Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Mkuu,Wewe umeshaisoma hiyo rasimu na kufanya analysis ya kila kipengele?
Kama umeisoma yote basi tugawie nakala yake ili na sisi tuisome na kuifanyia a comprehensive analysis.
Haya majibu ni kwa malebarali tu!
CCM ni sawa na nyoka bila kumponda kichwa kabisa hafi,hii ni rasimu inaenda kupita kwenye mabaraza ya katiba na bunge la katiba ambapo ccm tayari wameshapenyeza watu wao so lazima tujiandae kuwakabili kwenye hatua hizo wasije kujipenyeza na kuharibu hii rasimu, naamini swala la serikali tatu hawatalikubali, mgombea binafsi hawataki na tume huru hawataki !! kwa vyovyote kazi bado pevu mbele yetu!!Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Mkuu,
Nimeshangaa kwa muda mfupi mwenzetu ameshaisoma na kuichambua hiyo rasimu na tayari amekuja na uchambuzi wa mistari miwili. Kama kweli ameisoma nilitegemea pamoja na mambo mengine, afanye haya:
1. Atuwekee hiyo rasimu ili na sisi tuisome kisha twende sawa katika uchambuzi.
2. Atoe uchambuzi wa kina halafu na sisi tujadili kutokana na huo uchambuzi wake, badala ya kutuletea kikombe kilichojaa maji halafu anatuambia hii ni bahari. Na ukichukulia taaluma/kazi yake, nilitarajia aende mbali zaidi ya hicho alichokiandika.
Mkuu, hapa nilipo tayari ninayo maana nilikuwa Karimjee. Ina kurasa 133 za A4. Kimsingi ina vionjo vitamu sana. Nikipata soft copy naiweka hapa mara moja.
Unadhani watu wote wanaweza kuwa ulipo wewe muda wote!?TV zote kubwa nchini, pamoja na redio zinazosikika nchi nzima, zimetangaza. Hukuwa na muda wa kuambulia lolote?
Hili halina ubishi, CCM ina mtihani mgumu katika hili lakini vile vile litaondoa rushwa iliyokuwa inazidi kuongeza katika chaguzi na teuzi zao. Watakao pelekwa kugombea, watakuwa wasafi kwa vile kule watapambana siyo tu na wagombea wengine kutoka kwenye vyama vingine bali pia na independent ambao wana uwezo kikazi na kifedha.Waungwana pamoja na Mapungufu aliyonayo Manyerere ( kama mlionayo nyinyi ) lakini kwenye hili ni kama mnamuonea tu , hebu twende kwenye ukweli , Wagombea binafsi Ni Tabu zaidi kwa CCM KULIKO CHAMA CHOCHOTE , bado sijajua pale palipo oza hadi Pakanuka ( TUME YA UCHAGUZI ) patakuwaje , nikipata ILE FULL TEXT nitajadili kwa upana .
Tatizo lako umekaa kichama zaidi sema hivi kwa katiba vyama vya siasa vyote vinachangamoto make mtu ataweza kujitathimini akiona anapendwa atakwenda kugombea yeye kama yeye kama yeye bila kutegemea chama.
Pamoja na rasimu kuchukua hoja nyingi za Chadema unafikiri Chadema kimeishiwa hoja, mbona matatizo ya watanzania bado ni mengi tuu.Manyerere kumbuka katiba hii imeteka hoja nyingi za chadema. kui- neutralize hoja ya mpinzani kisiasa ni ushindi pia.
Nchi za wenzetu Ulaya na marekani wanazitumia sana hoja za wapinzani ili wakati wa kampeni za uchaguzi wapinzani wawe na hoja chache dhidi ya chama tawala.
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.