Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

nahitahitaji kuanzisha biashara ya juis za matunda,naomba msaada wa mchanganuo na location nzuri
Hii ni Moja ya biashara nzuri mno
.
Unaweza Kuanza kwa kutembeza mitaani au Kwenye maofisi, anza na dumu 2 zenye ladha tofauti, kuna mtu atataka umchanganyie, mwengine atapenda moja zaidi.
.
Pia jitahidi iwe na ubaridi vizuri maana ndio inayopendwa zaidi. .
.
Pia hakikisha usiuze juice iliyolala ili kuepusha mtu kuumwa tumbo.

MAMBO YA KUZINGATIA.

USAFI
Usafi binafsi kwako muuzaji, usafi wa vyombo na mahali unapoandalia juice.
.
SOKO
Soko ni Kubwa, mtaani, masokoni, kwenye maofisi, kwenye Migahawa na shughuli mbalimbali.

BEI
Tengeneza za kuanzia Tsh 500_5000 na zaidi ukijenga jina

MAHITAJI
Blender heavy duty ni zuri zaidi na litadumu, package nzuri, mirija, fridge, maji masafi, chujio, vyombo vinginevyo

TENGENEZA JUICE PENDWA
Juice pendwa ni Maembe, maparachichi, Passion, Ukwaju, Ubuyu, Rosella, juice ya Tende, juice pendwa ya miwa na Smoothies

CONSISTENCY (Usiache)
Fanya kwa muendelezo Mpaka ujenge jina.
.
PANUA SOKO, FANYA KWA UKUBWA.
Usiogope kuomba tenda kwenye Migahawa ya kuwa muuzaji wa juice. Migahawa mingi hawatengenezi juice, wewe nenda waombe kuuza juice kwa wateja wanaonujua chakula.
.
TENGENEZA JUICE KWA ODA.
.
Kwenye sherehe zote omba nafasi ya kutengeneza juice, iwe ni kipaimara au harusi omba nafasi. Kama sherehe ni kubwa omba wakulipe Advance kwanza.
.
Hii ni biashara nzuri unayoweza kuanza sasa na kuanza na kuanza kutengeneza faida.
.
Unatamani kujifunza kuhusu hii biashara kiundani? Kuna vitabu vya jinsi ya kutengeneza aina mbalimbali za juice, mbinu, mauzo na masoko.

........
Mawazo mbalimbali ya biashara pitia page yangu ya instagram ya @kelvinkibenje utashukuru
 
shukurani mkuu,huwa napitia page yako
 
Kiongoz naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara ya nguo za watoto nahitaji sana kuifanya.
Kiongozi naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara ya nguo za watoto nahitaji sana kuifanyaa.
 
Hakuna kazi isiyolipa,kikubwa usimamizi tu.
Lakini kwa mtaji wake,bado kuna vitu hajaweka wazi:
-Makazi vipi(kama analipia kodi,bili za hapa na pale)
-Maisha kwa ujumla(kama mahitaji yote anajitegemea au kama kuna kasapoti, ie anakaa kwa ndugu au mtu).
Kwa vyovyote akianza,kama hana backup,lazima nauli,makolokolo mengine ya kutumia,yakitoka humo,mtaji ule lazima upungue.

Na hakika,mtu kama huyu(kasema yeye,ila ni wengi wanaoogopa lakini wana mawazo kama yake),anahitaji biashara inayozaa kila siku anaiona pesa.
Kama akiweka usomi au aibu pembeni,hakika atatoka.
-kwa kuanzia,afanye survey vizuri. Mahindi ya kuchoma yanalipa.
-kama vipi,ajifunze hata kuchoma mishkaki.

Watu wengi wanapenda kuona wanawake wakithubutu,hivyo wateja kwake ni uhakika. Kwa mtaji huo, hapo anachohitaji chabgharama ni jiko
 
Kimsingi kuna mdada mmoja mwanza pale namfahamu fika maeneo ya greenview anauza msosi from jioni hadi usiku wa saa 5-6. Kulaza 30elfu na zaidi kwa siku wala sj suala la kuuliza ambapo mtaji wake ni vilaki tu. We kalia kulinganisha bajaji ya milion 7 na mtaji wa laki 2. Vocha ya ya 500 lakini faida yake ni ndogo less than 15sh lakini chungwa la 200 ujue faida yake si chinj ya 50sh
 
Inawezekana tena sana tu, tembea uone na ujifunze.
 
Group ambalo huwez changia maon la nn
 
Mkuu mimi hapa ndy nimekua saiv yaan wazo mlilopitisha mwaka 015 wakati mm nipo kidato cha 3 naenda kwenye point hilo group bado lipo hai
 
Biashara gani iliyopo msufini mlandizi kwa alie kaaa pale na kuifanya akafanikiwa na kupata matokeo nisaidieni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…