Kwa ufaulu huu kidato 6, 2023. Bila upanuzi vyuo vikuu ni Div one tu wataingia vyuo vikuu

Tozo

Member
Aug 23, 2021
76
154
Matokeo ya kidato cha sita 2023. Karibu shule zote daraja lenye idadi kubwa ya waliofanya vizuri ni daraja la kwanza ( Division one). Kwa matiki hiyo mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;

1. Kama vyuo vikuu vitachukua wanafunzi kulingana na uwezo wake kama miaka ya nyuma ni dhahili kuwa wanafunzi watakao ingia vyuo vikuu vyote vya umma na binafsi watakuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza tu.
2. Kama vyuo vitalazimika kuongeza idadi ya wanafunzi pasipo kwenda sambamba na kuongeza miundo mbinu yake na kuajiri wahadhiri wengine hasa ukizingatia muda haitoshi kulingana na kuanza mwaka wa masomo Oktoba ni dhahili itasababisha kushuka kwa ubora wa elimu itakayotolewa.

3. Tutarajie shule za binafsi kuanza kukosa wanafunzi. Kwani kwa matokeo ya mwaka huu ufaulu umekuwa wa kufanana kwa shule zote, zile za vipaji maalumu, shule za binafsi na hata shule za bweni kawaida na zile za kata Zipo shule za bweni kawaida hazijatoa hata wanafunzi wa daraja la tatu au la pili kabisa. Kwa sababu hiyo wazazi hawataona sababu ya kuwapeleka watoto wao shule za kulipia wakati ufaulu hautofautiani na shule za bure za umma.

Ni wakati wa serikali kujipanga sasa na kukabiliana na ongezeko la ufaulu huu mkubwa kwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Kwa mfano kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha tano kufungua shule Julai kama ilivyozoeleka na kusongeza mpaka Agosti ni ushahidi wa waziri kuwa serikali haina mipango ya muda mrefu. Huu siyo wakati wa kujenga madarasa kwani walitakiwa kuelewa mapema kuhitajika kwa madarasa.

Wataalamu wao wa Chuo cha Mipango Dodoma wanatakiwa kutumika mapema kuepusha uzembe wa aina hii.
 
Ni wakati wa serikali kujipanga sasa na kukabiliana na ongezeko la ufaulu huu mkubwa kwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Kwa mfano kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha tano kufungua shule Julai kama ilivyozoeleka na kusongeza mpaka Agosti ni ushahidi wa waziri kuwa serikali haina mipango ya muda mrefu. Huu siyo wakati wa kujenga madarasa kwani walitakiwa kuelewa mapema kuhitajika kwa madarasa. Wataalamu wao wa Chuo cha Mipango Dodoma wanatakiwa kutumika mapema kuepusha uzembe wa aina hii.
Vyuo vikuu vinatosha sana kwa sasa mpk vinahangaika kutangaza ili kupata wanafunzi.
Vyuo kwa kukosa wanafunzi sasa hv wamejaza wanafunzi wa Certificate na Diploma.
UDOM yenyewe bado inahitaji sana tu.
 
Wakati nikiwa likizo nyumbani nilitembelewa na kijana mmoja aliyemaliza Form 6 akiwa na DIV2 akiniomba nimsaidie kupata chuo Marekani ninakofanyia kazi zangu. Nikamfanyia usaili wa haraka haraka wa Calculus na Physics nikamkuta ni mweupe kabisa. Inawezekana mitihani ya siku hizi inahusu maswali basic tu au ni maswali yaliyokwisha jirudia sana kiasi kuwa wanafunzi wanakuwa wanajiandaa kwa kutumia past papers tu bila kuwa na deep understanding ya subject matter.
 
Matokeo ya kidato cha sita 2023. Karibu shule zote daraja lenye idadi kubwa ya waliofanya vizuri ni daraja la kwanza ( Division one). Kwa matiki hiyo mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;

1. Kama vyuo vikuu vitachukua wanafunzi kulingana na uwezo wake kama miaka ya nyuma ni dhahili kuwa wanafunzi watakao ingia vyuo vikuu vyote vya umma na binafsi watakuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza tu.
2. Kama vyuo vitalazimika kuongeza idadi ya wanafunzi pasipo kwenda sambamba na kuongeza miundo mbinu yake na kuajiri wahadhiri wengine hasa ukizingatia muda haitoshi kulingana na kuanza mwaka wa masomo Oktoba ni dhahili itasababisha kushuka kwa ubora wa elimu itakayotolewa.

3. Tutarajie shule za binafsi kuanza kukosa wanafunzi. Kwani kwa matokeo ya mwaka huu ufaulu umekuwa wa kufanana kwa shule zote, zile za vipaji maalumu, shule za binafsi na hata shule za bweni kawaida na zile za kata Zipo shule za bweni kawaida hazijatoa hata wanafunzi wa daraja la tatu au la pili kabisa. Kwa sababu hiyo wazazi hawataona sababu ya kuwapeleka watoto wao shule za kulipia wakati ufaulu hautofautiani na shule za bure za umma.

Ni wakati wa serikali kujipanga sasa na kukabiliana na ongezeko la ufaulu huu mkubwa kwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Kwa mfano kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha tano kufungua shule Julai kama ilivyozoeleka na kusongeza mpaka Agosti ni ushahidi wa waziri kuwa serikali haina mipango ya muda mrefu. Huu siyo wakati wa kujenga madarasa kwani walitakiwa kuelewa mapema kuhitajika kwa madarasa.

Wataalamu wao wa Chuo cha Mipango Dodoma wanatakiwa kutumika mapema kuepusha uzembe wa aina hii.
Labda Kwa Arts lakini Kwa Science huwezi kuwaacha division II maana Kwa matokeo hayo ndo wachache kuliko div.1 na div.3.
 
Kuna siasa zimeingia sana kwenye elimu. Nimeshangaa hakuna penalty ya Basic Maths kwa O-level. Huko form four watoto wanapiga One kama uchafu kumbe siri ni kuondoa penalty ya Maths. Sina uhakika ila nahisi form six pia kuna siasa za kupanua goli. Ni kweli watoto wana akili sana sasa hivi na wazazi wengi wameshtuka na kutaka watoto wasome...
 
Back
Top Bottom