Mkuu, pamoja na ushabiki wa kivyama, ni ukweli usiopingika kuwa, CCM kama chama tawala kimekuwa mstari wa mbele kupinga wagombea binafsi. Rejea kesi ya Mch. Mtikila dhidi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ya TZ, na hukumu yake na nini kilifuatia kuhusu utekelezaji wa hukumu hiyo? Ndiyo maana huyu bwana pamoja na mambo mengine ya rasimu ya katiba amekuja na mada hiyo ambayo kwake ameona ni ya muhimu. Sasa iwapo kwako si ya muhimu basi achana nayo, siyo lazima kuchangia kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa.
kama kweli ni mzima huumwi wakati unaandika unafikiri hii ni hoja ya kubadili sura ya siasa kwa ujumla tuombe mungu atupe uzima bado mda kidogo tu mtakuja mkimbiane watu hawaongei mambo yaliyopita wanatafakari maisha mapya wewe mkuu vipi kwa mwendo wa mawazo haya utataabika siku ikifika.