Rais Samia Suluhu Salamu zako kwa bodaboda

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,553
2,992
Habari!!

Ndugu zangu katika Mipaka hii ya jamhuri ya muungano mimi ni mwananchi mwenzenu ambaye ni mkazi wa jiji la dar es salaam ila heka heka zangu zinanipeleka muda mwengine visiwani na baadhi ya mikoa na kwasasa nimerudi tena dar es salaam.

Uwepo wangu katika jiji la Dar es salaam kwa hivi sasa kumenifanya nimuandikie uzi Rais wa Jamhuri ya Tanzania yeye akiwa kama muwakilishi wa Boda Boda,Wamachinga na Wafanyabiashara katika nchi yetu ikiwa pamoja na chama chake cha siasa kimebeba Uhusika mkuu wa Itikadi ya wavuja jasho(Wakulima na Wafanyakazi) hivyo naamini uwepo wa Chama chake ni kiashirio tosha kuwa Mawazo na Malalamiko yang yatakuwa yenye kuonwa na kutiliwa mkazo.

Ndugu Rais wa Jamhuri ya muungano licha ya kujitambulisha ukazi wangu ila niongezee kusema kwamba mimi ni Muhitimu wa shahada ya sanaa kutoka chuo X ambaye nimejiari kupitia biashara ya chombo chenye kutumia maringi mawili maarufu bodaboda, hivyo katika Kuandika Uzi huu nimevaa kofia 2 moja ni Muhitimu wa shahada na pili bodaboda jijini dar es salaam.

Ndugu Rais wa Jamhuri ya Tanzania, mimi bodaboda nakuomba kwa ridhaa yako utafute namna ya upendeleo kwetu kutupunguzia gharama za usajiri/ukataji wa leseni kwani imekuwa changamoto mno kwetu,na inatufagharimu muda mwingi mno kushinda vituoni kuliko kufanya kazi muhimu katika Taifa letu,na kama itakupendeza kutumia mfumo wa vitambulisho kama ilivyokuwa awamu ya tano kwani itakuwa inapunguza gharama na muda wa kuzunguka hovyo kwenye hati za udereva.

Mwisho naomba yazingatiwe maoni yangu kama Raia Mwema wa Taifa hili.

MHAFIDHINA
 
Back
Top Bottom