wanandoa wanatofautiana!
   
 4. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Fuata mila na desturi za jamii yako pamoja na mafundisho ya dini yako ukiweka utandawazi ndani yake umeliwa
   
 5. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  yaani unataka tukubaliane juu ya system ya kutumia, mi naona itakuwa ngumu sana we tumia mfumo unaoona unafanya kazi kwa upande wako. Binafsi baba ndio kichwa cha familia kwa hiyo if I say yes ni yes na kama no it means no.
   
 6. chiko

  chiko JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
   
 7. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  hiyo nimeipenda sana if YES ni Yes if NO ni No

  kuna jamaa yangu nimeona life analoishi na mkewe limenishangaza kidogo maana jamaa anaishi kama jeshini akiingia home mkewe hata kama alikuwa jikoni lazima atoke mbio kuja kumpokea na kumwamkia kabisa
   
 8. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  karibu tena na mabangili yako
   
 9. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mie nilijua wakaka mtamwagiana kitchen party humu.......mmezuga balaa!...eti hamna formular...mbona hata sie wanawake tunatongozwa tofauti na tunaishi na nyie wanaume tofauti na bado imekuwa kama sheria,ukiolewa lazima upitie kitchen party...

  am drunk!:twitch:
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mwanaume ndiye kichwa cha nyumba/ndoa, mwanamke ni ubavu..mwanaume aliumbwa na Mungu kutoka kwenye udongo kabisa akapuliziwa pumzi ya uhai na Mungu mwenyewe, mwanamke aliumbwa kutoka kwenye ubavu uliochomolewa toka kwa mwanaume ambaye tayari alishakuwa ameumbwa...Mungu mwanzoni alimwumba tu mwanaume, mwanamke alikuja kuubwa baadaye baada ya kuona mwanaume/adam amekuwa bored mno anahitaji mtu wa kuongea naye, kulala naye etc na kuijaza dunia ndo akasema si vyema mtu akae peke yake nitamfanyia msaidizi...inawezakana kabisa kuwa kama Mungu angeamua, asingemwumba kabisa mwanamke...

  mwanamke alilaaniwa na Mungu kuwa siku zote atakuwa na tamaa kwa mumewe...wivu lazima unao kwa mumeo.....mwanamke ameamrishwa kumtii mumewe wakati mwanamme amelazimishwa kumpenda (sio kumtii) mkewe,....hivyo ni lazima mwanaume ndo awe boss wa nyuma, kama mwanaume si boss wa nyumba, uyo mwanaume hafai hata kuwa kiongozi kama ameshindwa kumtawala mkewe na familia yake atawezaje kuwatawala walioko chini yao?

  niko tayari kupokea marungu toka kwa wanabeijing hapa, najua mtakuja juu...lakini nipo hapahapa kumbana nanyii....
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Cha msingi ni kushirikiana kama wana timu moja.
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kushirikiana kivipi?..cha muhimu ni mmoja kuongoza familia period....mmoja boss mwingine msaidizi anayefanana naye....ukileta kulegea itabidi wote mvae siketi na mtandio.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kushirikiana ktk mambo yote. Kwenye kulea watoto, kwenye kufanya maamuzi, kwenye mawasiliano, kwenye kutunza mji wenu, n.k. Hayo mambo ya mmoja awe ndio kibosile na mwingine msaidizi mimi siafikiani nayo. Mke au mumeo ni mshirika wako ktk maisha. Kushirikiana ndio kunafaa. It's all about team work.
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  umeoa lakini, usijekuwa unaongelea uzoefu wa wenzio?
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hali yangu ya kindoa haijalishi.
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,731
  Likes Received: 647
  Trophy Points: 280
  Hata timu huwa ina Manager na Captain. Cha muhimu ni kuelewa nani ni kiongozi wa hii entity inayoitwa familia na huyu siyo mwingine ni baba wa familia.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi nazungumzia team work i.e. where the players play as a team and not as individuals.

  Na kwenye ndoa mke na mume wote ni viongozi.
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Na kwa kuongezea alichosema NN, Team work ndio hupelekea mafanikio.. huyo anayesema kuna sijui boss au meneja? Wengine wasipofanya kazi utakuwaje meneja?
  Hata kiongozi asipokuwa na followership/wanaoongozwa, ataongoza hewa?
  Mfano mzuri ni timu ya mpira... kuna mpangilio au mgawanyo mzuri sana wa roles.. ukijiona wewe ni bora zaidi kwa vile wewe ni mfungaji, wenzio wasipokupasia mpira utafunga hewa?

  Tukija kwa wanandoa, baba anaweza kuwa kichwa/kiongozi - captain. Haina ubaya na ni vizuri sana maana kila hali inahitaji kiongozi.Ila kuwa kiongozi haina maana kukandamiza au kuburuta wengine.Ukifanya kosa hilo ujue mwenyewe utaumia..hutafurahi uongozi wako, hutapata ushirikiano, na pia ujue u will be the most unpopular figure in your family.Kumbuka utaleta ubabe uwapo kijana, uzee ukiingia ubabe uliowekeza utauvuna na utalia mwenye kwa jinsi watakavyokutenda hao hao unaowanyanyasa.Mifano ipo mingi sana.Ogopa kuonea hasa watoto.. wakikua utajilaumu na hawakawii.
   
 19. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mama, hakuna mtu anayeweza kuonea watoto wake damu yake...huo utakuwa upunguani..ninachopinga mimi ni usawa wa beijing..na ndio maana niliongea vile...ya kwamba, baba ni kichwa cha nyumba, mama ni msaidizi wa baba...hatushindani ndani ya nyumba kila mtu anajua wajibu wake....ndio maana hata sheria za nchi yako zinamlazimisha baba kumtunza mkewe hata kama mkewe anapesa, mumeo analazimika kukununulia vitu ndani ya uwezo wake, kukulisha, na mahitaji yote ya lazima kulingana na kipato chake...ndio maana ya laana waliyopewa wanaume ya kupigwa jua wakitafuta pesa kwaajili ya mkewe na watoto...nyie wanawake ni msaada tu wa kuchangia pale ambapo kichwa kimefanya ndio maana mnatakiwa kumsikiliza kichwa...don't be blinded kuwa ukizeeka utapata shida...labda wewe kama unawanyanyapaa wazee wako...haiko hivyo...una wajibu wote wa kuhakikisha watoto na watu wote ndani ya nyumba yako wanakuwa na adabu na ustaarabu kama hutafanya hivyo utapata shida na haohao watoto wako baadaye na watakuja kukulaumu kuwa haukuwaelekeza kwenye njia sahihi....sijasema kushirikiana hakupo, kupo, ila mmoja ni boss meingine msaidizi..ofisi hapo inaenda.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aisee tone yako ni mbaya unaposema "mmoja ni boss".....it just doesn't sound right to my ears. In a marriage, both husband and wife are supposed to be co-bosses, if I may use your term. This doesn't mean that the wife can also do oil changes and the like. Not at all (though if she can why not)....What I mean is that both of you should treat each other fairly, you should respect each other, and love each other equally and also understand your roles as husband and wife. But to say one is the boss so who/what is the other half supposed to be - subordinate? Come on man...what kind thinking is that?
   
Loading...