Kwa tuliopata ziro(0) form four hebu tukutane hapa

Huu uzi unaletewa mzaha lakini ungekuws serious unaweza kusaidia watu.

Wengi wanapata 0 form IV au VI halafu wanachizi kabisa, wengine mpaka wanakunywa sumu. Kwa waliowahi kupata 0, share experience.

Mimi nitashare ya mwalimu wangu chuo

Alipiga 3 akiwa form 4, form Six akapiga 0. Anakwambia home kulikuwa kubaya kuliko maelezo. Bahati nzuri kuna ndugu yake alikuwa chuo, akamwambia njoo ufanye certificate ya IT. Na jamaa alikuwa interest na computers. Akatoboa vizuri certificate, akaenda Diploma akapiga vizuri. Akaanza Degree ya Computer Science, jamaa aliongoza course nzima. Chuo kikampeleka Finland kufanya masters na ajira akapata. Leo ni Networking guru, PHD, na mwalimu mzuri sana.
 
Nilifeli masomo yote ya science form 4 lakini nashukuru Mungu kwenye arts nilibutua nikiwa na A ya Kiswahili na C kwenye masomo mengine na kuambulia div 3 .. nikaenda A level napo nashukuru Mungu matokeo hayakuwa mabaya ..

All in all mliopass sciences salute kwenu! ..
 
kupata div. zero iwe form four /six ni uzembe wa hali ya juu……………………….
 
Nilifeli masomo yote ya science form 4 lakini nashukuru Mungu kwenye arts nilibutua nikiwa na A ya Kiswahili na C kwenye masomo mengine na kuambulia div 3 .. nikaenda A level napo nashukuru Mungu matokeo hayakuwa mabaya ..

All in all mliopass sciences salute kwenu! ..
Inaonekana shida kwako ilikua kingereza , masomo ya sayansi yangekuwa yanafundishwa kwa kiswahili ungebutua vizuri kabisa
 
Hapana mkuu, nazungumza kingereza bila tabu yoyote ila tatizo nilikuwa stubborn sana sana Yani sikuwa serious kabisa na masomo ndo maana ikapelekea kufeli sciences..

Alafu sciences haziitaji kingereza kingi ni arts ndo inataka kingereza sana sababu ya kuandika kwingi ..
 
Bila kingereza utaelewaje swali mbona kiswahili umefaulu kwa A. Watu wengi wanafeli kwasababu kingereza kinazingua
 
Yaani unapata zero na unatapa, unajitokeza kabisa bila aibu mbele za watu unatangaza hilo.

Kweli dunia imeisha!
 
Bila kingereza utaelewaje swali mbona kiswahili umefaulu kwa A. Watu wengi wanafeli kwasababu kingereza kinazingua
Bro acha ubishi, mi nimesomea Uganda ambapo hata Kiswahili hawakijui na hicho kingereza nimebutua vile vile ..
 
Mbona kiswahili kinafundishwa kwa lugha ya kiswahili na bado watu wanafeli.
Sayansi sio lelemama
Kiswahili kimefanywa kuwa kigumu . Sayansi ikifundishwa kwa kiswahili ni rahisi zaidi ikumbukwe sayansi ni nature no imagination ila kiswahili mfano fasihi ni mambo ya dhahania zaidi na watu kiswahili wanafeli kwenye fasihi sio sarufi. Fasihi kwakweli ni ngumu sana na baraza la mitihani wameivuruga kabisa
 
Kiswahili kigumu maana hata hatuongei lugha fasaha.
Fikiria glass, box, peni, stapler ni maneno ya kingereza tunatumia kama kiswahil
 
Back
Top Bottom