Kwa spidi hii Rwanda watatuacha

BTW Rwanda ina eneo la ukubwa wa kiasi gani?

Je Eneo hilo tunaweza kulilinganisha na Tanzania kwa mara ngapi?

Je Rwanda ina population ya watu wangapi?

GDP ya Rwanda ni kiasi gani?

Je kiwango cha kufuta ujinga kipo cha kiasi gani?

Je, kwa wastani, daktari mmoja anahudumia wagonjwa wangapi?

Je, mifumo yao ya usawa kwa mlinganisho wanakilometa ngapi za lami zaidi ya Tanzania?

Je, Rwanda inategemea nini hasa katika uchumi wa nchi yake?

Je, balance of trade ta Rwanda iko vipi?

Je, uchumi wa Rwanda unakuwa kwa kiasi gani kwa mwaka na ukuwaji wake kwa miaka mitano iliyopita?

Ninataka kuchangia lakini ninahitahaji data na ikibidi nifanye utafiti.
 
The area of Rwanda is 26,338 sq km

The population is 10,186,063 as of July 2008 estimates

GDP per capita is $800

The literacy level is Male 76.3 and female 64.7

Economy is mainly agriculture and the main export goods are coffee, tea, hides, tin ore

The main industries are cement, agricultural products, small-scale beverages, soap, furniture, shoes, plastic goods, textiles, cigarettes

it grows at a rate of 5.8% (2006)

Sources: Rwanda Facts, [ame=http://en.wikipedia.org/wiki/Economy_of_Rwanda]Economy of Rwanda - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]

Kwenye hizo sources kuna extra information and data but nimeamua kukuandikia ulizo ulizia kwa kadri nilivyo zipata.
 
Ukiangalia data: Rwanda are not any better..Tz tumewazidi!

Ukiangalia Global Peace Index (GPI)..Tz we are 59 Rwanda 118!!
 
Tanzania
Idadi ya watu 41,048,532
Eneo 945,087 sq km
Ongezeko la watu 2.04%

GDP per capita$1,300
GDP ppp $54.26 billion

Literacy
male: 77.5%
female: 62.2%

Watumiaji wa internet 400,000

Rwanda
Idadi ya watu 10,473,282
Eneo 26,338 sq km
Ongezeko la watu 2.782%

GDP per capita $900
GDP ppp $9.061 billion

Literacy
male: 76.3%
female: 64.7%

Watumiaji wa Internet 100,000
 
Kitu kikubwa cha kujifunza kutoka Rwanda ni usafi. Mji wao wa Kgali na viunga vyake ni visafi sana, ukilinganisha na Dar na miji mingine Tanzania. Sisi ni wachafu sana sanaa.... We need to learn from them in that aspect..... Accept that please...

Kuna vitu vizuri pia vya kujifunza toka kwa Kagame....... He is a hard working man...
 
shiumiti,
Kigali yawezekana ni safi! Pia tz tafadhali usigeneralize- kuna miji misafi tu sana kama Moshi, Iringa, n.k! Rwanda ni kanchi kadogo kama Mkoa wa Kagera and Kigoma commbined!

Sii kweli kuwa Watz wote tu wachafu!
 
Nadhani ni vyema tukawa na wivu wa maendeleo. Wivu huu asili yake ni kujifunza kwenye yale mazuri wanayoyafanya watu wa nchi nyingine na si kutumia udhaifu wao kuhukumu hata yale mazuri wanayoyafanya. Muono huo hauwasaidii hao wa nchi nyingine wala hautusaidii sisi. Nakiri kuwa Rwanda leo iko katika mstari. Ukitua Kigali ukatembea mjini pale unaona matumaini hata kwenye nyuso za watu, tofauti na hapa ambapo unakuta watu wanaonyesha kutoridhika na kila kitu. Inawezekana Rwanda isifikie huko inapotaka kwenda kwa sababu anuani lakini tukiri tu kwa sasa wako katika mstari, na kuwa wakiendeleza juhudi zao watafika mbali. Yako mengi ya kujifunza kutoka kwao. Kubwa kabisa ni NIDHAMU iliyoko baina ya mtu na mtu, mtu na taasisi, chombo cha dola na raia na Rais na wananchi wake. Hili sisi tumelipoteza................. Ni vyema kuipima au kuihukumu Rwanda kwa juhudi ilizozifanya katika miaka ya karibuni tokea mauaji ya kutisha ya kimbari ya mwaka 1994. Rwanda ingeweza kuishia kuwa 'failed state'. lililo dhahiri ni kuwa wameweza kuigeuza hali hiyo na kuelekea kuwa nchi yenye tumaini jipya. Na hilo ndilo la kujifunza pamoja na hayo yaliyoainishwa na mwenzetu hapo juu.
 
Kitu kikubwa cha kujifunza kutoka Rwanda ni usafi. Mji wao wa Kgali na viunga vyake ni visafi sana, ukilinganisha na Dar na miji mingine Tanzania. Sisi ni wachafu sana sanaa.... We need to learn from them in that aspect..... Accept that please...

Kuna vitu vizuri pia vya kujifunza toka kwa Kagame....... He is a hard working man...

Rwanda kila jumamosi ya mwisho mwa mwenzi husimamisha kazi nchi nzima na kuanza kusafisha nchi yako kwa masaa sita....na kuna kuwa na attendece record ambayo inafatiliwa na mahudhulio yako kila sehemu..

Kama huto udhuria kwenye usafi huo kwa mara mbili bila sababu za msingi..basi wanakufungua hata hudumu za jamii..kama hispitali na maji...ikibidi tunakuchapa viboko...

U can see why nchi ni safi au mji wa kigali ni msafi....vinginevyo ungekuwa ni wa kawaida tu kama morogoro.
 
shiumiti,
Kigali yawezekana ni safi! Pia tz tafadhali usigeneralize- kuna miji misafi tu sana kama Moshi, Iringa, n.k! Rwanda ni kanchi kadogo kama Mkoa wa Kagera and Kigoma commbined!

Sii kweli kuwa Watz wote tu wachafu!

Mzalendohalisi,

Sijawahi kufika Kigali ila kusema Dar, Iringa na Moshi ni miji safi sikubaliani na wewe. Hiyo miji haina usafi wowote. Labda enzi zile za Mrema ilikuwa nafuu.

Hao viongozi wetu wanazunguka dunia nzima na kuona miji ya wenzetu ilivyo safi, lakini wakifika nyumbani wanaruka takataka barabarani.
 
Ukiangalia data: Rwanda are not any better..Tz tumewazidi!

Ukiangalia Global Peace Index (GPI)..Tz we are 59 Rwanda 118!!

For how long will you still be better than Rwanda? .
Thats the question.
And please bear in mind that about 45 years ago Malaysia(called Malay then),Singapore, Indonesia and even to some extent India were in the same position as we are now.
They have developed by huge leaps, while we are still stagnant.
That is the issue here.
Rwanda watatupita hivi hivi na sisi tunaona, misingi ya maendeleo yao tunaiona lakini tunabishania statistics
 
sasa hapo kuna nini cha kujifunza ktka kwa huyo kagame na ujumbe wake ndugu muheshimiwa??

KIJAKAZI umenisikitisha kwamba hujaona cha ajabu. Recall mikataba yetu ya rasilimali kama madini , utalii n.k. Nafikiri tafakari kwanza kabla ya kuandika
 
Hawa jamaa wako serious, ukimwangalia kagame akiongea unaamini kwamba anamaanisha anachoongea, ukimwangalia JK akiongea unaona kabisa kwamba huyu ni msanii! Hivi karibuni nikiangalia CNN nilimwona kagame akiwashangaa viongozi wenzake wa kiafrika wanaosema kwamba afrika haikuwa msababishaji wa mdororo wa uchumi, alisema kwamba kitendo cha kutokuwa msababishaji maana yake ni kwamba wewe sio mchezaji. Kwa mtazamo huo unaweza ukaona tofauti ya huyu jamaa alivyo visionary kuliko huyu wa kwetu ambaye badala ya kuomba ujuzi anaishia kuomba net za mbu na vijisenti. HEKOKAGAME
 
Baada ya miaka kumi kuanzia sasa Rwanda itakuwa si ulimwengu wa tatu. Mimi nimekwenda na kuona mwenyewe. Hawaba naneno ya kisisasa- wanachapa kazi na wana vision. Tanzania tutabaki nyuma kwa ushabiki wa kisiasa na kufikiri kushinda uchanguzi ni lazima kununua kura na shahada! Tutabaki nyuma!
 
For how long will you still be better than Rwanda? .
Thats the question.
And please bear in mind that about 45 years ago Malaysia(called Malay then),Singapore, Indonesia and even to some extent India were in the same position as we are now.
They have developed by huge leaps, while we are still stagnant.
That is the issue here.
Rwanda watatupita hivi hivi na sisi tunaona, misingi ya maendeleo yao tunaiona lakini tunabishania statistics

Mkuu tupo pamoja nashangaa watu wanahangaika na statistics while ignoring the hard painful truth on the ground...serikali yetu inadhani investors wataikomboa Tanzania..wakati rwanda wanajua mrwanda mwenyewe ndo atajikomboa...from the facts coming out right now kwenye governance wametuacha vibaya sana na soon hao investors tunaowataka waitaishia kwenda rwanda.
 
Hawa jamaa wako serious, ukimwangalia kagame akiongea unaamini kwamba anamaanisha anachoongea, ukimwangalia JK akiongea unaona kabisa kwamba huyu ni msanii! Hivi karibuni nikiangalia CNN nilimwona kagame akiwashangaa viongozi wenzake wa kiafrika wanaosema kwamba afrika haikuwa msababishaji wa mdororo wa uchumi, alisema kwamba kitendo cha kutokuwa msababishaji maana yake ni kwamba wewe sio mchezaji. Kwa mtazamo huo unaweza ukaona tofauti ya huyu jamaa alivyo visionary kuliko huyu wa kwetu ambaye badala ya kuomba ujuzi anaishia kuomba net za mbu na vijisenti. HEKOKAGAME

Mkuu tupo pamoja..kwenye world economic forum kagame alisema haya, it was like he was dissing kikwete LIVE! kwasababu a few weeks ago interview ya kikwete ameng'ang'ania africa is not the cause of the crisis..kagame hadi akachekesha watu kwa kusEma we should be argueing why africa is not part of the problem of the crisis..watasema ni dicteta lakini vision yake inatisha ukicompare na mugabe marehemu bongo...hata huyu raisi wetu!

Kama mdau mmoja alivyosema 'TANZANIA TUSIONE AIBU KUONA WIVU WA MAENDELEO, PERSONALLY NAONEA RWANDA WIVU AS WE SPEAK'
 
Mambo ya kujifunza ni haya:

[Source: Game theory

3. Rwanda ili kuondokana na ukabila ingependa kutoa uraia kwa watu wa mataifa mengi zaidi hivyo Rais kawaalika wengi wajitokeze hata kuomba uraia, ''watu wanaona hili ni tatizo mimi naona ni faida kwa nchi mradi wanaopewa uraia wanafuata sheria''

Taratibu mkuu, yawezekana lisiwe la kujifunza, yawezekana ikawa ni trick!!

Nchi yao ni ndogo sana na kwa ujinga wa watu wetu wa nchi masikini kama tulivyo sisi Tz, wameendelea kuzaliana pasipo kuzingatia udogo wa nchi yao na ukuaji uchumi. Hivyo pale tayari kuna msongamano, ni wachache watakaokuwa na utashi wa kuomba uraia na watakaofanya hivyo lengo litakuwa ni la muda(biashara) tu.

Shinikizo kwa TZ kutoa uraia kwa utashi wao linaweza likawa na malengo tofauti na wale wanaokaribishwa kuomba uraia kwa Mh Kagame.

Ni mapema mno kujifunza kitu kwenye ajenda ya uraia.

Ni maoni yangu
 
tatizo kubwa la watanzania ni jinsi/ au criteria tunazotumia kuwachagua viongozi wetu kwa kuangalia sura dini na mengine ya kipuuzi kwa hili tutabaki tukiwafagillia wenzetu kila siku
 
Nimewai kuona documentary moja inaonyesha jinsi rwanda inavyowafungia umeme wa solar wananchi vijijini. Tena wamepeleka wamama wajane (wa vita) nje ya nchi kuwa trained kufunga umeme huo bure vijijini. Jamaa wako mbali sana na watakuwa kama sychells soon. Wana uzalendo wa hali ya juu. Kwa Tz maendeleo ni ndoto kwani hamna nchi duniani iliyoendelea bila kuwa na uongozi competent.

Mfano ukiwauliza wa malaysia siri ya maendeleo yao watakwambia ni Dr. Mahtir, Ukiwauliza Japani watakwambia Tanaka (if am correct) Ukiwauliza South Korea they also have their champion kama nakumbuka vizuri it was a military family. Hata tuwe na wasomi na rasilimali kiasi gani, tutaendelea kuporwa until we find a president kama Kagame. Maana mmejionea wenyewe jinsi rais alivyo na madaraka yote pale Pinda alipokuwa anajikanyaga juzi.

I believe Rwanda hawana tatizo la umeme kama Tanzania
 
Kama sijakosea kwenye Internet browsing wako: RWANDA=30%,UG+KE=20% & TZ=7%!
 
Back
Top Bottom