Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,455
- 52,095
Hakuna mzalendo tangu 1995! Tulipinga humu awamu ile kujinasibu ni wazalendo wenye uchungu na Nchi lkn kibaya zaid awamu hiyo ikapitisha sheria bungeni ya kuwaongezea kinga mihimili mingine. Hapo ndipo niliona hakuna nia njema dhidi ya kupambana na wabadhirifu na mafisad!!!KWA WALIOTUNGA SHERIA HII; KAMA RAIS NI MZALENDO NA MUADILIFU NI SABABU GANI IKAWEPO KINGA YA KUTOSHTAKIWA?
Anaandika, Robert Heriel
Kwa sasa Dar es salaam
KATIBA hii ya Jamuhuri ya muungano wa Tz, na CCM ndio jinamizi la watanzania kutopata maendeleo ya haraka,Kumbuka Marais wa Afrika kuwa wachafu ni lazima ndio maana KATIBA haziwagusi asikudanyanye mtu.KWA WALIOTUNGA SHERIA HII; KAMA RAIS NI MZALENDO NA MUADILIFU NI SABABU GANI IKAWEPO KINGA YA KUTOSHTAKIWA?
Anaandika, Robert Heriel
Moja ya sheria inayonifanya nione nchi yetu bado hatuko serious ni sheria inayomkingia Kifua Rais KUTOSHTAKIWA. Kwa kweli sheria Hii sio tuu ni ya ajabu Bali ni sheria iliyolenga kumfanya Rais aabudiwe, awe mungu mtakatifu, Wakati kimsingi sivyo.
Hakuna mzalendo tangu 1995! Tulipinga humu awamu ile kujinasibu ni wazalendo wenye uchungu na Nchi lkn kibaya zaid awamu hiyo ikapitisha sheria bungeni ya kuwaongezea kinga mihimili mingine. Hapo ndipo niliona hakuna nia njema dhidi ya kupambana na wabadhirifu na mafisad!!!
Kuna chawa fulani wachache ndiyo waliipenyeza kwa manufaa yao binafsi, wakimpotosha Rais akaharibu linakuwa lake na kwakuwa sheria inamlinda basi na yeye Rais anajibanza hapoRais kama binadamu wengine anaweza kufanya Makosa na uhalifu kama wanavyofanya wengine. Ni muhimu sheria Hii ikaondolewa.
Hatutaki kuchagua Rais ambaye atakuwa na kinga akifanya uhalifu au Makosa. Hilo hatutaki. Ninapotumia wingi ninamaanisha Watu wote wenye fikra na mtazamo kama wangu.
Kitendo cha Sheria hiyo kumkinga Rais asistakiwe automatically kinawakinga na vipenzi wa Rais husika. Ikiwa Rais ambaye ni Kiongozi wa nchi sheria inamlinda basi kimantiki ni kuwa sheria hiyo itawalinda na vipenzi wa Rais.
Sheria hiyo pia inawapa ugumu Mahakimu na majaji kufanya kazi Yao vizuri hasa katika kudili na kesi Kwa baadhi ya Watu hasa vipenzi wa Rais. Hii itafanya Na kuwaingiza Mahakimu na majaji katika Wakati mgumu katika kutoa Haki pindi wafanyapo kazi zao.
Hiyo ni akili ya ma ccm ya kulindana, na ndio inayotuletea hawa machawa wa sasa!.
Washachoka kifikra maan dunia ya sasa sio ile ya 5-2-1977!!Ni kweli Kabisa.
Kwenye nchi na jamii yenye Haki na uungwana hakuna aliyejuu ya sheria. Kwamba huyu anaweza kupelekwa Mahakamani, lakini Yule hawezi kisa anacheo Fulani. Lakini kosa kafanya. Hivi hizi Akili huwa zinatokaga wapi? Ni Akili za ajabu
Kuna chawa fulani wachache ndiyo waliipenyeza kwa manufaa yao binafsi, wakimpotosha Rais akaharibu linakuwa lake na kwakuwa sheria inamlinda basi na yeye Rais anajibanza hapo
Bahati mbaya Rais anaweza kuwa mzembe asiyetaka kushughulisha kichwa chake, akaenda kuwatumbukiza shimoni watanganyika kwasababu ya uvivu wake wa kujisomea, bahati mbaya anakuja kulindwa na sheria.
NA HILO HEBU NENDENI MKALITAZAMEEE...... ππππ
Na imeongezeka kinga ya wana TISS...
Unganisha dots