Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799
Naam baada ya baadhi ya watu humu kuacha vivywa wazi kwenye ile thread ya Viwanda vya Sudan sasa someni VISHINDO vya wanyaRWANDA hii nimeiata toka kwa mwenzetu YAKUBU ambaye alikwepo na mhishimiwa KAGAME alipokwenda London
Msafara mzito wa Rais Paul Kagame na viongozi wa serikali ya Rwanda leo hii umefanya mkutano mkubwa hapa London na wawekezaji/wanaotaka kuwekeza Rwanda ambapo serikali imeainisha maeneo makuu yanayoweza kuvutia wawekezaji. Ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika hapa UK na kwangu kuwa ni mara ya kwanza kumuona Rais Paul Kagame ''in action'' kuna mambo kadhaa yamenivutia:
1. Ukweli kwamba alikataa kuwa mzungumzaji mkuu katika mkutano huo kwa vile alitaka kusikiliza zaidi hasa fursa ya maswali na maoni kujua nini hasa wawekezaji wanataka na vipi Rwanda inaweza kusaidia. Alipotakiwa kusalimia alitaja mambo mawili ya msingi:
- Alisema Rwanda inakerwa na hali ya utegemezi na wanajitahidi kuondokana nao, mwaka 1994 walikuwa wakitegemea misaada toka nje kwa 99% hivi sasa 49%
- Alitoa hadithi ya wawekezaji waliotaka kununua kahawa kwa centi 90 za dola wakiahidi kujenga shule,hospitali nk akawaambia huo utakuwa bado ni utegemezi bado ''tulipeni dola mbili kwa kilo na tutajenga hospitali na shule wenyewe''!
2. Ukweli kwamba wafanyakazi wengi wa ngazi za juu wa Rwanda ni vijana wadogo tu, alikuwepo Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji, Naibu Gavana wa Benki Kuu wote wakiwa ni vijana wenye uchungu na maendeleo.
3. Rwanda ili kuondokana na ukabila ingependa kutoa uraia kwa watu wa mataifa mengi zaidi hivyo Rais kawaalika wengi wajitokeze hata kuomba uraia, ''watu wanaona hili ni tatizo mimi naona ni faida kwa nchi mradi wanaopewa uraia wanafuata sheria''
4. Rwanda imejipanga vizuri kutumia vyema Bandari yetu kwa kuuza kwa nguvu zote na kwa msisitizo mkubwa kuwa Reli ya kutoka Isaka-Kigali itawanufaisha wao zaidi kwa vile nchi yao haina bandari. Reli hiyo itagharimu Dola bilioni mbili lakini ina faida kubwa kwa Rwanda na wataigharimia hata kwa mikopo.
5. Ifikapo mwaka 2010 Rwanda itakuwa imeunganishwa na wireless internet nchi nzima!
Katika hali ya kawaida baadhi ya mambo ningeona kwenye mikutano mingine kama ni matamko ya kisiasa tu lakini pale palikuwa na mikakati ya uhakika...Kwa jinsi mambo yalivyokuwa yakienda katika mkutano huo, wazo la kuendesha serikali kama kampuni katika baadhi ya maeneo ilikuwa na maana kubwa!Mengi katika haya nadhani Tanzania tungeweza kujifunza...
SOURCE:
http://www.saidiyakubu.blogspot.com/