Wangapi tunajutia Kuyakwepa Masomo tuliyoyadharau O na A levels ambapo kama tungeyasoma leo tusingekuwa tunapigika hivi Kimaisha?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,709
109,142
Yaani GENTAMYCINE nisingekuwa namkwepa Mwalimu wa Somo la Useremala ( Wood Work ) Shuleni nilipokuwa Form One hadi Form Four ( tena akinibembeleza kama Mwanafunzi ) leo hii ningekuwa bonge la Fundi Samani Keko na Tajiri mno tu.

Sasa Kumi ni pale aliyekuwa Kocha wangu wa Mpira ( sasa Marehemu ) baada ya Kuvutiwa na Kipaji changu Kikubwa cha Kucheza Soka mwaka 1999 alitaka Kuniunganisha na Timu ya Vijana ya Sports Club Villa ya Uganda kisha nikipikwa pale niuzwe Ulaya ( Uingereza ) ila Wivu wa kuwa mbali na Demu wangu wa Kiganda nikaikataa hiyo Fursa na baadae hata Demu Mwenyewe nae tukamwagana, Kipaji changu Tukuka cha Mpira kikapotea na sasa nipo tu na Msoto huku nikijutia.

Watanzania kabla ya Kumuimba Mbwana Samatta wenu kwa Kipaji cha Kucheza Mpira nilichokuwa nacho nina uhakika Wote mngekuwa mkiniimba tu GENTAMYCINE huku nikiwa nachezea Chama langu tukuka la Liverpool FC.

RAI yangu kwa Wadogo zangu tafadhalini Maisha ya sasa ni Magumu, zingatieni Masomo, kuweni na Nidhamu za Kitaaluma, Msilibague Somo lolote lile Shuleni kwani huenda hilo Unalolidharau ndiyo litakuja Kukukomboa katika Nyakati kama hizi Soko la Ajira ni Gumu ila kwa waliosomea Masomo ya Ufundi Stadi Wao wanapeta tu kwakuwa Fani zao ni muhimu, zinalipa na zina Soko 24/7 kutokana na kuongezeka kwa ubunifu mkubwa duniani na katika Jamii yetu.

Na wale wenye Vipaji mbalimbali ( hasa vya Michezo ) tafadhalini Viendelezeni ili vije kuwafaeni Kimaisha huku mbeleni na Ukubwani.

Mwisho Wazazi acheni Ushamba ( Upang'ang'a ) wa kulazimisha Watoto wenu Wasome yale Masomo mliyosoma nyie na wakitaa mnawatishia Kuwalaani kwani kwa 55% hadi 60% nanyi pia ni sehemu ya Tatizo katika Kuongeza Ugumu na Idadi ya Soko la Ajira nchini na kuzidi kuongeza Umasikini kwa Watanzania na kuirudisha nyuma Kimaendeleo na Kiuchumi Tanzania yetu.

Zanaki, Yao na Genius nimemaliza!!!
 
Sijutii nilikua nakwepa somo la Home management and food nutrition

Mwalimu alikua anatufundisha majukumu ya wamama
Ila niamini Mkuu ungelipenda nina uhakika ungeondoka na Kitu ambacho kingekuja Kukusaidia mahala fulani hata kama hivi sasa umefanikiwa Kimaisha kwa Kusoma Fani nyingine / Somo jingine.
 
Yaani GENTAMYCINE nisingekuwa namkwepa Mwalimu wa Somo la Useremala ( Wood Work ) Shuleni nilipokuwa Form One hadi Form Four ( tena akinibembeleza kama Mwanafunzi ) leo hii ningekuwa bonge la Fundi Samani Keko na Tajiri mno tu.

Sasa Kumi ni pale aliyekuwa Kocha wangu wa Mpira ( sasa Marehemu ) baada ya Kuvutiwa na Kipaji changu Kikubwa cha Kucheza Soka mwaka 1999 alitaka Kuniunganisha na Timu ya Vijana ya Sports Club Villa ya Uganda kisha nikipikwa pale niuzwe Ulaya ( Uingereza ) ila Wivu wa kuwa mbali na Demu wangu wa Kiganda nikaikataa hiyo Fursa na baadae hata Demu Mwenyewe nae tukamwagana, Kipaji changu Tukuka cha Mpira kikapotea na sasa nipo tu na Msoto huku nikijutia.

Watanzania kabla ya Kumuimba Mbwana Samatta wenu kwa Kipaji cha Kucheza Mpira nilichokuwa nacho nina uhakika Wote mngekuwa mkiniimba tu GENTAMYCINE huku nikiwa nachezea Chama langu tukuka la Liverpool FC.

RAI yangu kwa Wadogo zangu tafadhalini Maisha ya sasa ni Magumu, zingatieni Masomo, kuweni na Nidhamu za Kitaaluma, Msilibague Somo lolote lile Shuleni kwani huenda hilo Unalolidharau ndiyo litakuja Kukukomboa katika Nyakati kama hizi Soko la Ajira ni Gumu ila kwa waliosomea Masomo ya Ufundi Stadi Wao wanapeta tu kwakuwa Fani zao ni muhimu, zinalipa na zina Soko 24/7 kutokana na kuongezeka kwa ubunifu mkubwa duniani na katika Jamii yetu.

Na wale wenye Vipaji mbalimbali ( hasa vya Michezo ) tafadhalini Viendelezeni ili vije kuwafaeni Kimaisha huku mbeleni na Ukubwani.

Mwisho Wazazi acheni Ushamba ( Upang'ang'a ) wa kulazimisha Watoto wenu Wasome yale Masomo mliyosoma nyie na wakitaa mnawatishia Kuwalaani kwani kwa 55% hadi 60% nanyi pia ni sehemu ya Tatizo katika Kuongeza Ugumu na Idadi ya Soko la Ajira nchini na kuzidi kuongeza Umasikini kwa Watanzania na kuirudisha nyuma Kimaendeleo na Kiuchumi Tanzania yetu.

Zanaki, Yao na Genius nimemaliza!!!
"Waliopata sifuri kwenye mitihani ya Taifa wafuatiliwe yawezekana wakawa ni msaada mkubwa Kwa jamii zao na Taifa""
 
Back
Top Bottom