Bima ya Afya kwa wote ni kitanzi kwa CCM

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,213
3,598
Huu mpango wa Bima ya Afya kwa wote ni kitanzi kwa wananchi na CCM kuliko hata Pembejeo zilivyo.

Jinsi mpango huu ulivyotengenezwa naona kabisa dhahir shahir unaenda kuwa kama mikopo ya elimu ya juu ambapo maskini ndiyo wataambiwa walipe halafu fungu walilotengewa kulipiwa maskini litatumika kulipia matajiri na wenye uwezo wa kujilipia. Huu unabii mtaukumbuka utapotimia, vuteni subira.

Bima hii, maskini akiishabaguliwa, kama ilivyokuwa kodi ya kichwa ya maendeleo, watu (maskini) watakimbilia porini kujificha wasikamatwe kwa sababu sheria yake imeifanya kuwa lazima kwa kila mtu.

Kundi kubwa la watu litapoteza haki zao za msingi na za kikatiba, mfano usipokuwa na Bima ya Afya hupati vifuatavyo:-

1. Kadi ya NIDA (utapoteza uraia wako)

2. Leseni ya Udereva (utapoteza ajira)

3. Kudahiliwa kidato cha 5 (wajinga wataongezeka nchini)

4. Usajili wa BRELA (wigo wa kodi nchini utapungua na kupunguza mapato ya serikali)

5. Hati ya kusafiria nje ya Jamhuri (hutosafiri kwenda masomoni ughaibuni, kutembelea ndugu na marafiki, kuhudhuria mikutano, kufuata biashara, kutalii na kutibiwa ughaibuni)

6. Ajira (hutoajirika na uhalifu utaongezeka nchini)

Nk nk nk

Maadui 3 wa taifa (ujinga, maradhi na umaskini) watapandisha bendera zao za ushindi juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro na juu ya paa za kila kaya nchini kuashiria wamefanikiwa kuteka nchi.

Iile bundle la Toto Afya lilikuwa 50,000/ sasa limefutwa na kuwa 350,000/, ebu fikiria baba yako kule Kijijini ana wake 5 kila mke mmoja ana watoto wadogo 3 jumla 15 mara 350,000/ = 5,250,000/ ÷ kwa 200,000/ bei ya ng'ombe mdogo basi babako kwa mwaka atatakiwa kuuza ng'ombe 26 kulipia Bima ya watoto tu (bado tegemezi wake wakubwa) ambayo hii ni kununua umaskini kwa sababu kila mwaka atakuwa anauza ng'ombe 26 plus kulipia Bima ya Afya ya watoto tu, huku wewe pia ulisomea mkopo wa serikali bado unapambana kulipa (makato makubwa) na unatakiwa ukatwe na Bima ya Afya pia.

Baba yako anakutazama umsaidie na wewe unamtazama akusaidie, mnatazamana.

Nchi yetu inabuni mipango mizuri kisayansi (kitaalam) lakini inatekeleza mipango ya kitaalam kisiasa.

Mfano TAHLISO inatangazia wanachuo wenye umri wa miaka 18 kuendelea kutafuta kitambulisho cha NIDA ili kitumike kama mbadala wa kadi ya Bima ya Afya wakati upatikanaji wa kadi ya NIDA yenyewe hauwezekani kwa zaidi ya asilimia elfu moja.

Tupo tulioomba ID za NIDA mwaka 2018 hadi leo miaka 5 hatujazipata. Juzi nafuatilia naambiwa hawajui kwa uhakika lini zitapatikana.

Yaani ningekuwa ni mwanachuo maana yake ni kwamba ningeomba ID hiyo na ningekuwa nimeishamaliza chuo (miaka 3 hadi 5) sijapata ID na hivyo basi ningekosa fursa ya hicho kifurushi cha bima kwa wanafunzi wa vyuo vinavyohudumiwa na TAHLISO.

Kwanini usiamini Bima ya Afya ni kitanzi kwa CCM na wananchi kuliko hata pembejeo?

Kwanini usiamini kwamba ili CCM iwe salama 2025 (isilazimike kucheza rafu kwenye masanduku ya kura) ingesubiri uchaguzi upite salama kwanza ndiyo serikali yake ije na mpango wa Bima ya Afya kwa wote?

Vinginevyo CCM itapata ushindi wa machozi maana serikali yake itakuwa imeleta zimwi (Bima ya Afya kwa wote) kukusanyia ela za chaguzi labda.

Kubuni jambo na kuparamia kulitekeleza ni rahisi sana maana inahitaji tu makofi ya Wabunge, lakini kulitekeleza kwa uzoefu wa historia ya Tz ni majuto tupu, ni msiba mkuu, ni kufukuza utajiri mdogo wa wananchi na kukaribisha umaskini mkubwa kwao (unabadilisha umaskini kwa utajiri kama watani zangu Wakwere wanaouza nanasi kununua mua).

Kimsingi ieleweke kwamba sipingani na mpango huu ambao ndiyo muelekeo wa dunia ya sasa kwenye tasnia ya afya, tena mimi natamani sana mpango huu ungeanza tangu awamu ya pili ya safu ya nchi yetu, ninachopingana nacho ni UTUMISHI WA MAZOEA KATIKA KUTEKELEZA MPANGO HUU; UNAOLETA MADHARA KWA JAMII KWA MAMBO YANAYOGUSA UHAI WAO, USTAWI NA MAENDELEO YAO NA KUTWEZA TASWIRA NZURI YA TAIFA LETU.

Unawapaje watumishi waliofeli mpango nyeti kama huu wautekeleze? Wamefelisha mpango wa kwanza uliokuwepo (NHIF), unawezaje kuuhakikishia umma kwamba mpango huu mpya wa Bima ya Afya kwa Wote wataufanikisha kwa mindsets zile zile?

Aidha, naichagiza serikali kuingiza kwenye kanuni za sheria ya Bima ya Afya kwa wote ili gharama za kuhifadhi na kutoa maiti nazo ziingizwe kwenye bima hiyo. Kuwa na bima ya kuhudumia ugonjwa tu bila kuhudumia maiti ya mgonjwa anapokufa ni sawa na kuwa na ugali unaolika kwa mboga moja tu huku hauliki kwa mboga nyingine alafu ukaridhika eti una chakula huwezi kulala njaa.

Hapa si Bunge limedanganywa? Umma si umedanganywa? CCM si kimechonganishwa na wapigakura?

Tutashuhudia Mifuko binafsi ya Bima za Afya zikinawiri huku Mfuko wa serikali wa Bima ya Afya ukifa kwa ufisadi na utendaji wa mazoea kwenye mazingira ya soko moja hilo hilo.

Hali hii ndiyo natabiri inaenda kulikumba TRC baada ya SGR kuanza kazi. Namshauri Mhe. rais apeleke muswada wa sheria Bungeni kutenganisha TRC kuwa mashirika mawili ya:-

1. TRC kwa ajili ya reli ya MGR.

2. Shirika lingine kwa ajili ya reli ya SGR.

Na

3. TAZARA iendelee kubaki kwa ajili ya reli ya CGR.

NB.
Aidha, ninaamini mgodi mmoja wa nchi hii ungetosha kulipia raia 61+ml Bima ya Afya na mikopo ya elimu ya juu kama tungekuwa na wataalam wazuri wa mipango na usimamizi wa tija wa migodi yetu.

Kama tamu meza kama gwadu tema.
 
Bima ya Afya kwa wote haitofanikiwa kwa sababu ipo kisiasa zaidi.

Lengo la kuanzisha bima ya Afya kwa wote ni kuokoa mfuko wa bima ( NHIF) na sio kusaidia jamii. Na hili ndio litasababisha mpango wao kufeli vibaya.

Kitu kingine kitakacho leta fujo ni watu wasiostaili kulipiwa watalipiwa kwa sababu tu ni wanaccm au wanamtandao ( hili ni kawaida kwa ccm mfano 10%ya halmashauri)

Wamefanikiwa kwa KIKOKOTOO kwa sababu ya ubabe wao ila kwa BIMA YA AFYA KWA WOTE kamwe hawatofanikiwa.
 
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama mambo yenyewe mdio hayo ya kunyimwa hadi passport basi ni kheri nikabadili uraia mapemaa tu maana lwanza hapa watawwla wenyewe wamesha fail
 
Back
Top Bottom