EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,347
TV zote kubwa nchini, pamoja na redio zinazosikika nchi nzima, zimetangaza. Hukuwa na muda wa kuambulia lolote?
Emphasis hapo kwenye red.
TV zote kubwa nchini, pamoja na redio zinazosikika nchi nzima, zimetangaza. Hukuwa na muda wa kuambulia lolote?
Emphasis hapo kwenye red.
We jamaa sikujua kama u zezeta kiasi hiki.
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Na wewe mbona una chuki za kijinga?Unadhani watu wote wanaweza kuwa ulipo wewe muda wote!?
Mkuu, tangu mwanzo wa uzi huu umekuwa ukimshambulia mleta mada. Ni dhahiri kabisa una chuki za kitoto na huyu bwana. Katika kuchangia mada si muhimu kujua nani kaileta, bali inahusu nini. Au ni kanuni ipi ya JF inayosema ili u-post mada ndani yake ni lazima uwe mwandishi wa habari? Hukulazimishwa kuisoma na wala kuchangia. Tunaofuatilia mada za JF, tunataka kusoma michango ya GTs na inapobidi kuchangia na siyo unachoki-post wewe, ambacho kinakera sana na kutuondolea umakini wa JF. Samahani kama nimekukera.Umeongea pointi nzuri sana. Nasikia huyu ni mwandishi wa habari? Ni kweli? Kama ni kweli basi kazi tunayo Watanzania, kuwa na wanahabar wa upeo wa huyu...
Umekubali wewe ni muumini mzuri waliberali
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Zimerusha matangazo ya sauti na picha moja kwa moja (live).
Nimeelezea pale nilipom-quote EMT.Na wewe mbona una chuki za kijinga?
Alicholeta manyerere au kilichotolewa na Tume ya warioba ni dibaji na Contents ambazo inshort kama unaishughulisha akili yako unaelewa wazi kile kilichomo.
Kumbuka hili siyo gazeti bali ni thread ambayo Members wengine wataiongezea nyama na kutoa mitazamo yao, nashangaa wewe umemkomalia mleta hoja tu vipi Jombaaa!!
Hi rasimu ya katiba ni kifo cha CCM na sipati picha uko mbele itakuwaje ili CCM waikubali maana wao wapo wengi kwenye vyombo vya maamuzi, hili ni pigo takatifu kwa CCM na wengi walidhani Warioba atakuwa mnafki wa kuibeba CCM kumbe sivyo na hajawasahau kitendo walichomfanyia swahiba yake Salim Ahmed Salim.
Kwa Wazee wenye busara kuna umri mtu akifika anaka kuacha legacy kwenye society na Warioba nadhani hili ndio lengo lake na anajuwa ana miaka mingi zaidi ya kuishi Duniani.
Tanzania kwa maswala ya IT bado nyuma sana.
Tume ya Warioba pamoja na kutengewa mabilioni ya pesa, lakini wanashindwa hata kuajiri mtu/kampuni full time katika kuweka documents muhimu kama rasimu kwenye website yao ili wananchi waisome.
Mkuu, tangu mwanzo wa uzi huu umekuwa ukimshambulia mleta mada. Ni dhahiri kabisa una chuki za kitoto na huyu bwana. Katika kuchangia mada si muhimu kujua nani kaileta, bali inahusu nini. Au ni kanuni ipi ya JF inayosema ili u-post mada ndani yake ni lazima uwe mwandishi wa habari? Hukulazimishwa kuisoma na wala kuchangia. Tunaofuatilia mada za JF, tunataka kusoma michango ya GTs na inapobidi kuchangia na siyo unachoki-post wewe, ambacho kinakera sana na kutuondolea umakini wa JF. Samahani kama nimekukera.
Hakuna cha kushabikia....mabaraza ya Katiba na Bunge la Katiba ndo yataamua mwisho wa Katiba..humu mote CCM ipo na ina majority!!yanayoenda kuiumiza CCM hayatakubalika!..Ni sawa na uwe na ndoto ya kupata watoto mapacha,Ultra Sound ikupe majibu ya mapacha..lakn miscarriage kwa mke ifute ndoto za mapacha...Mabaraza ya Katiba yaliyojaa makada wa CCM Yatawauwa mapacha wa ndoto zetu
Hata mimi nimepita hapo nikakuta hakuna lolote zaidi ya design ya kitoto kitoto.Kwenye presentation yake amesema "Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz"
Lakini hakuna chochote kwenye hiyo tovuti. Hapa pana summary tuu ya alichoongelea: https://dl.dropboxusercontent.com/u/92908476/Speech/Hotuba%20ya%20Warioba,%20Rasimu%20ya%20Katiba%20Mpya,%20June%203,%202013.pdf