Kwa laki moja tu unapata driving licence

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,791
Reaction score
830,944
Tanzania mahali pazuri mno pa kuishi hata kama huna ujuzi wala elimu yoyote almradi tu uwe na shekeli kidogo, unahitaji chochote utapata iwe kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini, hati ya kusafiria vyeti vya shule, chuo nk! lakini fungakazi ya yote ni leseni za udereva, karibia kika mgeni anamiliki leseni na ukienda kwenye database ya POLISI na TRA utakuta wametimiza vigezo vyote, ila katika uhalisia si kweli. vijana wengi wa bodaboda wanazo leseni lakini hata mlango wa chuo cha udereva haujui. uzalendo umetutoka kabisa kila mtu anaangalia anapata bei gani kwenye nini! na kwa njia hii tunaimaliza nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe
 
Hahaaa trafic elf 20, pale TRA elfu 40, kishoka elf 20 umemaliza.
 
Mkuu biashara hiyo imeshamiri pale Mayfair Plaza Mikocheni,hadi kwa shs 80,000/= unapata tena siku hiyo hiyo kama ukienda saa 2 asubuhi au Kesho yake tayari una ganda,pale bwana hadi vyoo vyao vinanuka rushwa maana watu wanakula na kuny.a rushwa kwa kwenda mbele!!!
 
mkuu kuna mambo mengi mno siyo leseni peke yake,.
 
Yes, fungulia nyuzi uyaanike, ni njia mojawapo ya kufikisha ujumbe, huyu aliyeleta hii mada kajikita kwenye leseni za udereva.
 
mshana jr, nitampa mtoto wangu jina lako kwa kuwa tu UNAWAZA KAMA MIMI, I can see my self in you
Tanzania mahali pazuri mno pa kuishi hata kama huna ujuzi wala elimu yoyote almradi tu uwe na shekeli kidogo, unahitaji chochote utapata iwe kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini, hati ya kusafiria vyeti vya shule, chuo nk! lakini fungakazi ya yote ni leseni za udereva, karibia kika mgeni anamiliki leseni na ukienda kwenye database ya POLISI na TRA utakuta wametimiza vigezo vyote, ila katika uhalisia si kweli. vijana wengi wa bodaboda wanazo leseni lakini hata mlango wa chuo cha udereva haujui. uzalendo umetutoka kabisa kila mtu anaangalia anapata bei gani kwenye nini! na kwa njia hii tunaimaliza nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Mzizi wa matatizo yote ni CCM

Na mfumbuzi wa matatizo ni CCM.

Imagine ingekuwa Serikali ya chadema, ikiwa Mwenyekiti anampigia simu hawara ageuze na aache safari ya kikazi aelekee Dubai kula bata badala ya kazi aliyotumwa na bunge, tena kwa gharama za bunge. Ingekuwaje?

Waswahili tuna msemo, aheri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Chini ya utawala wa CCM hakuna kisisichowezekana
 
Trafick wote ni wahasibu huru,wana uwezo wa hari ya juu katika kukusanya mapato yasiyo rasmi.
 
Na mfumbuzi wa matatizo ni CCM.

Imagine ingekuwa Serikali ya chadema, ikiwa Mwenyekiti anampigia simu hawara ageuze na aache safari ya kikazi aelekee Dubai kula bata badala ya kazi aliyotumwa na bunge, tena kwa gharama za bunge. Ingekuwaje?

Waswahili tuna msemo, aheri nusu shari kuliko shari kamili.

Faizafoxy waweza kuwa sahihi ukilenga individuals, lakini tukiongelea taasisi kwakweli CCM lazima iondoke sasa, tusifike mahali ilipofikia Zimbabwe! Tunahitaji mbadala wa CCM n this must be very soon before it is too late! deni la taifa linazidi kupaa, maisha yanazidi kudidimia huku kuna kilinge cha wachache wanaishi kwenye ukwasi wa kutisha, tunajiandalia bomu la nuklia
 
Tatizo kubwa la CCM ni upinzani mbovu.

Upinzani ukiwa na nguvu hutayaona yote hayo.

Bili kuwa na upinzani wa kweli na wenye nguvu, tukubali matokeo.

Mtakazana CCM mbovu wakati wao ndio chama pekee chenye ushawishi kwa wananchi walio wengi, unategemea nini?

Fikiri kwa rekodi ya Slaa ni nani mwenye akili timamu atamchaguwa kuwa Rais? Unataka tuongozwe na mtu hata maadili ya Kanisa lake alilosomea kanuni zake ameshindwa kuzihimili.
 
Ni sawa Faidha lakini bado naomba tujikije kwenye taasisi na system nzima hawa viongozi wa CDM ni individuals, hizi chuki dhidi yao tuziweke pembeni kwanza ili tuweze kushiriki kwa undani kile tunachokijadili
 
Back
Top Bottom