Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Manyara-Hanang, ekali inategemea bei ya kukodi ni elfu 50 mpaka laki, gharama za kulima ni elfu 40 kwa eka

''Aut Vincere Aut Mori''
Yes... Hanang nasikia ni maarufu kwa kulima ngano. Hata huku Arusha kuna mahala nilienda nikakuta kuna mashamba ya ngano, ni kwamba ardhi yake inakubali. ila bado sijajua mchanganuo wake uko vipi katika kilimo.
Kilimo cha ngano ni moja aina za kilimo ninazotiizamia kuja zifanya kwa kiwango kikubwa sana siku za usoni maana asilimia kubwa ya ngano tunayotumia inakuwa imported hasa kutoka nje kama vile Africa Kusini na huko pia bado wanaimport...so ukizungumzia ngano unazungumzia soko kubwa sana maana mahitaji yake ni makubwa.

Kila siku watu hutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa ngano:maandazi,mikate,keki,chapati, na hata viwandani ngano hutumika kuzalishia vinywaji kama bia.

Kilimo cha ngano si cha kudharau hata kidogo...
bado nakitafutia taarifa za kutosha ili nianze kulima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu.
Lakini naomba ufafanuzi kidogo, niweke ya ng'ombe au mbuzi kisha niweke hizo nyingine? Kwa kipimo gani? Nina miti yenye miezi manane na mingine ina mwaka na nusu.

Ya ng'ombe au mbuzi ukiweza weka ndoo moja kila mmea kwa kuzungusha umbali toka shina ni nusu ya upana wa jani au tawi.
Ya kiwandani zungusha gm 50 mpaka 100 kwa kila mmea
 
the horticultutist naomba unisaidie ratiba ya utunzaji wa miti ya miembe ya kisasa eg.ukishapanda unatumia lets say samadi, then itakubidi after muda gani uweke mbolea lets say ya kukuzia nk, nk, maana ni muda mredu, yani nisaidie ratiba nzima hadi mvuno wa kwanza.asante
 
naomba kufahamu Mbolea au aina ya Mbolea itumikayo wkt tikiti ikitoa maua, tikiti ina mwez

Kwenye kipindi cha maua unahitaji madini ya potassium ili itoe maua na madini ya calcium ili isidondoshe maua na kutengeneza ngozi ya tunda.
Hivyo weka npk haswa yara winner ili ikupe micro nutrients pia wiki hii then next week weka CAN ya yara pia tumia yaraliva nitrabor
Njia ya pili chukua ya MOP na CAN weka uwiano wa 2:1 yaani mop gm 10 can gm 5 kwa kila mche. Gm 5 ni kifuniko kimoja flat cha chupa ya maji au soda ya take away
 
the horticultutist naomba unisaidie ratiba ya utunzaji wa miti ya miembe ya kisasa eg.ukishapanda unatumia lets say samadi, then itakubidi after muda gani uweke mbolea lets say ya kukuzia nk, nk, maana ni muda mredu, yani nisaidie ratiba nzima hadi mvuno wa kwanza.asante

Huo ni mti samadi inatosha pandia na utakua ukiweka kwa kuzungushia mche wako mbolea za kiwandani haziwezi kukisaidia sana kwa info zaidi cheki hapa pia.
http://www.infonet-biovision.org/PlantHealth/Crops/Mango
 
Habari wana jukwaa!!

Nategemea kuingia kwenye kilimo cha ngano hivi karibuni. Naomba tusaidiane kujua changamoto mbalimbali pamoja na masoko. Farming techniques nzuri ilikupata more yield per hectre na mengine mengi. karibuni tujuzane kuhusu Kilimo cha ngano.
 
Badilisha mbolea tumia ya ngombe au ya mbuzi ,pia weka mbolea ya npk this week baada ya wiki moja weka mbolea ya can utaona matokeo

Mkuu, nimerejea kutoa mrejesho.
Siku hiyo hiyo ya Aug 17 Niliweka Mbolea aina ya NPK Kwa kipimo cha gramu 30 Kwa kila mti.
Baada ya wiki Niliweka CAN Kwa kipimo hicho hicho huku nikiendelea na ratiba yangu ya kumwagilia.
Jioni hii nimeanza kuona mabadiliko, miti mingi imeanza kuweka matunda! Natumaini hayatadondoka kama hapo awali.
Ninatarajia kuongeza gram nyingine 30 za mbolea ifikapo mwezi oktoba.
Natanguliza shukran.
 
Mkuu, nimerejea kutoa mrejesho.
Siku hiyo hiyo ya Aug 17 Niliweka Mbolea aina ya NPK Kwa kipimo cha gramu 30 Kwa kila mti.
Baada ya wiki Niliweka CAN Kwa kipimo hicho hicho huku nikiendelea na ratiba yangu ya kumwagilia.
Jioni hii nimeanza kuona mabadiliko, miti mingi imeanza kuweka matunda! Natumaini hayatadondoka kama hapo awali.
Ninatarajia kuongeza gram nyingine 30 za mbolea ifikapo mwezi oktoba.
Natanguliza shukran.

Karibu sana ndugu yangu
 
Mkuu.
Naomba msaada Kwa mara nyingine. Miti yangu miwili ya papai imekunja majani na hivyo tofauti na mingine haitengenezi matunda.
Je ni tatizo gani na nitumie dawa ipi?
 
Karibu sana,hapo kwa nyanya ni kwamb tunapanda mistari miwili kwenye tuta moja,inakua nyanya hadi nyanya ndani ya mstari mmoja ni 40sm,nyanya mstari mmoja hadi mwingine kwenye tuta moja nayo ni 40 halafu 150 ni mstari wa tuta hadi tuta ndugu
Katika mkoa wa mbeya ni wilaya gani hulima zao LA karanga?
Nataka kulima hili zao kibiashara.
Na ni mbegu gani hustawi vizuri?
[HASHTAG]#ubalikiwe[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom