Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Mkuu.
Naomba msaada Kwa mara nyingine. Miti yangu miwili ya papai imekunja majani na hivyo tofauti na mingine haitengenezi matunda.
Je ni tatizo gani na nitumie dawa ipi?
Ombi hili halijapata majibu na sasa lina maelezo ya ziada.
Majani huwa magumu, kubadilika rangi na kuwa ya njano huku eneo la kileleni mwa mti likipinda.
Majani haya huo kama yaliyoungua Moto.
Ni tatizo gani na nitumie dawa ipi?
 
weka picha, alafu hujasema umelima zao gani
 
weka picha, alafu hujasema umelima zao gani

Mkuu.
Mtandao unasumbua, ninashindwa kuweka picha. Kwa upande wa zao ni mipapai, ukiangalia vizuri utaona hili quote tangu nilivyotuma hapo awali.
Mahitaji mchango wa mawazo ili kesho ikiwezekana nitafute dawa husika.
Najaribu kufikiri tu, je inaweza kuwa ukungu au kuna shida kutoka ardhini?
 
sina uzoefu na papai, ngoja wataalam waje
 
Mkuu.
Mtandao unasumbua, ninashindwa kuweka picha. Kwa upande wa zao ni mipapai, ukiangalia vizuri utaona hili quote tangu nilivyotuma hapo awali.
Mahitaji mchango wa mawazo ili kesho ikiwezekana nitafute dawa husika.
Najaribu kufikiri tu, je inaweza kuwa ukungu au kuna shida kutoka ardhini?
Magonjwa yako mengi sana ndugu yangu ya majani kwa maelezo tu vigumu kupata jibu kamili,ingia infonet biovision ,i search Google kisha chagua crops uchague papaya uende kwenye Magonjwa ulinganishe picha na tatizo lako itakayoelekea leta jina lake nitakutajia dawa au mini cha kufanya

http://www.infonet-biovision.org/PlantHealth/Crops/Papaya
 
Ugonjwa wa kinyaushi unao nyausha nyanya na baadae kukauka unatibiwa na dawa gan?
Kuna minyausho ya aina tatu iko ya bakteria, wa fungus na wa minyoo fundo.
Ziko mbegu ambazo zinavumilia mnyauko ila lazima ujue kwako unao wa aina gani ndio uchague mbegu kwani unaweza kuta inavumilia myauko bakteria ila inapigwa na mnyauko wa fungus (fusarium).
Kingine muhimu lishe ya mmea iwe stahiki kupunguza mashambulizi na muhimu zaidi kuzungusha mazao yaani usilime zao la familia moja kwenye eneo moja kila siku.
 
Habari za leo wakuu, nina miche yangu ya miparachichi imepata ugonjwa wa majani ya juu kabisa yale machanga kujikunja sana, nimechunguza hilo eneo linalojikunja nimekuta kuna sisimizi wengi pamoja kama vijidudu fulani vyeupe,yaani kama pametiwa unga.
Je wajuzi wa mambo haya huu ni ugonjwa gani na tiba yake ni nini kwa dawa za kiwandani na za kienyeji kama zipo?
DSC_0054.JPG
DSC_0053.JPG
 
Habari za leo wakuu, nina miche yangu ya miparachichi imepata ugonjwa wa majani ya juu kabisa yale machanga kujikunja sana, nimechunguza hilo eneo linalojikunja nimekuta kuna sisimizi wengi pamoja kama vijidudu fulani vyeupe,yaani kama pametiwa unga.
Je wajuzi wa mambo haya huu ni ugonjwa gani na tiba yake ni nini kwa dawa za kiwandani na za kienyeji kama zipo?View attachment 652805View attachment 652806
Picha kwangu bahati mbaya hazifunguki ila hao wadudu ni kama wale ambao wanakua kwenye mananasi?
Kama ni hao tunawaita mealy bugs, nimewaza hawa baada ya kutaja kuna sisimizi, sisimizi wanawalinda na kuwasambaza mealy bugs kwahiyo kupambana na mealy bugs hakikisha pia umeteketeza sisimizi kwanza, ziko dawa za sisimizi utazipata kwenye maduka ya dawa za kilimo.
Kwa mealy bug unaweza tumia kuwakwangua maana ukiwatoa tu hapo walipo wanakufa huwa hawamove kwenda popote, maisha yao yote uhama mara moja tu yaani akiwa mdogo kuondoka alipozaliwa kwenda sehemu atakayo kaa ili ale na anasafurishwa na kuchukua lift kwenye migongo ya sisimizi.
Dawa tumia nematicide, actara etc, dawa lazima iwe systemic yaani iingie ndani ya mmea mdudu akila akutane nayo afe sababu kwa juu wameweka nywele dawa hazipiti.
Karibu sana
 
Habari za leo wakuu, nina miche yangu ya miparachichi imepata ugonjwa wa majani ya juu kabisa yale machanga kujikunja sana, nimechunguza hilo eneo linalojikunja nimekuta kuna sisimizi wengi pamoja kama vijidudu fulani vyeupe,yaani kama pametiwa unga.
Je wajuzi wa mambo haya huu ni ugonjwa gani na tiba yake ni nini kwa dawa za kiwandani na za kienyeji kama zipo?View attachment 652805View attachment 652806
Tazama pia ndani upande wa chini ya majani uone kuna nini, kama kuna wadudu piga picha tupia hapa
 
Back
Top Bottom