Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Mambo vp kiongozi. Naomba msaada, nyanya yangu majani yanapata kutu na kukauka,mwisho wa siku mpka mche unaathirika. Naomba nisaidie kujua dawa gani nitumie inisaidie kuzuia hii hali
IMG_2349.JPG
IMG_2353.JPG
 
Mambo vp kiongozi. Naomba msaada, nyanya yangu majani yanapata kutu na kukauka,mwisho wa siku mpka mche unaathirika. Naomba nisaidie kujua dawa gani nitumie inisaidie kuzuia hii haliView attachment 756186View attachment 756187
Kuna botrytis inakula mashina na vikonyo, kuna bacterial spot vidoti kwenye majani na kutu pia kuna baka jani wahi, utakua unapiga sana dawa yenye mancozeb na metalaxyl badili kiuatilifu tumia yenye copper na yenye cymoxanil yaani tumia blue copper na tumia milraz/power 76wp.

Ukiweza kupata othelo top ndio mwisho wa matatizo yote
 
Kuna botrytis inakula mashina na vikonyo, kuna bacterial spot vidoti kwenye majani na kutu pia kuna baka jani wahi, utakua unapiga sana dawa yenye mancozeb na metalaxyl badili kiuatilifu tumia yenye copper na yenye cymoxanil yaani tumia blue copper na tumia milraz/power 76wp.

Ukiweza kupata othelo top ndio mwisho wa matatizo yote

Nashukuru sana kwa ushauri wako kiongozi, ngoja niitafute nikifanikiwa nitaleta feedback hapa
 
Habari, nataka fanya istallation ya drip irrigation heka moja , je naweza lima mazoa tofauti let say nikagawa sehemu nne na kila sehemu nikapanda zao lake, natanguliza shukrani.
 
Habari za shughuli mkuu.Nimesia Vitunguu vina muda wa wiki mbili sasa kwenye kitalu.Naomba msaada kujua dawa gani nitumie ili kutibu ukungu kwenye mimea ..Nitumie dawa gani kuikinga mimea na ugonjwa wa mnyauko??..Msaada wako please
 
Mkuu habari,msaada kuhusu ABC za kilimo cha mtama,choroko na kunde.Napenda kujua jinsi ya ukulima uzalishaji na masoko ya mazao hapo tafadhali.thanks
 
Kwa hiyo system mpaka sasa unapata matatizo gani uliyokwisha kuyaona???

Pilipili ikiwa ndogo yaan wakati umehamishia shambani inataka phosphate ili ikuze mizizi,hii inapatikana kwenye DAP,MAP (ya drip) na NPK. Vyema kutumia DAP sababu ina Phosphate nyingi zaidi ya zote.

Kukuzuia mmea unataka zaidi nitrate hii inapatikana kwenye CAN,UREA,S.A,NPK,DAP etc. Vyema kutumia CAN au NPK sababu inakupa nitrate kabisa nyingine zinakupa Ammonium,DAP haifai sababu ina Ammonium kidogo sana ndio maana huwa tunapandia tu. UREA nzuri pia lakini jua ukiiweka inaanza kufanya kazi baada ya siku 18 na inakirutubisho kimoja tu,S.A inatabia ya kubadili udongo sababu ya Sulphur ila kwa pilipili unaweza kua na advantage ukiitumia kwa kuzalisha pilipili kali zaidi(sulphur ndio ile harufu ya ukali ya pilipili)

Wakati wa mmea kutoa maua na matunda unataka zaidi calcium na potassium ili kutoa maua,kuzuia maua yasidondoke,kutoa matunda,kutengeneza ngozi ya tunda,na kutengeneza Mbegu. Hivyo hapa unaweza tumia CAN,MOP au NPK. Sasa CAN ina nitrate na calcium,MOP ina potassium pekee na NPK ina nitrate,phosphorous na potassium. Utaona kupata madini mawili ya stage hii lazima utumie mbolea mbili sasa ukitumia CAN na NPK utaona una double nitrate hivyo mmea utakua zaidi hautajua unatakiwa uzae sasa,hivyo vyema kutumia CAN na MOP sababu utapata calcium,nitrate na potassium.

Kuhusu kuchanganya the more the better,calcium inatabia ya kureact na madini mengine but hiyo ni text book situation ambapo tunachukulia one element plus one element,ukija kwenye reality ukichanganya CAN na MOP inamaana mchanganyiko wako unakua na calcium,nitrate na potassium plus carrier materials sio rahisi kureact sababu haziko sehemu moja unaweza kuta mop zimekaa zenyewe au calcium zimekaa zenyewe so hiyo theory imeprove failure.

Karibu sana
Pia vipi kuhusu zile pilipili ndogo nyembamba nimeona u tube na nikavutiwa nazo kuzilima.Unaziotesha kwenye kitalu na transplant au unapanda mbegu moja kwa moja.pili unaweza Lima msimu wa mvua au ni za kumwagilia? Thanks
 
Back
Top Bottom