Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,410
Mr Manyerere Kengele ya Ng'ombe inafukuza wanyama ila ndege za Mwarabu zinawafutia wanyama,
sana tu mkuu, CCM kisiki cha mpingo, maneno yote hayo ni hofu.
Mr Manyerere Kengele ya Ng'ombe inafukuza wanyama ila ndege za Mwarabu zinawafutia wanyama,
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Hata mimi nimepita hapo nikakuta hakuna lolote zaidi ya design ya kitoto kitoto.
Cha kushangaza hata waandishi wa habari wetu baada ya kusema hivyo, wangeangalia haraka kupata uhakika na kumrudia na swali lakini wameamini maneno yake peke yake.
Kupata soft copy au kuwekwa kwenye website yao usishangae itachukua weeks.
Na wewe mbona una chuki za kijinga?
Alicholeta manyerere au kilichotolewa na Tume ya warioba ni dibaji na Contents ambazo inshort kama unaishughulisha akili yako unaelewa wazi kile kilichomo.
Kumbuka hili siyo gazeti bali ni thread ambayo Members wengine wataiongezea nyama na kutoa mitazamo yao, nashangaa wewe umemkomalia mleta hoja tu vipi Jombaaa!!
Hi rasimu ya katiba ni kifo cha CCM na sipati picha uko mbele itakuwaje ili CCM waikubali maana wao wapo wengi kwenye vyombo vya maamuzi, hili ni pigo takatifu kwa CCM na wengi walidhani Warioba atakuwa mnafki wa kuibeba CCM kumbe sivyo na hajawasahau kitendo walichomfanyia swahiba yake Salim Ahmed Salim.
Kwa Wazee wenye busara kuna umri mtu akifika anaka kuacha legacy kwenye society na Warioba nadhani hili ndio lengo lake na anajuwa ana miaka mingi zaidi ya kuishi Duniani.
Yaani waondolewe CCM kwa kuonewa then wagawe kura za upinzani how!. Imagine Lowassa afanyiwe mizengwe halafu agombee kama mgombea binafsi unategemea kura za CCM zitabaki zilezile.Kitakachotokea sasa ni kwamba wale watu ambao wana mitandao yao binafsi wakishindwa CCM, au wasiporidhika na utendaji wa CCM, sasa watagombea kama wagombea binafsi na kuishia kugawa kura za upinzani.
Mkuu, ina maana tume haikupendekeza independent candidate kwa chaguzi zote? Mbona Manyerere Jackton ameonyesha kama mapendekezo yako mpaka vitongoji.Mkuu Manyerere,
Kwa mawazo yangu mimi, hili suala la mgombea binafsi lina madhara zaidi kwa upinzani kuliko kwa CCM.
Watu wengi wazuri waliokuwa wanashindwa CCM kwa kuonewa au kwa njama zingine walikuwa wanakimbilia upinzani. Hata wale waliokuwa wanabaki bado wapenzi wao wengi walikuwa wanagoma kumpigia kura mgombea wa CCM na kuishia
kuchagua upinzani.
Kitakachotokea sasa ni kwamba wale watu ambao wana mitandao yao binafsi wakishindwa CCM, au wasiporidhika na utendaji wa CCM, sasa watagombea kama wagombea binafsi na kuishia kugawa kura za upinzani.
Imagine hili lingelikuwepo 2010, huenda leo hii Msigwa na Lema wasingelikuwa wabunge. Watu wengi wa Mwakalebela walimpigia kura Msigwa na hivyo hivyo watu wengi wa Mrema kule Arusha walimpigia kura Lema.
CCM wanalijua hili na ndio maana katika vyama ni wao walipendekeza hili la mgombea huru ingawaje wao walitaka litumike kuanzia chini mpaka ubunge.
CCM ni sawa na nyoka bila kumponda kichwa kabisa hafi,hii ni rasimu inaenda kupita kwenye mabaraza ya katiba na bunge la katiba ambapo ccm tayari wameshapenyeza watu wao so lazima tujiandae kuwakabili kwenye hatua hizo wasije kujipenyeza na kuharibu hii rasimu, naamini swala la serikali tatu hawatalikubali, mgombea binafsi hawataki na tume huru hawataki !! kwa vyovyote kazi bado pevu mbele yetu!!
Chama kina utaratibu wa kukua na kubadilisha mifumo yake inayotumika katika kujiendesha lakini kwa sasa pamoja na kele zote hizi za upinzani bado CCM ni imara labda huko baadae.
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Hebu tuombe radhi kwanza kabla hujajibu maswali nyangu machache.......Kifo cha CCM kinatokea wapi kwenye hii rasimu?.
Kama chagizo ni independent candidate, CCM ndiyo walipendekeza hili kwenye mapendekezo yao kwa tume.
Kwa serikali tatu, CCM hawakuwa na jinsi na katika kolido za kiutawala, kwao hili ni ushindi kwa sababu mzimu wa Mwl. Nyerere wamepata njia ya kuutua.
Tume ya uchaguzi kuunganishwa na msajiri wa vyama lilikuwa ni obvious lingetokea kulingana na demokrasia za nchi nyingi za Africa.
Kama ni kufa basi lazima itakuwa imekufa zamani lakini siyo kwa hili kwa sababu haya karibia yote ni mapendekezo ya CCM.
Mbona watu mnajivua uelewa au memory?
Yaani waondolewe CCM kwa kuonewa then wagawe kura za upinzani how!. Imagine Lowassa afanyiwe mizengwe halafu agombee kama mgombea binafsi unategemea kura za CCM zitabaki zilezile.
Mleta mada mwenyewe kaileta kinafiki tu na ndiyo anapata mashambulizi, badala aongelee rasmu yenyewe anaanza kutaja vyama, mbona hakusema rasimu hiyo itakifufua chama gani kama itaua CCM.
Wadau, wale tuliofuatilia vema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, ni wazi kwamba kwa mapendekezo ya rasimu, CCM inakufa. Kuruhusu wagombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi Taifa, kunatoa mwanya kwa wanaCCM wengi wasiopenda yanayoendelea ndani ya chama hicho, wawe huru kuamua pa kwenda. Aidha, mapendekezo haya ya Katiba mpya yanaleta utaifa zaidi ya u-chama. Sioni CCM watachomoka vipi.
Sijui wengine mna mtazamo gani.
Wewe nawe unajifanya Mwandishi lakini uandishi wako uko shallow kupita maelezo.
Nyie ndio maripota wa matukio halafu mnajiita wandishi.
Kwa lugha ya kisheria Mzee Warioba amedanganya!!.Bora asingesema kuwa "Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz" unless alikuwa na uhakika kuwa tayari ilikuwa pale.
Hebu tuombe radhi kwanza kabla hujajibu maswali nyangu machache.......
Sera ya serikali 3 ni sera ya chama gani?
hoja ya mgombea binafsi muhasisi ni nani na ninani amekuwa akiipinga kwa nguvu zote mpaka kuitisha Court of appeal full bench?
Ni Ilani ya chama gani Tanzania ambayo ilani yake iliahidi Mahakama ya kadhi? je ahadi hiyo ilitekelezwa? na kama haijatekelezwa kwenye rasimu ya katiba mpya ipo Mahakama ya kadhi? je CCM ina gutts za kuomba kura za waislamu mwaka 2015? wait n see.
CCM sio kwamba wamependa iwe hivyo wamelazimika wakubali yaishe, Waryoba hakuwa rahisi kuyumbishwa kama mlivyotegemea.CCM siyo wajinga wa kujimaliza kirahisi hivyo. They know what they are doing. Kama unapima upepo wa ushabiki wa watu kwenye katiba haina tatizo. Naamini kabisa CCM watakuwa wamefanyia kazi 'Scenarios' zote ambazo wewe unaona zinaweza kuwamaliza na kubuni mbinu za kuikinga. Kama mwandishi ulitakiwa kutafikiti kwa nini CCM wameamua vile na madhara yake wamejipangaje kuyakabili?
Hivi unafikiri kuachia dola ni kazi rahisi sana, tena Afrikaaaaaaaaaa?
Umeongea pointi nzuri sana. Nasikia huyu ni mwandishi wa habari? Ni kweli? Kama ni kweli basi kazi tunayo Watanzania, kuwa na wanahabar wa upeo wa huyu...