Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Haha ndo huyo nimesoma nae mkuu, alikua na jamaa yake anaitwa shaka wanafatana muda wote, japo shaka hakuingia top 10 ila alipiga one ya tatu safi kabisa.... Japhet ni shida sana.... Jamaa hajawahi kukaa kusoma yeye alikua analetewa maswali tu anasolve
Jamaa ni programmer mzuri sana.
Yuko vyedi kwenye hili soko la software development.
 
Wana- perform vizuri shuleni ila hata kikwangulio cha karoti tunaagiza China.
Nilikuwa natafuta such a comment. Huu uzi nimesoma, aibu imenijaa mimi huku msambikanyukwa. Pamoja na sifa zote humu, na struggles za shule, yet.....mambo yanayoendelea katika sekta zote haviendani na elimu yetu/ufaulu wetu.

Kwa waliosoma nchi za nje (wanavyodai) elimu ya huko sio complicated kama ya bongo. Maswali ya mitihan ni straight to the point na ishu kama hizo, na bado mambo wanayobuni ni makubwa vile vile. Sisi tunapewa machands+ma-abbort lakin ndo maisha hayaakisi yale magumu tumepitia.

Am sometimes forced to believe labda tungekuwa na mitaala yetu, labda...tungebuni vya kwetu kwa ukubwa zaidi. Baba zetu kweli elimu zenu zilikua standard lakin very complicated, na mpaka leo yapo mliyoyafanya lakin machache sana. Maana kama mpaka sasa mifumo ya sekta mbalimbali haiko sawa then faida iko wapi...sanasana uadilifu kwa baadhi yenu. Masikitiko 😞😞😞
 
Maandazi tena chief😃😃😃
Yaani Chief Mr mutuu , Maticha wa Azania walikuwa hawapo serious sana lakini baada ya kuja kupata akili nikaja kugundua wengi pale walikuwa ni Mashushu. Kuna mmoja alikuwa anajifanya CUF kindakindaki lakini enzi za Jakaya Kikwete akawa ni Mkuu wa Wilaya na unajua kabisa Ma DC ni Chama Tawala lia lia 😂😂😂😂
 
Nina washkaji zangu wakali wa mathematics mwaka huo waliondoka na C ,hata ndegeulaya alipiga C ,ule mtihani wa mwaka 2013 ulikuwa wa laana aisee , Tanzania nzima A za advance mathematics zilikuwa 12

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Huko mwaka NECTA walikua na hasira na sisi. One za masomo yote zilikua hazizidi 350 Tanzania yote aisee.
 
walkuja telecom hawa enzi hizo telecom haishikiki na bado japhe aliongoz (first class honours) ila michael shaka alkuw wakawaida sana
Michael shaka alifichwa na kivuli Cha japhe ila na yeye ni mtu mbaad sana aisee.... Kuna mtu hapa anasema tele siku izi wanachukua mpaka 1.8 ndo namwambia kipindi chetu 1.5 hunusi tele
 
Hizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma

Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti Moja ya shule tajwa hapo combination ya pcm... Kipindi hicho special school wamejaa watoto wa dar kutoka (kibaha, Azania, pugu) aisee Hawa madogo wana sifa kishenzi.... Mtu anakuja kuripoti form 5 ameshamaliza topic zote za form 5 anakaribia kumaliza za form 6

Sasa si matozi tulivyomaliza form 4 vitabu tukatupa Kule mpaka siku ya kuripoti hujawahi kupiga pindi lolote... Unakutana na vitoto vimesoma sijui mchikichini huko aisee wamefuta topic zote, aisee nilipata presha sana mpaka kuzoea ile Hali.... Nakuta madogo wanapiga integration kama hawana akili, ukikaa bwenini wanaulizana kwa nguvu reaction za organic. Chemistry huko....

Dah yaani mwezi wa kwanza form 5 watu wanasolve necta review nikasema hapa nimeyatimba... Aisee ile presha ya ku catch up nilipata shida Sana sio Siri... Ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa Moja kwa Moja

Kuna dogo tumeingia form 5 alikua anaitwa T.O (Tanzania one) alitukimbiza wote form 4 aisee huyu Jamaa mpaka Leo hua namuogopa. Hua namwambia hata hii kazi ya u engineer unayofanya unastahili kua somewhere else una potential kubwa sana, picha linaanza tumeingia form 5 hapo.... Sasa form 6 walikua wanafanya fitness tests (hii anatokea mwanafunzi mmoja au wawili wanatunga mtihani alafu wengine wanafanya japo sio lazima)

Ujinga wa hii mitihani wanafunzi wanajua kukomoana yaani maswali yote unakuta ya kibabe... Kuzungusha 0 huku ni kawaida tu ndo maana wengi walikua hawataki huu ujinga, dogo bana tunafika form 5 kaskia form 6 wanafanya fitness test ya physics dogo akazamia akapiga Pepa... Matokeo yanatoka form 6 karibu wote wamefeli dogo kawakimbiza.... Wote wanaulizana hili jina nani mbona hatumjui... Kuja kuulizia wakaja kugundua ni dogo wa form 5 aisee jamaa walimind kinoma akapigwa marufuku kabisa kusogeza pua kwenye fitness tests za form 6

Huyu dogo tulipofika form 6 sidhani kama aliwahi kukaa akasoma, jamaa alikua anakaa zake class watu wamepanga foleni na maswali Yao yaliowashinda dogo anapiga yote tu hajali kama ni ya physics, chemistry, pure au bam ye anasolve tu. Alikuja kua Tanzania one tena form 6 jamaa walimtangaza hesabu paper 1 na 2 zote alipiga 100%.

Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
Kwa mtu anayejielewa ni vizuri kwenda shule kama hizo


Hao wanafunzi ndio watakuwa walimu wake walimu wake wa kumkatia mapindi
 
Shule zote za government wanafunzi Wana viherehere nakumbuka nikiwa advance Kuna jamaa walinifukuza kwenye room kisa nalala Sanaa, eti nawatia uvivu kusoma yaani prepo ikiisha saa4, mijamaa inaunga kusoma Hadi saa6, alafu saa9 inaamka Dom Kuna viti na meza, na baridi la umbwe mijitu inajitesa tu
Haha kibosho umbwe hapo hukupata demu wa somsom au mlama kweli chief??
 
Nilikuwa na demu alikua anakaa mitaa ya kagera pale kwenye gulio,
Umbwe shule ya kibabe, Kuna mwalimu alipigwa tofali usiku kwenye ile njia juu ya dining hall kuelekea nyumba ya walimu akakaa hospital zaidi ya mwezi, headmaster kaja parade anawaambia walimu ikifika saa Moja jioni marufuku mwalimu kuingia eneo la wanafunzi huko😃😃
 
Back
Top Bottom