Kidato cha 6 waruhusiwe kufundisha somo la Hisabati

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Nchi yetu imekuwa na nia njema sana ya kuendeleza Vijana katika fani mbalimbali hasa za ufundi na ujasiriamali.

Kimsingi vijana wenye uelewa wa somo la hesabu wanaweza kufanya vizuri sana katika fani hizo za ufundi na ujasiriamali.

Hata hivyo kutokana na upungufu/ ukosefu wa waalimu wa hesabu katika Shule za msingi na upungufu mkubwa katika shule za Sekondari, wanafunzi wengi wanaotarajiwa kujiunga na fani hizo humaliza wakiwa wamepata alama sifuri.

Napendekeza Vijana wa Kidato cha sita wenye Ufaulu wa C na kuendelea katika somo la Hesabu waruhusiwe kufundisha somo la Hesabu shule za Sekondari na Vijana wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa C katika somo la hesabu na kuendelea waruhusiwe kufundisha shule za msingi.

Hii itasaidia kupunguza pengo wakati tunajipanga.
 
Nchi yetu imekuwa na nia njema sana ya kuendeleza Vijana katika fani mbalimbali hasa za ufundi na ujasiriamali. Kimsingi vijana wenye uelewa wa somo la hesabu wanaweza kufanya vizuri sana katika fani hizo za ufundi na ujasiriamali
Hata hivyo kutokana na upungufu/ukosefu wa waalimu wa hesabu katika Shule za msingi na upungufu mkubwa katika shule za Sekondari, wanafunzi wengi wanaotarajiwa kujiunga na fani hizo humaliza wakiwa wamepata alama sifuri
Napendekeza: Vijana wa Kidato cha sita wenye Ufaulu wa C na kuendelea katika somo la Hesabu waruhusiwe kufundisha somo la Hesabu shule za Sekondari na Vijana wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa C katika somo la hesabu na kuendelea waruhusiwe kufundisha shule za msingi
Hii itasaidia kupunguza pengo wakati tunajipanga
Kufika kidato cha sita ndio sifa ya kufundisha?

Hata uwe na degree bado siyo sifa ya kufundisha.
 
Vijana wa Kidato cha sita wenye Ufaulu wa C na kuendelea katika somo la Hesabu waruhusiwe kufundisha somo la Hesabu shule za Sekondari na Vijana wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa C katika somo la hesabu na kuendelea waruhusiwe kufundisha shule za msingi

Unajua daraja C kwa A-Level ni marks ngapi kwa namba?
 
H
Kufika kidato cha sita ndio sifa ya kufundisha?

Hata uwe na degree bado siyo sifa ya kufundisha.

Kimsingi vinategemeana; hata ukiwa na Degree ya Ualimu kama huna ufaulu wa somo la Hesabu, huwezi kufundisha hesabu hata shule ya msingi
Hivyo umahiri wa somo husika unabeba kama 75% na hiyo 25 ndio mbinu za kufundisha
Chuoni unafundisshwa tu mbinu za kufundisha saikologia....sasa kama somo husika hulijui utafundisha nini?
 
hilo nalo ni swali? nimepita huko tena kipindi kile ambacho PCB/M ilikuwa tishio; sio sasa hivi....

Weka hizo namba sasa, sio kujifaragua kuwa umepita sijui kipindi gani...

Kwani nani hakupita huko?
 
Halafu walimu wa hesabu wakaajiriwe wapi ??

If you try to think try think critical.

Then, heshimu uwalimu kama trauma si kila mtu aingilie tu kazi ya uwalimu.
 
Nchi yetu imekuwa na nia njema sana ya kuendeleza Vijana katika fani mbalimbali hasa za ufundi na ujasiriamali. Kimsingi vijana wenye uelewa wa somo la hesabu wanaweza kufanya vizuri sana katika fani hizo za ufundi na ujasiriamali
Hata hivyo kutokana na upungufu/ukosefu wa waalimu wa hesabu katika Shule za msingi na upungufu mkubwa katika shule za Sekondari, wanafunzi wengi wanaotarajiwa kujiunga na fani hizo humaliza wakiwa wamepata alama sifuri
Napendekeza: Vijana wa Kidato cha sita wenye Ufaulu wa C na kuendelea katika somo la Hesabu waruhusiwe kufundisha somo la Hesabu shule za Sekondari na Vijana wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa C katika somo la hesabu na kuendelea waruhusiwe kufundisha shule za msingi
Hii itasaidia kupunguza pengo wakati tunajipanga
Unadhani walimu wa hesabu hawapo mtaani?

Walimu wapo wengi tu ila kuajiri ndio hawataki

Hovyo ni bora ushauri serikali iajiri walimu
Hovyo
 
Nini kiliifanya serikali ya ccm ,kufuta kozi ya ualimu pale Mkwawa CNE ambacho kilikua kinatupa super teachers wa grade 111A kwa shule za msingi kwa masomo ya hesabu na sciences?,hiki chuo pia kilitupatia super teachers wa masomo ya Hesabu na sciences kwa waalimu wa secondary schools?,kulikua na combinations za PC,PG,PM,CM,CB na hawa ni zaidi ya waalimu 100 kwa kila mwaka, tuangalie tulipojikwaa sio kuangukia,pia why walifuta FTCs?,jibu langu binafsi ni kuendeleza ujinga wa watanzania ili royal families ziendelee kula pie ya taifa,President JMP ni tunda la CM &Education pale Mkwawa CNE
 
Unaona ambavyo mtu aliyepata karai anachezea mbali...

Sasa mtu ako na grade la wastani, unataka akamfundishe mtu mwingine ili akapate daraja la juu...
Mtu aliyefauli Hesabu kidato cha sita hata kwa D, anaweza kufundisha hesabu ya kidato cha nne mtu apate A
Unajua pure mathematics wewe
 
Nini kiliifanya serikali ya ccm ,kufuta kozi ya ualimu pale Mkwawa CNE ambacho kilikua kinatupa super teachers wa grade 111A kwa shule za msingi kwa masomo ya hesabu na sciences?,hiki chuo pia kilitupatia super teachers wa masomo ya Hesabu na sciences kwa waalimu wa secondary schools?,kulikua na combinations za PC,PG,PM,CM,CB na hawa ni zaidi ya waalimu 100 kwa kila mwaka, tuangalie tulipojikwaa sio kuangukia,pia why walifuta FTCs?,jibu langu binafsi ni kuendeleza ujinga wa watanzania ili royal families ziendelee kula pie ya taifa,President JMP ni tunda la CM &Education pale Mkwawa CNE
CNE=College of National Deduction 🤣🤣🤣🤣🪑💺
 
Unadhani walimu wa hesabu hawapo mtaani?

Walimu wapo wengi tu ila kuajiri ndio hawataki

Hovyo ni bora ushauri serikali iajiri walimu
Hovyo

Nathamini sana waalimu
Hata hivyo, tuendelee kuwa na kizazi chenye sifuri za hesabu hadi Serikali itakapopata uwezo wa kuajiri?
Hii ni sawa na kuacha watoto wakae chini madarasani tukisubiri Serikali ije kutengeneza madawati ambapo ni kweli itatengeneza lakini lini?
.
 
Mtu aliyefauli kidato cha sita hata kwa D, anaweza kufundisha hesabu ya kidato cha nne mtu apate A
Unajua pure mathematics wewe au unafikiri....zile hadithi za Vasco Dagama
Nimecheka wallah. Daaah.
 
Hadi Sasa Wengi Wanaofundisha Huko Ni Wamepata Chini Ya Grade Hilo.

Mathematics Wote Wanaopata Kuanzia Daraja La C Almost 80% Huwa Wanaenda Course Za Engineering ( Uhandisi).

Sasa Wewe Unavyosema Wapewe Nafasi Ya Kufundisha Sijui Utawapata Wapi Hao?

C Grade Kwa Advance Kama Sijakosea Kwa Sasa Ni 60 - 69% Sasa Hapo Si Pakitoto.

Paper One Ndio Inaangusha Wengi Ila Paper Two Huwa Ni Nyeupe Japo Yote Inahitaji Utashi Na Kujituma & Speed.
 
Mtu aliyefauli kidato cha sita hata kwa D, anaweza kufundisha hesabu ya kidato cha nne mtu apate A
Unajua pure mathematics wewe au unafikiri....zile hadithi za Vasco Dagama

Ninaifahamu tena advanced maths (paper I&II NECTA) na nimesoma kwenye hizo shule serikali inaita za vipaji maalumu scored A in both CSE na ACSEE, huwa sipendi kubrag JF kuficha identity na nimekuandikia uelewe...

So next time usilete habari za kusoma sijui Pure maths, Additional maths uone ndio dunia ya hesabu umeimaliza...
 
Hongera sana Kiongozi
japo watu waliosoma hesabu hawajinasibu hivyo. Lakini pia kwa mtu aliyesoma Hesabu anauwezo wa kutafsiri kirahisi tu kuwa; aliyepata C ya hesabu kidato cha nne; anauwezo wa kufundisha hesabu ya primary vizuri kwa asilimia 99%
 
Hongera sana Kiongozi
japo sidhani kama ulisoma Combination ya Hesabu, kwani kwa mtu aliyesoma Hesabu anauwezo wa kutafsiri kirahisi tu kuwa; aliyepata C ya hesabu kidato cha nne; anauwezo wa kufundisha hesabu ya primary vizuri kwa asilimia 99%

Okay tufanye sijasoma, tukubali kutokukubaliana...
 
Ninaifahamu tena advanced maths (paper I&II NECTA) na nimesoma kwenye hizo shule serikali inaita za vipaji maalumu scored A in both CSE na ACSEE, huwa sipendi kubrag JF kuficha identity na nimekuandikia uelewe...

So next time usilete habari za kusoma sijui Pure maths, Additional maths uone ndio dunia ya hesabu umeimaliza...
HKL acha maneno!
 
Back
Top Bottom