Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Mtaalam
nakusalim sana..kuna mdau mmoja nnlikua napitia comments kauliza kua mbegu ya kitunguu anzia siku ile ya kusia,,inatakiwa ikae siku ngapi kwenye kitalu ??

Pia naomba kufahamishwa kua hivi kitunguu huwa kinapigwagwa buster??
Kitunguu kina siku 45 kwenye kitalu ,booster ndio ziko za kupiga kwenye kitalu seedling starter yenye npk ratio ya 19-19-19, na shambani utapiga booster yenye boron na sulphur kama utakua hujatumia yara winner (npk) ,maana urea na can hazina sulphur wala boron na ni muhimu sana kwa kitunguu
 
Kitunguu kina siku 45 kwenye kitalu ,booster ndio ziko za kupiga kwenye kitalu seedling starter yenye npk ratio ya 19-19-19, na shambani utapiga booster yenye boron na sulphur kama utakua hujatumia yara winner (npk) ,maana urea na can hazina sulphur wala boron na ni muhimu sana kwa kitunguu

Aloo asante sana mkuu..
hii yara winner ni kitu gani hiki??
 
Mara ngapi naweza kuvuna,hlf matumizi ya mbolea,naweka mara ngapi?umwagiliaji naweza kumwagilia hata mchana wa jua kali?
 
Itanigharimu kiasi gani kuandaa hadi uvunaji shamba LA alizeti ukwa heka moja? Nakusudia kulima heka kumi
 
kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo cha mboga,matunda,maua,viungo na dawa.Wataalam na wakulima tukutane hapa
Nipo Igunga nimepanda miche mitano ya zabibu aina ya table kwa ajili ya matumizi ya familia ninapenda kujua namna ya matunzo hadi kuanza kuvuna,namna ya kuzikatia na kama kuna aina gani ya hormones za kupulizia kusaidia bud bursting
 
Je KIPINDI hiki cha mvua za mchoo na vuli naweza kukima nini maeneo ya MKURANGA?muhogo,mahindi vipi?
 
Mkuu naomba kujua mimea kama pilipili hoho, ngogwe na pilipili mbuzi zinahitaji maji kiasi gani kwa wiki kwani nataka nipunguze kubeba ndoo nataka niweke makopo so nikipata kiasi cha maji kwa wiki kwa mimea tajwa utakuwa umenitua ndoo,.
 
Habari wakuu???

Naomba kujua yafuatayo ;
1.Sehemu ngano inakolimwa kwa wing km hekari 200 ivi
2. Gharama za kulima kwa hekari
3.Ardhi wanakod bei gan kwa hekari
4.Faida na changamoto zake...

NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manyara-Hanang, ekali inategemea bei ya kukodi ni elfu 50 mpaka laki, gharama za kulima ni elfu 40 kwa eka

''Aut Vincere Aut Mori''
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom